Home » » Wanafunzi wa kike ikuwo sekondari MAKETE NJOMBE wanalala chini‏

Wanafunzi wa kike ikuwo sekondari MAKETE NJOMBE wanalala chini‏


 Wanafunzi wa kike wa Ikuwo sekondari kwa sasa wanalala hapa kama ilivyoshuhudiwa na mtandao huu.
 kama kawaida wamepanga magodoro yao chini kwa raha zao
 Mkuu wa shule ya Ikuwo Sekondari akifafanua jambo kwa mwandishi wetu.
=====

Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana na idadi ya wanafunzi wengi wa kike wilayani Makete mkoani Njombe kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba, shule ya sekondari Ikuwo imeonesha kukerwa na tatizo hilo na kuamua kuchukua hatua za awali za kupambana nalo

Mwandishi wa mtandao huu alifika shuleni hapo na kukuta wanafunzi wa kike wote wakiwa wanalala shuleni hapo licha ya mabweni hayo kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa vitanda

Mkuu wa shule hiyo akizungumza na mwandishi wetu amesema kutokana na tatizo hilo kuzidi kuwa kubwa, uongozi wa shule na wilaya kwa ujumla walikubaliana wanafunzi hao watandike magodoro sakafuni waendelee kulala mabwenini humo, wakati serikali ikiendelea kutafuta vitanda kwa ajili ya mabweni hayo

"Kwa wakati huu ambao tunasubiri kuletewa vitanda na serikali, tumeona ni bora wanafunzi hawa wa kike waendelee kulala chini kwa kutandika matandiko yao ili kupunguza ukubwa wa kupata mimba pamoja na kufeli" alisema mwalimu mkuu huyo

Mtandao huu ulipenya kwenye mambweni hayo na kushuhudia magodoro yaliyotandikwa kwa unadhifu wa hali ya juu, ambapo wanafunzi hao wanalala kwa muda wakisubiria vitanda

Hivi karibuni katika mahafali ya kidato cha nne Iwawa sekondari afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena alikaririwa akisisitiza wanafunzi wa kike wa shule hiyo waanze kulala shuleni kuanzia mwakani hata kama mabweni hayana vitanda kama wanavyofanya Ikuwo sekondari

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa