Njombe.Uchangiaji mdogo wa halmashauri katika
sekta ya afya kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani, umeelezwa kuwa
miongoni mwa changamoto zinazovikabili vituo vingi vya kutolea huduma ya
afya.
Hayo yalisemwa juzi na Mratibu wa Ukimwi katika
Halmashauri ya Mji wa Makambako, Dk. Margreth Msasi, alipokuwa
akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya Tokomeza Maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda mtoto.
Dk Msasi alisema hali hiyo inachagiza utekelezaji
wa mpango wa kuzuia maambuki ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto.
Alisema changangamoto nyingine katika utekelezaji wa mpango huo ni ukosefu wa dawa katika Bohari Kuu ya Dawa.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment