MKUU WA WILAYA YA MAKETE AFANYA KIKAO CHA MAENDELEO NA WANAMAKETE WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM‏


 Mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.

Wananchi waliozaliwa wilayani Makete mkoani Njombe ambao wanaishi nje ya wilaya hiyo, wameshauriwa kuipenda wilaya yao kwa kuja kuwekeza pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya wilaya hiyo

Rai hiyo imetolewa hii leo na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika kikao baina yake na wananchi wa Makete waishio jijini Dar es Salaam kilichofanyika jijini humo
Katika kikao hicho mkuu wa wilaya amewashirikisha mambo mengi ya kimaendeleo katika wilaya ya Makete ikiwemo uwepo wa shule ya sekondari ya wasichana ya Makete Girls secondary ambayo pamoja na kuanza kufanya kazi bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali

Mh. Matiro amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bweni na kuwa wanafunzi wanalala kwenye vyumba vilivyojengwa kwa ajili ya madarasa, bwalo, jiko pamoja na maabara ambavyo vinatakiwa viwepo

Amewaomba wananchi hao kuunga mkono kwa jinsi Mungu alivyowajalia na kwamba yeyote atakayejisikia kuchangia anaombwa kufanya hivyo kwani kila mmoja kwa nafasi yake ana mchango katika shule hiyo ili iondokane na changamoto hizo
"Ndugu zangu wilaya yetu inawatambua sana. tunaomba na tunahitaji sana ushirikiano wenu katika maendeleo ya makete, tukishirikiana kwa pamoja kwa kadri Mungu alivyotujalia kwa hakika shule hii itaimarika sana" amesema Matiro

Kwa upande wao washiriki wameoneshwa kufurahishwa na maendeleo ya kasi katika wilaya ya makete huku wakiipogeza serikali kwa juhudi zake za maendeleo hasa katika elimu, barabara, umeme pamoja na mambo mengine huku wakisema wataunga mkono maendeleo ya wilaya yao kwa kadri ya uwezo wao
Pia wameonesha kufurahishwa na Mh Matiro kuwatafuta na kuzungumza nao kwani wamesema amekuwa mkuu wa wilaya wa kwanza kuzungumza nao toka wilaya hiyo imeanzishwa na kumtaka kuwa na moyo wa kuipenda wilaya ya Makete kama mkuu wa wilaya
 Wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya.

Baada ya kushirikishwa hivyo wameahidi kushirikiana na mkuu huyo wa wilaya kutatua changamoto hizo.


Na Edwin Moshi, Dar es salaam
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WATENDAJI NJOMBE KUTUMIA VEMA BARAZA LA BIASHARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WATENDAJI wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa Baraza la Biashara la Mkoa kuunganisha sekta ya umma na binafsi kujadili kutatua changamoto zilizopo katika biashara na kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya biashara zilivyopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Mkurugenzi wa Biashara wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Arthur Mtafya, alisema wajumbe wa baraza hilo hawana budi kuzingatia fursa za uchumi zilizo katika mkoa huo na kujadiliana juu ya vikwazo vya biashara, ili kupanua wigo wa uwekezaji mkoani humo.
“Nia ya kuanzisha baraza katika ngazi ya mkoa na wilaya ni kurahisisha utendaji kutoka ngazi ya taifa mpaka wilayani, kwani kuna mambo yanayoweza kushughulikiwa katika ngazi ya mkoa,” alisema.
Mtafya alisema sera za nchi zinaruhusu baadhi ya changamoto zinazohusu mkoa fulani zitatuliwe katika ngazi ya mkoa na kwamba hiyo inasaidia utendaji na uwajibikaji na kuwa yanaposhindikana ndipo huwasilishwa katika ngazi ya taifa, ili kufanyiwa kazi. Alisema ushiriki kamilifu wa sekta hizo mbili katika ngazi ya mkoa na wilaya utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuinua hali ya biashara na uwekezaji katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kapteni Mstaafu Asei Msangi, alisema baraza hilo jipya litakuwa chachu ya maendeleo kwa kuunganisha sekta ya umma na binafsi katika kujadili vikwazo vya biashara, ili kukuza uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Chanzo:Tanzani Daima 

MABINTI PACHA WALIOUNGANA KUHITIMU KIDATO CHA NNE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

HATUA ya kwanza ya ndoto ya kuzama katika elimu ya mabinti pacha walioungana kiwiliwili, Consolata na Maria Mwakikuti (18) wa Kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoa mpya wa Njombe, inatarajiwa kutimia Novemba mwaka huu, wakati mabinti hao watakapofanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.
Itakumbukwa kwamba walipokuwa wakimaliza elimu ya msingi mwaka 2009 kijijini kwao Ikonda, walikuwa na umri wa miaka 13 na katika ndoto zao kwa pamoja walisema wanataka kuwa wasomi waliobobea katika utaalamu wa kompyuta.
Lakini, kwa sasa, wanasema wanatamani kufanya kazi ya Ukatibu Muhtasi. Wanafunzi hao ambao mwaka 2010 walichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, Dar es Salaam.
Kwa sasa wanasoma katika Shule ya Sekondari ya Maria Consolata iliyopo Kidabaga wilayani Kilolo mkoani Iringa.
Shule hiyo inamilikiwa na Kituo cha Nyota ya Asubuhi ya Wamisionari Wakatoliki wa Italia, kinachosaidia kuwatunza watoto wanaotoka katika mazingira magumu.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii shuleni hapo hivi karibuni, walisema wanafurahi kuwa miongoni mwa watahiniwa watakaofanya mtihani huo wa kidato cha nne mwaka huu.
“Tunafurahi, tunajiandaa tunasoma kwa bidii, mtihani uko karibu tunataka tufaulu vizuri masomo yetu, ili ile ndoto yetu ya kuwa Makatibu Muhtasi itimie,” walisema Maria na Consolata, ambao wanatumia baiskeli maalumu kuwapeleka darasani, ambako pia wana kiti maalumu.
Pacha hao wameshangaza watu wengi kwa jinsi walivyo, ambapo kila mmoja ana madaftari yake. Wakati wa kufanya mazoezi au kuandika kazi wanazopewa, mmoja huanza kuandika, akimaliza na mwingine huandika.
“Wala hatupati shida tumezoea, kila mmoja anafanya kazi yake, mimi naandika kwa mkono wa kushoto na Maria anaandika kwa mkono wa kulia,” anasema Consolata, ambaye anaonekana kuwa mchangamfu zaidi.
Shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Ilianzishwa mwaka 2006 na hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 183. Wote wanaishi kituoni hapo na wote wanatoka kwenye mazingira magumu.
Changamoto kubwa iliyokuwa shuleni hapo ni ukosefu wa nishati ya umeme, ambapo uongozi wa shule na kituo hicho unalazimika kutumia jenereta na umemejua, jambo ambalo mapema wiki hii Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA), imewaondolea adha kwa kuwapelekea umeme.
Pacha hao walizaliwa mwaka 1996 wakiwa wameungana katika Hospitali ya Ikonda wilayani Makete mkoani Iringa. Walifaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2010, ambapo kila mmoja alipata alama 151, ingawa walitofautiana ufaulu kwenye masomo yao.
Katika somo la Maarifa ya Jamii, Consolata alipata alama 29 na Maria alama 25, kwenye somo la Kiingereza, Maria alipata alama 36 na kumzidi Consolata aliyepata alama 34, wakati kwenye somo la Sayansi, Maria alimzidi Consolata kwa kupata alama 31 dhidi ya 29.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliwapanga pacha hao kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam. Hata hivyo hawakujiunga na sekondari hiyo, kutokana na hali yao na pia umbali kutoka Iringa hadi Dar es Salaam.
Ndipo Wamisionari hao wakawachukua mwaka 2011 na kuanza kidato cha kwanza.
Kuzaliwa kwao
Walizaliwa kwenye Hospitali ya Misheni ya Ikonda mwaka 1996. Lakini, taarifa zao hazikufahamika hadi pale walipoandikishwa kuanza elimu ya msingi Ikonda na kutafutiwa mlezi wa kuwaangalia, baada ya wazazi wao kufariki dunia wakiwa bado wadogo.
Sisi wa HabariLeo tunawatakia kila la heri katika maandalizi yao ya mtihani wa kumaliza Kidato cha Nne.
Chanzo:Habari Leo

WATENDAJI NJOMBE KUTUMIA VEMA BARAZA LA BIASHARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WATENDAJI wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa Baraza la Biashara la Mkoa kuunganisha sekta ya umma na binafsi kujadili kutatua changamoto zilizopo katika biashara na kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya biashara zilivyopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Mkurugenzi wa Biashara wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Arthur Mtafya, alisema wajumbe wa baraza hilo hawana budi kuzingatia fursa za uchumi zilizo katika mkoa huo na kujadiliana juu ya vikwazo vya biashara, ili kupanua wigo wa uwekezaji mkoani humo.
“Nia ya kuanzisha baraza katika ngazi ya mkoa na wilaya ni kurahisisha utendaji kutoka ngazi ya taifa mpaka wilayani, kwani kuna mambo yanayoweza kushughulikiwa katika ngazi ya mkoa,” alisema.
Mtafya alisema sera za nchi zinaruhusu baadhi ya changamoto zinazohusu mkoa fulani zitatuliwe katika ngazi ya mkoa na kwamba hiyo inasaidia utendaji na uwajibikaji na kuwa yanaposhindikana ndipo huwasilishwa katika ngazi ya taifa, ili kufanyiwa kazi. Alisema ushiriki kamilifu wa sekta hizo mbili katika ngazi ya mkoa na wilaya utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuinua hali ya biashara na uwekezaji katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kapteni Mstaafu Asei Msangi, alisema baraza hilo jipya litakuwa chachu ya maendeleo kwa kuunganisha sekta ya umma na binafsi katika kujadili vikwazo vya biashara, ili kukuza uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Chanzo:Tanzania Daima

WANAWAKE VAENI NGUO SASA, KAMA KUVUA MUMESHAVUA IMETOSHA‏


MOJA ya sifa ya mwandishi ni kusoma, na katika kusoma huko na kupekua pekua hapa na pale unaweza kujifunza na kupata la kuandika kupitia maandiko ya watu wengine na kutoa elimu kwa umma. Leo nimepita pita katika kurasa za marafiki zangu huko katika uso wa kitabu ‘Facebook nikakutana na nasaha ya ndugu yangu Victory Richard, juu ya kuwasihi wanawake kwamba  sasa wavae nguo.

Ndugu yangu yule amechoshwa na tabia za dada zetu, wake zetu na hata mama zetu wakati mwingine wanavyotembea uchi, ndio! utavaaje nguo fupiii au skintight halafu useme umevaa nguo?. Binafsi naomba radhi kama nitakuwa nimemkwaza mtu hasa hao mama zetu, Ah! Lakini potelea mbali Anko Kidevu sijali kitu si wamejitakia.

Hivi akina mama na dada zetu kweli jamani katika yooote ambayo mnalilia usawa na sisi tunakubali kuwa sawa, hili la kutembea uchi au kuvaa mavazi nusu uchi mbona mnapitiliza?

Ndio mmepitiliza Anko nimebaini kuwa mmetupita maana sisi tukivaa sana ni kaptura au bichkoma na kawosh au singlendi lakini sasa naona mmepita katika sketi na sasa mna vimini na kuacha vifua wazi.

Ni nani awezaye kuona aibu yenu zaidi yangu mimi Anko Kidevu na kaka yenu Victor Richard, tafadhalini tunawasihi, hebu vaeni nguo sasa na jamii itawaheshimu maana hakuna heshima kwa mwanamke hata kidogo. Na kama mnahisi mnaheshimika kwa hilo ni bure kabisa. SOMA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TANGAZO MUHIMU KWA WAHITIMU WOTE WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) , WANAALIKWA KWENYE MKUTANO 4 OKTOBA 2014


C H U O   C H A   E L I M U   Y A   B I A S H A R A (CBE)

CHINI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA”
MKUTANO WA CBE ALUMNI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI



         KAMPASI YA MBEYA
Mkuu wa Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Mbeya, Dionize A. Lwanga , Akizungumzia Mikakati na maandalizi ya awali ya Kutimiza Miaka 50 ya Chuo hicho, na Mkutano Mkubwa utakaofanyika Mwezi Octoba ambao utawakutanisha wanafunzi wote waliowahi kusoma chuo hicho ili kujadiliana mambo kadha wa kadha wakati wanajiandaa na miaka hiyo 50 na kutengeneza Alumni Association.
 Afisa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mbeya akizungumza Jambo wakati wa Majadiliano juu ya maandalizi ya Kikao cha mwezi Octoba.
Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mbeya Akizungumza jambo wakati wa mazungumzo mafupi juu ya Maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika Octoba
Majadiliano yakiwa yanaendelea




MKUU WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA ANAWATANGAZIA WAHITIMU WOTE WA MIAKA YA NYUMA NA WA SASA WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA WANAOISHI KATIKA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA WANA JUMUIA YA CBE (CBE ALUMNI) UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 4, 10, 2014 KATIKA VIWANJA VYA MBEYA HOTEL, JIJINI MBEYA, KUANZIA SAA 7.00 MCHANA. BAADA YA MKUTANO KUTAKUWA NA CHAKULA CHA PAMOJA.

MIONGONI MWA MAMBO YATAKAYOFANYIKA SIKU HIYO NI PAMOJA NA:

1)      KUUNDA ALUMNI ASSOCIATION KWA NYANDA ZA JUU KUSINI

2)      KUCHAGUA VIONGOZI WA ALUMNI ASSOCIATION WA KANDA

3)      KUPATA TAARIFA YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CBE

4)      MADA KUHUSU MCHANGO WA CBE KATIKA KUENDELEZA BIASHARA NCHINI

5)      MADA KUHUSU CBE ILIPOTOKA, ILIPO KWA SASA NA CBE IJAYO

6)      KUBADILISHANA UZOEFU NA MAWAZO (NETWORKING)

MADA HIZI ZITAWASILISHWA NA WAKUFUNZI, WAHITIMU, WANAFUNZI NA WADAU WENGINE WA CBE.

TAFADHALI, UPATAPO TAARIFA HII MJULISHE NA MWENZIO.

 PAMOJA TUNAWEZA

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA MKUU WA KAMPASI YA MBEYA

BARUA PEPE: dir.mbeya@cbe.ac.tz

Simu                 :025- 2500571
                          :0654- 878704, 0717 -288874, 0655- 080858






C H U O   C H A    E L I M U    Y A    B I A S H A R A (CBE)


CHINI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA”

KAMPASI YA MBEYA



NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO NGAZI YA ASTASHAHADA (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 KATIKA FANI ZIFUATAZO:


  • Uhasibu ( Accountancy)
  • Masoko (Marketing Management)
  • Ununuzi na Ugavi (Procurement & Supplies Management)
  • Usimamizi wa Biashara (Business Administration)

1.  Fomu za kujiunga zinapatikana Chuoni Jengo la chuo kikuu Huria ( Kituo cha Mbeya) Forest ya zamani, CBE DAR ES SALAAM, CBE DODOMA, CBE MWANZA au   Bofya hapa Chini Ku Download


2. Wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu usiopungua D nne watajiunga moja kwa moja.

3. Kujiunga na stashahada (diploma) wahitimu wa kidato cha sitwenye    ufaulu usiopungua Principal pass moja, subsidiary pass mbilAu wenye    astashahada husika yaani (certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa na NACTE



Masomo kwa ngazi zote yanatolewa kuanzia asubuhi hadi jioni (FULL TIME)  na jioni (EVENING PROGRAM) jumatatu hadi ijumaa.


Ewe mwananchi jiunge na chuo chenye uzoefu wa zaidi ya miaka 49 katika elimu ya Biashara, Ujasiriamali, Ushauri na Utafiti.


Tunaendelea kupokea maombi ya kujiunga katika ngazi zote



Kwa maelezo zaidi piga  simu namba, 0654-878704 / 0767-288874
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa