MBUNGE MGAYA AWASAIDIA WANAWAKE VYEREHANI 370 NJOMBE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe Neema Mgaya (katikati mstari wa mbele) akiwa na baadhi ya wanawake aliowakabidhi vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 90 Halmashauri ya Makambako Mkoani Njombe ili wajikwamue kiuchumi.
Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Njombe, Neema Mgaya (mbele) akiwa na baadhi ya wanawake aliowakabidhi vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 90 Halmashauri ya Makambako Mkoani Njombe ili wajikwamue kiuchumi.
Baadhi ya vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 90 vilivyolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Neema Mgaya vikiwa tayari kukabidhiwa kwa baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Njombe ili wajikwamue kiuchumi. 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Neema Mgaya ametoa msaada wa vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Milioni 90 kwa wanawake mkoani humo ili wajikwamue kiuchumi huku akiunga mkono juhudi za Serikali inayohimiza uchumi wa viwanda. Akizungumza Mjini Makambako wakati wa hafla ya kukabidhi vyerehani hivyo kwa baadhi ya wanawake, Mgaya amesema amefikia uamuzi huo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa taifa la uchumi wa kati kupitia viwanda. Akibainisha zaidi ameeleza juhudi za kumkomboa mwanamke wa mkoa wa Njombe ni jambo linalopiganiwa kwa miaka mingi hivyo vyerehani hivyo vitawafungulia njia kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Nimekuwa sina papara katika utendaji wangu, mwaka jana nilitoa msaada wa vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari Halmashauri ya Makambako, ambapo kwa mwaka huu nimeamua kuunga mkono juhudi za serikali upande wa viwanda kwa kuwasadia wanawake hawa vyerehani hivi 370,” alisema Mgaya.

Akifafanua amesema anatambua thamani kubwa walionayo wanawake hivyo kwa kuwawezesha vyerehani hivyo kutainua familia na jamii zinazowazunguka kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia huduma za kijamii na mahitaji mengine.

“Mtu ninayemthamini huwa nampa kitu ambacho kitadumu na kumsaidia kwa muda mrefu, mimi nimeamua kutowapa samaki kwani mtamla ataisha, nimewapa nyavu ambayo mtaitumia kuvua samaki, nendeni mkavitunze vyerehani hivi kujiletea maendeleo endelevu,” alisema Mgaya.

Akizungumza baada ya kupokea cherehani yake Diwani wa Viti Maalum Lupembe Neema Limbanga amesema alilolifanya Mbunge huyo wa Viti Maalum halijawahi kutokea katika maisha yake na kwamba vyerehani hivyo vimewafungulia njia kimaisha.

Naye Diwani wa Viti Maalum CCM Njombe, Stella Francis amesema Mgaya amewapa zawadi ambayo licha ya kuwainua kiuchumi itakuwa mkombozi hasa katika ndoa zao, kwani sasa wataweza kuhudumia familia kwa kushirikiana na wanaume zao.

Kutolewa kwa vyerehani hivyo 370 ambavyo ni sawa na viwanda vidogo 92 kwa dhana ya vyerehani vinne sawa na kiwanda kimoja kidogo kunaufanya mkoa wa Njombe kuitikia vilivyo wito wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhamasisha uchumi wa viwanda. Lengo la Mkoa kupitia wanawake ni kuwa na viwanda vidogo 35 hivyo kwa vyerehani  370 ambavyo Neema amevitoa ni kwamba lengo la kimkoa kupitia wanawake limeshafikiwa.

WAKULIMA 206 WAPATA MAFUNZO YA KILIMO CHA CHAI KUTOKA NOSC

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah(wapili kushoto) akikabidhi cheti bwana Thiemo Msewa(kulia) katika hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NOSC, Bwana Filbert Kavia. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Ruth Msafiri 
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah akizungumza jambo wakati wa hafla hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. 
Operation Director wa Wood foundation Tanzania Bwana Mathew Ng’enda(watatu kushoto) akishangilia mara baada ya wakulima kuwasilisha mada mbalimbali juu ya elimu ya kilimo cha chai (farmer field school) waliyoipata kutoka Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah. na watatu kulia ni Mkurugenzi mkuu wa NOSC Bwana Filbert Kavia. 

KUTOKANA na ushirikishwaji wa wakulima wadogo katika zao la chai kupitia Kampuni ya Kuhudumia Wakulima Wadogo Njombe (NOSC), viongozi wa Mkoa wa Njombe wanajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kilimo cha chai kilichosaidia kuinua kipato cha wakulima wadogo na kuongeza fedha za kigeni.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Njombe, Bwana Lameck Noah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka mkoani hapa jana katika mahafali ya mwaka mmoja kuhusiana na mafunzo ya kilimo cha chai kilichohusisha wakulima zaidi ya 206.

“Katika mkoa wetu tulijiwekea utaratibu kuwa kila mkulima alime mazao ya aina mbili ya chakula na biashara, kwa upande wa chai tatizo lilikuwa ni aina ya miche, ilikua inachukua muda mrefu kukua lakini tunaishukuru NOSC imetuletea mice inayokua kwa miezi 12 mkulima anaanza kupata majani mabichi ya chai,” alisema Bw. Noah.

Alibainisha kuwa elimu hiyo ina maana kubwa kwa mkoa wake kwa sababu itawasaidia kulima kisasa na kuwaongezea kipato wananchi wa mkoa huo, lakini pia viwanda vitapata malighafi hiyo muhimu kwa ajili ya soko la ndani na nje.

“Tunafahamu chai inapendwa na mataifa ya magharibi, zao hili lina fedha nyingi za kigeni. Soko la chai lipo na tunawahakikishia wakulima serikali inahangaika kupata mnada wa chai katika ukanda huu badala ya kufanyika Mombasa nchini Kenya.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa