Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akikagua gwaride la wanamgambo
Mkuu wa wilaya akitoa hotuba yake
Na Edwin Moshi, Makete
Vijana
wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutambua kuwa suala la wao
kushiriki mafunzo ya mgambo lipo kisheria hivyo kuitaka jamii kwa ujumla
kushirikiana ili malengo ya mafunzo hayo yatimie
Rai
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Bi Josephine Matiro wakati
akifunga mafunzo ya mgambo yaliyofanyika kwa kipindi cha miezi minne
katika kata ya Lupila wilayani Makete
Bi
Matiro amefikia hatua hiyo kutokana na risala ya mgambo hao kuonesha
kuwa wapo walioandikishwa kushiriki mafunzo hayo lakini waliyakatisha
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uvivu na kutoona umuhimu wa
mafunzo hayo ambapo awali waliandikishwa zaidi ya 150 lakini wamehitimu
61 tu
Katika
hatua nyingine Mkuu wa wilaya amewashauri mgambo hao kuanzisha kikundi
chao cha ujasiriamali na endapo watafanya hivyo serikali itawapatia
mikopo itakayowasaidia kujiendessha kupitia vikundi
Wakizungumza
na mtandao huu baadhi ya mgambo waliohitimu kwenye mafunzo wameshukuru
na kusema kuwa wameelewa mambo mengi ikiwemo kutumia silaha, kukabiliana
na adui hata kama ana silaha, mbinu za kivita pamoja na huduma ya
kwanza
0 comments:
Post a Comment