Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Katikati) alipotembelea Hospital ya Mji wa Makambako.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akisalimia na Muuguzi
wa Hospital ya Mji wa Makambako alipotembelea Hospital hiyo kukagua
utoaji wa uduma za Afya
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Njombe Mhe.Lucy Msafiri wakati wa ziara yake katika Hospital
ya Mji wa Makambako.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo katika Picha ya pamoja
na viongozi wa Wilaya pamoja na watumishi wa Hospital ya Mji wa
Makambako.
Huu ndio Muonekano wa Hospital ya Makambako unavyoonekana kwa hivi sasa
Nteghenjwa Hosseah,Makambako.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako Mhe. Deo Sanga kwa jitihada
mbalimbali anazozifanya katika kuboresha Sekta ya Afya katika Jimbo
hilo.
Jafo
ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospital ya Mji wa Makambako na
kuona vyumba viwili vya Madaktari ambavyo vimejengwa na Mbunge Mhe.
Sanga.
“Kwa
dhati kabisa nimpongeze Mhe. Sanga kwa kujitoa kuboresha huduma za
Jamiia hii inaonyesha nia yake njema katika kuwaletea wananchi maendeleo
kwa sabababu wananchi wakiwa na Afya Njema wataweza kuendelea na
shughuli zao kikamilifu za kujitaftia kipato kisha kupata maendeleo”
Alisema Jafo
Kwa
kutambua Idadi kubwa ya watu wanaopata huduma katika Hospital hiyo
ambayo ina miundombinu Duni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Jengo la
kisasa la Kuhifadhia Maiti pamoja na Ukosefu wa wodi mbalimbali.Waziri
Jafo amesema Serikali itaangalia jinsi ya kuboresha miundombuni hiyo
ili wakazi wa Makambako waweze kupata huduma bora za Afya kama
Watanzania wanazopata wengine.
“Tutaweka
Jitihada katika kutafuta Fedha kutoka kwenye vyanzo vyetu Ili kuongeza
miundombinu ya Afya na hospital hii iweze kuwa na hadhi ya kuwa na
Hospital ya Mji” Alisema Jafo.Hata
hivyo Jafo amechukua kilio cha Hospital hiyo kuendelea kupata mgao wa
Kituo cha Afya wakati imeshapandishwa hadhi kuwa Hospital ya Mji ana
ameahidi kulishughulikia.
“Makambako
ni eneo muhimu sana katika Kanda hii yenye wakazi wengi, shughuli
nyingi za kiuchumi na muingiliano wa watu wengi kutoka ndani na nje ya
Nchi hivyo inahitaji huduma bora zaidi za Afya kwa kwa kuzingatia
umuhimu wa eneo na wananchi wake” alisema Jafo.
Waziri
Jafo anaendelea na ziara yake katika Mikoa Mbalimbali lengo ni ukaguzi
wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo iki chini ya Ofisi ya Rais
Tamisemi.
0 comments:
Post a Comment