Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi
8, mwaka huu kwa pamoja kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo
baada ya kujadiliana kwa kina katika mkutano huo
Miongoni
mwa viongozi waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho
wilaya ya Makete Bw. Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi
mzima uliokuwa ukiongoza chama hicho wilaya
Mkutano
huo ambao pia uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe
akiwemo mwenyekiti Bw. Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama
hicho wilayani Makete ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine licha ya
jitihada zinazofanywa na ndiyo maana wakaona wabadilishe uongozi
Katika
mkutano huo waliazimia kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi
miwili ya matazamio kuhakikisha wanakiimarisha chama katika kata zote za
wilaya ya Makete ikiwemo kuunda uongozi wa kila kata ambao unaweza
kufanya kazi kama inavyotakiwa
Viongozi
wa wa muda waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa
muda ni Bw. Ibrahim Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni
katibu na Bw. Stephano Kasanga ambaye ni katibu mwenezi
Mkutano
huo umewapa miezi miwili ya kukiimarisha chama kabla ya kuitishwa
mkutano mwingine ambao utakuwa wa uchaguzi wa wanachama kuwachagua
viongozi wa wilaya wa kukiongoza chama hicho.
0 comments:
Post a Comment