Home » » Apoteza maisha baada ya kudondokewa na kifusi Makete‏

Apoteza maisha baada ya kudondokewa na kifusi Makete‏



Na Edwin Moshi, Makete
Mtu mmoja ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ivalalila kata ya Iwawa wilayani Makete amefariki dunia baada ya kudondokewa na kifusi cha mchanga wakati akichimba mchanga
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa upelezi wilayani Makete Bw.Gozbert Komba amemtaja mkazi huyo kuwa ni Daudi Ilomo (42)amesema kuwa amefariki dunia wakati akichimba mchanga kijijini hapo

Aidha ameongeza kuwa mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umevunjika mguu mara mbili,pia alitokwa na damu puani na masikioni baada ya kifusi hicho kumbana katika mwili wake hasa kifuani

Hata hivyo marehemu wakati wa uhai wake kwa mara ya mwisho alikuwa na Bw.Polito ilomo

Pia OCCID Komba ametoa wito kwa wananchi  wote kuwa makini pindi wanapokuwa katika maeneo wanaojua kuwa ni hatarishi kwao kuwa katika makundi ili kusaidiana na kujiepusha katika majanga kama ya aina hiyo

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa