
NJOMBE – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, tarehe 24 Machi,2025 alifanya ziara mkoani Njombe ambapo, aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alitembelea Kiwanda cha Muricado Fruit Supplies kujionea uwekezaji mkubwa unaofanyika katika kuongeza thamani ya zao la parachichi.
Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mhe. Prof. Mkumbo alimpongeza muwekezaji kwa juhudi zake katika kukuza sekta ya viwanda na kilimo. "Huu ni uwekezaji wenye tija kwa wakulima wa parachichi na uchumi wa taifa kwa ujumla. Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani ili kuhakikisha viwanda vya aina hii vinakua na kuchangia maendeleo ya nchi," alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Josiah Mrimi, alisema kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza thamani ya zao la parachichi kwa kusindika na kuuza bidhaa zake katika soko la ndani na kimataifa.
Kiwanda cha Muricado Fruit Supplies kinatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wakulima wa parachichi kwa kuwapatia soko la uhakika, sambamba na kusaidia jitihada za serikali za kuendeleza sekta ya viwanda na kilimo nchini.
0 comments:
Post a Comment