MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 26, 2017

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


JUMIA TRAVEL YAZINDUA YAUNGANISHA MFUMO WA HUDUMA KWA WATEJA NA FACEBOOK MESSENGER

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Kampuni inayoongoza kwa uwakala wa huduma za kusafiri mtandaoni Afrika, Jumia Travel imezindua mfumo mpya wa huduma kwa wateja kupitia ‘Facebook Messenger’ kwa kushirikiana na Salesforce (Kampuni kinara kwenye Usimamizi wa Huduma kwa Wateja)

ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUENDESHA GARI UMBALI MREFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Na Jumia Travel Tanzania

Linaweza kuwa si jambo la kushangaza kuwaona watu wakisafiri kwenye usafiri wao binafsi kuelekea mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Na hii ni kutokana na maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa watanzania wengi ambapo hapo awali walikuwa wanategemea usafiri wa umma.

Sababu za kusafiri zinaweza kuwa nyingi kama vile kifamilia, kutembelea ndugu na jamaa au vivutio mbalimbali vya kitalii. Lakini je ni wangapi wanayafahamu mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuingia barabarani na usafiri binafsi kwenda umbali mrefu? Jumia Travel imekukusanyia masuala muhimu ambayo usipokuwa makini kuyafuata basi safari yako itakuwa ni shubiri badala ya asali huko njiani.

Jipange kwa safari nzima. Sidhani kama kuna jambo ambalo unaweza kufanikiwa bila ya kujipanga. Vivyo hivyo unapotaka kusafiri ni lazima uweke mipango madhubuti tangu mwanzo mpaka mwisho wa safari yako. Kwa mfano, safari itachukua muda gani, hoteli gani mtafikia, gari utakalolitumia litawatosha watu wangapi, gari litahitaji mafuta kiasi gani mpaka kumaliza safari, nini cha kufanya inapotokea dharura na kadhalika.   

Chunguza usafiri wako. Barabarani kuna mengi yanatokea ingawa kuna mengi unaweza kuyadhibiti endapo utachukua tahadhari kabla. Kwa mfano suala la gari kuharibika njiani linaweza kuepukika endapo utachukua muda wako kulipeleka kwa fundi kufanyiwa uchunguzi na matengezo pale yatakapohitajika. Huwezi jua inawezekana injini isingeweza kukupeleka hata nusu ya safari yako au jaribu kuvuta picha gari linapokuharibikia katikati ya msitu wenye wanyama wakali bila ya msaada.
Hakikisha usafiri wako umekidhi vigezo vyote vya kuwa barabarani. Kusafiri umbali mrefu hususani kutoka katikati ya jiji haimaanishi kwamba huko barabarani sheria hazifuatwi. Kwa hiyo hakikisha kuwa usafiri wako umekidhi vigezo vyote vya kuwepo barabarani kama vile leseni ya udereva, bima ya gari, leseni ya barabarani na sheria nyinginezo. Usipofanya hivi unaweza kujikuta unalipishwa faini, kukamatwa na hivyo kupotezewa muda ambao ilibidi uutumie kukufikisha huko uendako. Kwa mfano sio umefika Bagamoyo tu askari wa barabarani wanakukamata na kukuambia vibali vya gari lako kuwa barabarani vimekwisha muda wake.

Tarajia changamoto mbalimbali barabarani. Ni mara chache kusafiri barabarani bila ya kukutana na changamoto zozote kama vile foleni, njia kuwa mbovu, ukaguzi wa mara kwa mara, ajali na kadhalika. Hivyo lazima ujiandae kiakili wewe kama dereva pamoja na watu unaosafiri nao.
Usibebe mizigo mingi sana. Sawa mizigo ni muhimu kwa kuwa unasafiri umbali mrefu lakini kwa kufanya hivyo unaweza kujinyima fursa ya kubeba vitu vingine utakavyovutiwa navyo njiani. Hivyo basi hakikisha unabeba mizigo ambayo ni muhimu kwako kwani unaweza kupita sehemu na ukakuta vitu vya gharama nafuu ambavyo unaweza kununua.

Beba ramani ya kukusaidia huko uendako. Wengi wetu huwa tunapenda kwenda sehemu ambazo tunazifahamu hivyo inakuwa sio lazima sana kuwa na ramani ya kukupa mwongozo. Lakini siku hizi maendeleo ya teknolojia yamekuwa ni makubwa kwani sehemu nyingi zimewekwa kwenye ramani kupitia vifaa mbalimbali kama vile kompyuta, tabiti na simu. Mbali na teknolojia kurahisisha hilo lakini unashauriwa kubeba ramani ya karatasi, kwa mfano kama unanda Zanzibar unaweza kuwa na ramani inayokuonyesha sehemu zote za kule.
Kuwa na nyimbo au vitu vya kukuburudisha njiani. Kazi na dawa huwa wanasema Waswahili. Haimaanishi kwa sababu unasafiri umbali mrefu basi ndiyo uwe makini na usukani pasipo kujiburudisha. Beba vitu kama vile CD za muziki zenye nyimbo uzipendazo pamoja na michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto wako kama unasafiri nao. Lakini pia hata vinywaji na vitafunwa vinaweza kuifanya safari iwe ni fupi na ya kuifurahia.

Beba pesa ya akiba. Unaposafiri njiani unaweza kukutana na changamoto ambazo zitahitaji pesa ya papo kwa papo ili kuweza kuzitatua. Hivyo hakikisha unakuwa na kiasi cha pesa taslimu kwani mara nyingi sehemu za kuzipata huwa ni nadra. Pia itakusaidia hata kununua vitu vya njiani, kwa mfano Morogoro kuna bidhaa nyingi sana kutoka kwa wakulima.  

Jaribu kuipumzisha simu yako kwa muda. Itakuwa haileti maana kuwa upo kwenye usafiri pamoja na wenzako au familia yako lakini unawasiliana na watu uliowaacha ulipotoka. Lengo la safari za namna hii mara nyingi ni kujaribu kubadili na kufurahia mazingira mapya. Basi jaribu kuendana na mazingira hayo kwa kuzungumza na wenzako ndani ya gari ninaamini kutaifanya safari kuwa ni ya kusisimua zaidi.  

Piga picha kwa ajili ya kumbukumbu. Ni muhimu kuwa na kumbukumbu ya baadhi ya matukio unayoyaona. Siku hizi kamera inapatikana kwenye simu za mkononi hivyo kurahisisha kuhifadhi kumbukumbu ya matukio mbalimbali. Basi hakikisha unapiga picha za sehemu na matukio utakayovutiwa nayo au hata wewe mwenyewe ukiwemo ili iwe kama ni ukumbusho kwako. Kwa mfano haiwezekani ukapita mbuga ya Mikumi bila ya kupiga picha ya Tembo au pundamilia wanaokatiza barabarani.
Kusafiri kwa kutumia gari binafsi hususani umbali mrefu ni starehe kubwa ambayo wengi bado hawajaigundua. Wapo wengine wanapanda ndege ili kuwahi kufanya vitu vingi huko waendapo pamoja na kuepuka uchovu. Lakini Jumia Travel inasisitiza kwamba kusafiri kwa njia ya barabara kunakupa fursa kubwa ya kujionea ni jinsi gani nchi yako imebarikiwa na fursa ya kujifunza mengi zaidi.

Bweni la Itamba Sekondari Makete Likiteketea Kwa Moto

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bweni la Wasichana la shule ya sekondari Itamba iliyopo katika tarafa ya Matamba wilayani Makete mkoani Njombe leo limeteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika.

Waziri mkuu Mhe Majaliwa asema wanaojichomeka eneo la mgodo ili wapate Fidia kutolipwa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Waziri mkuu wa tanzania Mhe. Kassm Majaliwa (Katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi mkoani Njombe katika eneo la Liganga nyuma yake ni Mawe yanayo daiwa kuwa na Chuma Cha liganga
 Waziri Mkuu Wa Tanzania Kassm Majaliwa Akizungumza na wakazi wa Ludewa Mkoani Njombe ambako anatoa onyo wa wanao jifanya wananchi na kuvamia migodi la Liganga
 Ngomba ya Kinyakyusa ikimpokea waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanya vya shule ya mpira Ludewa Mjini ambako amezingunza na wananchi
SERIKALI imesema kuwa itahakikisha kuwa wananchi wanao zunguka mradi wa Machimbo ya Liganga machimbo ya chuma ambao unatarajia kuanza hivi karibuni ambapo kunatarajiwa wananchi hao kulipwa na kuanza Machimbo katika eneo hilo ambapo onyo kwa wale ambao wameanza kuanza kujichomeka na kupata fidia.

Waziri Mkuu ametembelea eneo la machimbo ya Liganga wilayani Ludewa ambapo mbunge wa jimbo la Ludewa anaomba kwa waziri wananchi wake kulipwa fidia na kuwekwa kwa lami barabara ya kutoka Mkiu kuingia mpaka katika mladi wa Liganga.

Waziri akielekea wilayani ludewa anakutana na wananchi wanao msimamisha katika kijiji cha Lusitu ambapo wananchi wanamfikishia kilio chao kwa kutumia nyimbo.

Kabla ya kuingia ludewa mjini waziri anaingia Liganga ambako chuma litachimbwa kwenye mlima wa mawe ya chuma lenye ukubwa wa kilomita kumi ambapo akiwa hapa anazungumza na viongozi wa mkoa wa Njombe.

Baada ya kumaliza kutembelea mradi huu waziri mkuu anakutanan ana wananchi ambapo suala ya fidia mbunge analisema mele ya mkutano wa hadhana huku barabara nayo ikiombwa kuwa ya lami kutoka Mkiu hadi Liganga.

Na haya ndio majibu ya waziri mkuu huhusu umeme, fidia na huduma zinginde za za kijamii.
Kuhusu kukamilika  kwa kulipa fidia na kuanza kwa mradio huo waziri anaongeza.

Baada ya kutoka eneo la mgodiwaziri mkuu anaelekea mjini  Ludewa kwaajili ya Mkutano wa Hadhara   na kuzungumza na wakazi wa  mjini Ludewa ambapo suala la maji na barabara linaibuka tena.


Wananchi waomba eneo lao Kupimwa ana kugawiwa viwanja Njombe

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadhara
Baadhi ya wakazi mjini njombe wakisikiliza mkutano wa mkuu wa wilaya ambapo walipata nafasi ya kutoa maoni yao

WANANCHI halmashauri ya Mji wa Njombe wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo Ruth Msafiri kuiamuru halmashauri hiyo kuwagawia wananchi viwanja vilivyopimwa ambapo katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2012 hakujapimwa tena viwanja.

Wananchi wanatoa kero zao wakati wa mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya na wananchi ambapo ni kitu cha kwanza kufanyika wilayani hapo.

Nestori Kigae akitoa kero yake kwa mkuu wa Wilaya ya Njombe alisema kuwa halmashauri hiyo haigawi viwanja kwa vijana na kuwa sasa ni muda mrefu viwanja havijagawiwa na kusasabisha wananchi kukosa maeneo ya kujenga.

Alisema kuwa vijana wapo tayari kujenga makazi yao lakini halmashauri hiyo haipimi viwanja na kuvigawa kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa afisa wa Ardhi kujibu masuala yanayo husu ardhi yaliyo ulizwa na wananchi.

Afisa ardhi Taday Kabonge alisema kuwa halmashauri yake ilipima viwanja mwaka 2012 lakini mpaka sasa haijawahi kupima na kuwa kuna viwanja ambavyo mpaka leo bado vipo havijachukuliwa.

Alisema kuwa viwanja vinavyo gawiwa na halmashauri vinauzwa na havigawiwi bure kwa wananchi na kuwa vinatolewa kwa wananchi wote wa halmashauri hiyo.
Katika hotuba ya mkuu wa wilaya ya Njombe ya lisaa limoja kwa wananchi anasema kuwa serikali itahakikisha kero kwa wananchi zinaondoka na kuishi kwa amani bila bughuza.

Hata hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inapima viwanja mara kwa mara ili wananchi wake kuendelea kupata maeneo ya kujenga na kuachana na kujenga maeneo ambayo hayahusiki.

Alisema kuwa haiwezekani halmashauri ikapima viwanja kila mara na sio baada ya miaka minne, na kuwa wananchi wanajenga kila wakati.

Hata hivyo diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo alilalamika viwanja vinavyo pimwa na halamshauri kuuzwa bei ghari na kusababisha wananchi kushindwa kuvimiliki.

Na Furaha Eliabu wa Habari Online na Elimtaa

WAFANYABIASHARA WA VIUMBE PORI HAI WAOMBA HURUMA YA RAIS MAGUFULI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Ally Daud-MAELEZO
WAFANYABIASHARA wa viumbe pori hai wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungulia biashara ya viumbe hao kutokana na kusitishwa Machi mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Magembe.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Viumbe pori hai Bw. Salim Mussa amesema kuwa wanamuomba Mh. Rais Magufuli aingilie kati swala hilo na kupata ufumbuzi wa kudumu wa kuendelea na biashara hiyo ya viumbe kwa maendeleo yao na uchumi wa taifa.
“Tunakuomba Mh. Rais Magufuli uingilie kati swala hili na kutupatia ufumbuzi wa kudumu ili kuendlea na biashara ya viumbe pori hai bila ya usumbufu wa mara kwa mara kwani biashara hii ipo kwa mujibu wa sheria , taratibu na kanuni za nchi” alisema Bw. Salim.
Aidha Bw. Salim amesema kuwa maamuzi hayo yanaweza kusababisha hasara kubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa viumbe hivyo na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani  muongozo haujatolewa tangu kusitishwa kwa biashara hiyo mwezi machi mwaka huu.
Kwa upande wake Msemaji wa wafanyabiashara wa viumbe pori hai Bw. Enock Balilemwa amesema kuwa kusitishwa kwa biashara hiyo imepunguza kiwango cha ajira kwa kiasi cha watanzania milioni moja ambao asilimia 95 wanaishi vijijini.
“kusitishwa kwa biashara hii ya viumbe pori hai imefanya watanzania takribani milioni moja hasa wakazi wa vijini asilimia 95 kukosa ajira jambo ambalo linapelekea wananchi hao kukosa uwezo wa kujikimu kwa maisha ya kila siku” alisema Bw. Balilemwa.
Biashara hiyo ya viumbe pori hai inayojumuisha Vyura, wadudu, ndege,mijusi na tumbili, zoo na mashamba ya wanyapori ilianza kabla ya uhuru sambamba na leseni zingine za uwindaji wa kitalii ambayo mpaka sasa inatambulika kwa sheria namba 5 ya mwaka 2009.

Serikali kukipandisha kituo cha afya cha Laela kuwa hospitali ya Wilaya

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kukarabati kituo cha afya cha Laela kilichopo mkoani Rukwa ili kikidhi vigezo vya kuwa Hospitali ya Wilaya ikiwa ni moja ya jitihada za kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya zilipo.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleimani Jafo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Malocha aliyehitaji kujua ni lini kituo hicho cha afya kitapewa hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya.

Mhe. Jafo amesema kuwa ni uamuzi wa muda mrefu wa Serikali kuiweka Hospitali hiyo kuwa ya Wilaya na ndiyo sababu ya kufanya jitihada za kukiongezea uwezo kituo hicho kwa kujenga wodi nyingi pamoja na kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya kwani kwa sasa kituo hicho kina upungufu wa watumishi .

Amefafanua kuwa hadi sasa kuna baadhi ya majengo ambayo tayari yameshakamilika ambayo ni jengo la upasuaji wa dharura, wodi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji pamoja na wodi ya mama wajawazito.

“Kwa sasa kituo cha afya cha Laela hakina miundombinu inayokidhi sifa za kuwa Hospitali ya Wilaya ila kutokana na kupanuka kwa Mji huo na kuongezeka kwa watu wanaohitaji huduma katika kituo hicho tumeamua kukiboresha ili kifikie hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya”, amesema Jafo.

Ameongeza kuwa kwa sasa huduma za rufaa kwa wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho zinatolewa kupitia magari ya kawaida ya Halmashauri kutokana na ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa lakini Wizara ina matarajio ya kutenga fedha ya kununulia gari hilo katika Bajeti ya mwaka 2017/2018.

Aidha, Mhe. Jafo amethibitisha kuwa kituo hicho kimetengewa jumla ya shilingi 9,358,100 katika Bajeti ya fedha ya mwaka huu ambayo itagharamia kununua dawa na vifaa tiba vitakavyorahisisha upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Wizara hiyo inaendelea kuipitia mikataba ya makampuni binafsi ili kuangalia namna ya kushirikiana nao katika kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba katika Hospitali na vituo vya afya nchini.


KAMPUNI YA TANWAT YATOZWA FAINI YA MILIONI HAMSINI KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Na Lulu Mussa
Njombe

Wadau wa Mazingira wametakiwa kufuata Sera, Kanuni na Tararibu katika kuendesha shughuli zao.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameyasema hayo leo Mkoani Njombe alipokuwa katika mwendelezo wa ziara ya kutembelea Mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kujionea hali ya mazingira na kutoa maelekezo stahiki.
Waziri Makamba ametoza faini Kampuni ya TANMAT kwa kuikuka Sheria ya Mazingira inayokataza upandaji wa miti ndani mita sitini kutoka katika chanzo cha maji. "Kampuni hii imevunja sheria hivyo hamna budi kuchukuliwa hatua stahiki ili iwe mfano na kwa wengine" alisisitiza Waziri Makamba.
Kampuni hiyo imeagizwa kulipa faini hiyo ndani siku saba na endapo watakiuka hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Waziri Makamba pia ameiagiza Kampuni hiyo kuondoa miti hiyo ambayo si rafiki kwa mazingira mapema iwezekanavyo na kuagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwapa 'Restoration Order"  kurudisha mazingira katika hali yake ya kawaida.
Katika hatua nyingine, Meneja wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na upandaji wa miti Bw. Joseph Shirima amekiri kupokea barua zizoelekeza kusitisha uharibifu huo wa Mazingira katika chanzo cha Mto Mbukwa ambacho kinasambaza maji kwa wakazi wengi wa Wilaya ya Wanging'ombe.
Aidha, Waziri Makamba ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Njombe kupitia Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanachi kuacha kulima bustani za mbogamboga pembezoni mwa mito.
Dkt. Nchimbi alimfahamisha kuwa kwa sasa kuna kikundi kijulikanacho kwa jina la "Jerusalemu" kinachotoa mafunzo kwa wananchi juu ya matumizi bora ya ardhi na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira ambapo lengo ni kuanzisha vituo kama hivyo vya mafunzo kwa Halmashauri zote za Mkoa huo.
Waziri Makamba alitembelea na kuona "vinyungu" ambavyo awali vilikua vikilimwa kando ya mito na kwasasa vimehamishiwa majumbani, katika kuunga mkono jitihada hizo njema Waziri Makamba amechangia mifuko Hamsini ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa litakalotumika kutoa mafunzo zaidi ya kilimo.
Waziri Makamba Waziri Makamba anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya mazingira nchini, hii leo amewasili katika Mkoa wa Mbeya.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa