Home » » WAKUU WA IDARA WATAKIWA KUSHIRIKISHA WANANCHI KATIKA MIRADI

WAKUU WA IDARA WATAKIWA KUSHIRIKISHA WANANCHI KATIKA MIRADI

Kukosekana kwa ushirikishwaji wa jamii katika kupanga, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao kunachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha uwajibikaji kwa jamii ambapo jamii inashindwa kushiriki kikamilifu katika kusimamia miradi husika.
 
 Hali hii inasababisha  jamii kushindwa kutambua na kushiriki katika miradi inayotekelezwa na hivyo kukosa uendelevu licha ya kuwa miradi hiyo ipo katika maeneo yao

hayo yamebainika mkoani  Njombe katika Wilaya ya Makete baada ya  timu ya  shirika wanachama MIICO, kutembelea miradi kadhaa ya maendeleo katika wilaya hiyo na kubaini kuwa kuna hali ya wananchi kutoshirikishwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri hiyo  Nganya  Ephraim amekiri kuwa udhaifu wa watendaji unachangia kuwepo kwa mapungufu  hayo na kudai kuwa tatizo ni watendaji hawakuwa na ushirikiano na wakuu wa idara katika miradi.
 
Waganga ‘KAMCHAPE’ wakamatwa kwa utapeli Tabora
SERIKALI  Wilayani Tabora imewapa onyo waganga wa kienyeji wanaotapeli wananchi kwa kujifanya wanawabaini wachawi,Maarufu kama kamchape,na kuwataka waachane na tabia hiyo ya kudanganya wananchi vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora,Suleiman Kumchaya,amesema hayo mara baada ya kukamatwa kwa waganga wawili ambao walikiri kufanya utapeli kupitia uganga na kuahidi kuachana na kazi ya kamchape.

Mtendaji wa kata ya Kabila katika manispaa ya Tabora,Bw.Godfrey Selula, amesema waganga hao wamekuwa wakifanya shughuli zao kinyume cha sheria wakiwa na vibali visivyojulikana wala kutambulika kuanzia ngazi ya wilaya hadi kwenye Vijiji.

Kwa upande wao waganga hao wa kienyeji maarufu kama kamchape,Mohamed Ally na Hamis Juma,wamekiri kujihusisha na utapeli kupitia uganga na kuahidi kuachana na shughuli hiyo ya utapeli.

Waganga hao  maarufu kama kamchape wamekuwa wakiitwa katika Vijiji mbalimbali kwenye wilaya za Mkoa wa tabora kwa lengo la kuwabaini wachawi ambapo wamekuwa wakitoza malipo makubwa kwa kazi hiyo huku wakiishia kuleta mifarakano miongoni mwa wananchi.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa