PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU JOHN SIMALENGA MJINI NJOMBE LEO




 Waziri Mkuu, Mizengo pinda akisalimiana na Maaskofu wa kanisa la Anglican nchini wakati alipowasili kwenye kanisa kuu la Anglican la Njombe kuhudhuria mazishi ya Askofu wa Dayosisi  ya South West Tanganyika, , John  Andrew Simalenga 



 Waziri Mkuu, Mizengo Pindaakitoa heshima za mwisho kwa Askofu John Andrew Simalenga katika mazishi ya Askofu huyo wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican lyaliyofanyika Njombe  Novemba 28, 2013.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican nchini, Dr. Jacob  Chimeledya


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika yaliyofanyika Njombe 


 Mwili wa Askofu wa Kanisa la Anlican Dayosisi  ya Southa  west, John Andrew Simalenga ukitelemshwa kaburini kwenye mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la  Dayosisi hiyo mjini Njombe 


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la Askofu wa Dayosisi ya  South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican, John Andrew Simalenga yaliyofanyika  mjini Njombe

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu wa Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga  katika mazishi yaliyofanyika leo Njombe 


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa  la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga yaliyofanyika leo Njombe Novemba 28, 2013. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WATOA ELIMU YA KUPAMBANA NA UKATILI NA UNYANYASAJI KWA WATOTO WILAYANI MAKETE‏





 Miongoni mwa vitendo vinavyoshamiri Makete vya watoto kujihusisha na biashara ya kuuza mkaa


 Hapa watoto hao wakiandaa mkaa kwa ajili ya kuuza kwa wateja wao


 Mkaa ukisubiri wateja.

-------


Na Edwin Moshi

Mafunzo ya ulinzi na usalama wa mtoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji yaliyoanza jana wilayani Makete mkoani Njombe yanaendelea katika ukumbi wa Sumasesu Tandala



Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Makete Bw. Leonce Panga yameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, dawati la jinsia kutoka kituo cha polisi Makete, maafisa elimu, mwanasheria, magereza, wauguzi, madaktari pamoja na hakimu mfawidhi wa wilaya ya Makete



Katika mafunzo hayo yanayowezeshwa na Bi Asha Mbaruku pamoja na Ramadhani Yahaya kutoka  ustawi wa jamii makao makuu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kuwahudumia watoto wanaokuwa wamefika kwenye ofisi zao kupata msaada endapo anakuwa amepata tatizo akitolea mfano kufukuzwa shule kwa kukosa ada


HABARI KAMILI BOFYA HAPA


TSHs.BIL 13.647 ZAANZA KUTUMIKA KATIKA UJENZI WA BARABARA NJOMBE



Meneja wa barabara Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana.
Jumla ya Shilingi Bilioni 13.647  Ambazo ni Bajeti ya Barabara Mkoa wa Njombe Kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 Zimetajwa Kuanza Kutumika Katika Kuboresha Miundombinu ya Barabara Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Hapa.

Pamoja na Fedha Hizo Kushindwa Kufika Zote Kwa Wakati Lakini Hadi Sasa Fedha za Kuwalipa Wakandarasi Wanaomaliza Kazi Zao Zinaendelea Kutolewa Kutokana na Sekta ya Miundombinu ya Barabara Kupewa Kipaumbele Kikubwa Hapa Nchini.

Meneja wa Tanroad Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana Amesema Kuwa Fedha Hizo ni Zile za Barabara Zenye Urefu wa Kilomita 1123.42 Katika Maeneo Yote ya Barabara za Mkoa Ambazo Baadhi ya Zabuni Bado Hazijakamilika.

Mhandisi Mazana Amesema Kati ya Fedha Hizo Shilingi Bilioni 3.150 Zinatoka Kwenye Mfuko wa Matengezo wa Barabara na Kiasi cha Shilingi Bilioni 10.497 Zinatoka Kwenye Mfuko wa Barabara Kuu.

Katika Hatua Nyingine Ameeleza Kuwa Jumla ya Kilomita 719.44  za Barabara ni za Mkoa na Kilomita 403.98 ni Barabara Kuu Ambazo Zinaendelea Kulimwa Katika Kipindi Chote cha Mwaka wa Fedha.

Hata Hivyo Amewataka Wakandarasi Hao Kuhakikisha Wanakamilisha Kazi Zao Kwa Kiwango Kilicho Pangwa na Kwa  Mujibu wa Mikataba Yao Ili Kuendana na Kasi ya Maendeleo Katika Mkoa wa Njombe.




WAKUU WA IDARA WATAKIWA KUSHIRIKISHA WANANCHI KATIKA MIRADI

Kukosekana kwa ushirikishwaji wa jamii katika kupanga, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao kunachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha uwajibikaji kwa jamii ambapo jamii inashindwa kushiriki kikamilifu katika kusimamia miradi husika.
 
 Hali hii inasababisha  jamii kushindwa kutambua na kushiriki katika miradi inayotekelezwa na hivyo kukosa uendelevu licha ya kuwa miradi hiyo ipo katika maeneo yao

hayo yamebainika mkoani  Njombe katika Wilaya ya Makete baada ya  timu ya  shirika wanachama MIICO, kutembelea miradi kadhaa ya maendeleo katika wilaya hiyo na kubaini kuwa kuna hali ya wananchi kutoshirikishwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri hiyo  Nganya  Ephraim amekiri kuwa udhaifu wa watendaji unachangia kuwepo kwa mapungufu  hayo na kudai kuwa tatizo ni watendaji hawakuwa na ushirikiano na wakuu wa idara katika miradi.
 
Waganga ‘KAMCHAPE’ wakamatwa kwa utapeli Tabora
SERIKALI  Wilayani Tabora imewapa onyo waganga wa kienyeji wanaotapeli wananchi kwa kujifanya wanawabaini wachawi,Maarufu kama kamchape,na kuwataka waachane na tabia hiyo ya kudanganya wananchi vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora,Suleiman Kumchaya,amesema hayo mara baada ya kukamatwa kwa waganga wawili ambao walikiri kufanya utapeli kupitia uganga na kuahidi kuachana na kazi ya kamchape.

Mtendaji wa kata ya Kabila katika manispaa ya Tabora,Bw.Godfrey Selula, amesema waganga hao wamekuwa wakifanya shughuli zao kinyume cha sheria wakiwa na vibali visivyojulikana wala kutambulika kuanzia ngazi ya wilaya hadi kwenye Vijiji.

Kwa upande wao waganga hao wa kienyeji maarufu kama kamchape,Mohamed Ally na Hamis Juma,wamekiri kujihusisha na utapeli kupitia uganga na kuahidi kuachana na shughuli hiyo ya utapeli.

Waganga hao  maarufu kama kamchape wamekuwa wakiitwa katika Vijiji mbalimbali kwenye wilaya za Mkoa wa tabora kwa lengo la kuwabaini wachawi ambapo wamekuwa wakitoza malipo makubwa kwa kazi hiyo huku wakiishia kuleta mifarakano miongoni mwa wananchi.

Walalamikia mchango mdogo

Njombe.Uchangiaji mdogo wa halmashauri katika sekta ya afya kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani, umeelezwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazovikabili vituo vingi vya kutolea huduma ya afya.
Hayo yalisemwa juzi na Mratibu wa Ukimwi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, Dk. Margreth Msasi, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya Tokomeza Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda mtoto.
Dk Msasi alisema hali hiyo inachagiza utekelezaji wa mpango wa kuzuia maambuki ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Alisema changangamoto nyingine katika utekelezaji wa mpango huo ni ukosefu wa dawa katika Bohari Kuu ya Dawa.

Chanzo;Mwananchi

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA MKOA WA NJOMBE LA CHELEWESHA HUDUMA YA KUUNGANISHA UMEME KWA WATEJA

 
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Njombe Mhandisi Emanuel  Kachewa Amesema Tatizo Hilo Limetokana na Upungufu wa Vifaa Unaolikabili Shirika Hilo

 Hii ni Orodha ya Majina ya Wateja Waliolipia Huduma Hiyo Lakini Bado Hawajapata Kwa Zaidi ya Miezi Saba Sasa.

Zaidi ya Wateja Mia Sita wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilayani Njombe Wameulalamikia Uongozi wa Shirika Hilo Kwa Kushindwa Kuwaunganishia Huduma ya Umeme Kwa Zaidi ya Miezi Sita Licha ya Kukamilisha Taratibu Zote Ikiwemo Malipo ya Huduma Hiyo.

Aidha Wateja Hao Wamelalamikia Kitendo Cha Shirika Hilo Kukiuka Mkataba wa Huduma Kwa Mteja Ambao Kwa Mujibu wa Wateja Hao Walitakiwa Kuunganishiwa Huduma Hiyo Ndani ya
Siku Thelathini Baada ya Kukamilisha Malipo na Kujaza Mkataba.

Wakizungumza na mwandishi wa mtandao huu Baadhi ya Wateja Hao Wamesema Licha ya Kufika Mara Kadhaa Katika Ofisi za Shirika Hilo Kwaajili ya Kufuatilia,Bado Kumekuwa Hakuna Majibu ya Uhakika Jambo Linalosababisha Kushindwa Kupata Huduma Hiyo Hadi Sasa.

Akizungumzia Hali Hiyo Meneja wa TANESCO Wilaya ya Njombe Mhandisi Emanuel  Kachewa Amesema Tatizo Hilo Limetokana na Upungufu wa Vifaa Unaolikabili Shirika Hilo Kwasasa na Kusema Hali Hiyo Imeendelea Kujitokeza Katika Mikoa Mbalimbali Nchini.

Kutokana na Hali Hiyo Bw Kachewa Amewataka Wateja Hao Kuendelea Wavumilivu Katika Kipindi Hiki Ambapo Shirika Hilo Linaendelea Kulitafutia Ufumbuzi Tatizo Hilo na Kuongeza Kuwa Tayari Shirika Hilo

Limezungumza na Wateja Hao na Kuwafahamisha Tatizo Lililopo Kwasasa.
Na  Prosper  Mfugale Njombe 

NI SIKU TATU TUU ZIMEBAKIA KUPATIKANA KWA MAMA SHUJAA WA CHAKULA , MPENDEKEZE SASA


Tshs. Milioni 5 Kushindaniwa

Kama unamfahamu mkulima yeyote mwanamke, mtanzania, mwenye umri wa miaka 18 na zaidi, anayelima mazao ya chakula, huu ni wakati wako sasa wa kumpa zawadi ya kufungia mwaka.

Kampeni ya Grow inayoendeshwa na shirika la kimataifa la Oxfam kupitia balozi wake Shamim Mwasha (Blogger 8020fashions) inatoa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 5 pamoja na nafasi ya ushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2013 litakalofanyika sambamba na Maisha Plus.

Mpendekeze ashinde sasa kwa kubofya hapa na kujaza nafasi zote  surveymonkey.com/s/growtanzania

Zimebaki siku tatu tu kabla ya shindano kufungwa. Usikubali nafasi hii ikupite. 

Kasi ya maambukizi VVU Njombe inatisha



KATIBU Tawala wa Mkoa wa Njombe, Mgeni Baruani, amesema kuna kazi kubwa ya kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika mikoa ya Njombe na Iringa ambayo kiwango cha maambukizi kiko juu.
 Baruani alitoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa kampeni ya Tokomeza Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, uliofanyika katika Kituo cha Afya cha mji mdogo wa Makambako.
 Alisema Tanzania imeanzisha mpango wa kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na wakati huohuo kunawawezesha kina mama hao kuendelea kuishi wakiwa na afya bora.
Alisema jambo muhimu katika mpango huu ni mjamzito kupima afya ili anapogundulika na maambukizi, hatua husika zichukuliwe ili asimwambukize baada ya kuzaliwa.
 Mpango huu utakaotekelezwa nchini kote unatarajiwa kufanyika kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itahusisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu na Kagera na ya pili inatahusisha mikoa mingine yote iliyobaki.
 Alisema mapambano ya maambukizi mapya ya VVU ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha yanatokomea kwa kuwajibika kufuata ushauri na kubadili mienendo katika maisha yao.
 Utoaji huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika mji wa Makambako ulianza tangu mwaka 2007 ambapo hadi kufikia mwaka 2013 Oktoba, watu 8,641 wamenufaika na huduma hiyo japo kina mama 1,148 walikutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
 Hata hivyo watoto 738 waliozaliwa na kina mama hao walipimwa, watoto 85 walikutwa na maambukizi ya VVU.
Mkoa wa Iringa unaongoza kuwa na maambukizi ya VVU kwa asilimia 19.1 wakati Mkoa wa Njombe ukiwa na maambukizi ya VVU kwa asilimia 14.8. 

Chanzo;Tanzania Daima

Apoteza maisha baada ya kudondokewa na kifusi Makete‏



Na Edwin Moshi, Makete
Mtu mmoja ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ivalalila kata ya Iwawa wilayani Makete amefariki dunia baada ya kudondokewa na kifusi cha mchanga wakati akichimba mchanga
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa upelezi wilayani Makete Bw.Gozbert Komba amemtaja mkazi huyo kuwa ni Daudi Ilomo (42)amesema kuwa amefariki dunia wakati akichimba mchanga kijijini hapo

Aidha ameongeza kuwa mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umevunjika mguu mara mbili,pia alitokwa na damu puani na masikioni baada ya kifusi hicho kumbana katika mwili wake hasa kifuani

Hata hivyo marehemu wakati wa uhai wake kwa mara ya mwisho alikuwa na Bw.Polito ilomo

Pia OCCID Komba ametoa wito kwa wananchi  wote kuwa makini pindi wanapokuwa katika maeneo wanaojua kuwa ni hatarishi kwao kuwa katika makundi ili kusaidiana na kujiepusha katika majanga kama ya aina hiyo

VIJANA WA MAKETE WATAKIWA KUTOPUUZA MAFUNZO YA MGAMBO‏


 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akikagua gwaride la wanamgambo
 Mkuu wa wilaya akitoa hotuba yake
Na Edwin Moshi, Makete
Vijana wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutambua kuwa suala la wao kushiriki mafunzo ya mgambo lipo kisheria hivyo kuitaka jamii kwa ujumla kushirikiana ili malengo ya mafunzo hayo yatimie

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Bi Josephine Matiro wakati akifunga mafunzo ya mgambo yaliyofanyika kwa kipindi cha miezi minne katika kata ya Lupila wilayani Makete

Bi Matiro amefikia hatua hiyo kutokana na risala ya mgambo hao kuonesha kuwa wapo walioandikishwa kushiriki mafunzo hayo lakini waliyakatisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uvivu na kutoona umuhimu wa mafunzo hayo ambapo awali waliandikishwa zaidi ya 150 lakini wamehitimu 61 tu

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya amewashauri mgambo hao kuanzisha kikundi chao cha ujasiriamali na endapo watafanya hivyo serikali itawapatia mikopo itakayowasaidia kujiendessha kupitia vikundi

Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya mgambo waliohitimu kwenye mafunzo wameshukuru na kusema kuwa wameelewa mambo mengi ikiwemo kutumia silaha, kukabiliana na adui hata kama ana silaha, mbinu za kivita pamoja na huduma ya kwanza

CCM WILYA YA NJOMBE YATAKA KUENDELEZWA KWA MIRADI KATA YA MATOLA.

7 2aac9
 Chama cha Mapinduzi Wilayani Njombe Kimewataka Wananchi wa Kata ya Matola Kuiendeleza Miradi ya Maendeleo Inayotekelezwa Katika Kata Hiyo Kwa Lengo la Kusogeza na Kuboresha Huduma za Kijamii.

Agizo Hilo Limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Adam Msigwa Wakati wa Ziara ya Siku Moja Iliyolenga Kutembelea na Kukagua Miradi ya Maendeleo Inayotekelezwa  Katika Kata Hiyo , Ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2010/2015.

Aidha Mwenyekiti Huyo Aliyeambatana na Viongozi Wengi wa CCM Wilaya   Kwenye Ziara Hiyo Wametembelea na Kukagua Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa, Mabweni , Nyumba za Walimu, Zahanati, Pamoja na Vyoo Vya

Miradi Ambayo Inagharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 297  Hadi Kukamilika Kwake.

Akiongea na Wananchi wa Kata ya Matola  Katibu Mwenezi wa CCM  Wilaya ya Njombe Hitra Msola Amewataka Wananchi wa Kata Hiyo Kuwapuuza Watu Wanao Eneza Udini na Ukabila Kwani Husababisha Migogoro Katika Jamii.

Katika Hatua Nyingine Bwana Msigwa Amempongeza Diwani wa  Kata Hiyo Edwini Mwanzinga Pamoja na Wananchi  Wake Kwa Ushirikiano Waliyouonesha Katika Kusimamia Miradi ya Maendeleo na Kuhakikisha Wanasogeza Huduma za Kijamii.
 
Na  Steven  Ngole Njombe

WADAU WA MFUKO WA BIMA YA AFYA MKOA WA NJOMBE WAKUTANA LEO

Kaimu Mkurugenzi mkuu  wa NHIF Hamisi Mdee akitoa taarifa ya Utekelezaji ya kuanzia 2001 hadi June 2013,
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Balozi Ali  Mchumo akitoa salamu za NHIF kwa washiriki wa mkutano
RAS wa Njombe akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ktp. Mstaafu Assery Msangi, amesisitiza umuhimu wa kufanya NHIF/CHF/TIKA kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya maamuzi mkoani humo ili hatimaye wakazi wote wa mkoa wa Njombe wapate huduma za matibabu kupitia utaratibu wa kuchagia kabla
meneja uendeshaji wa NHIF, Salome Manyama akiwasilisha mada katika mkutano huo, picha ya tano wadau wa mkoa a Njombe wakifuatilia mada..

Fundi wa kujenga barabara achapwa bakora Ludewa

Alitakiwa kuondoa kifusi barabarani ili ofisa mmoja wa masuala ya usalama apite, akashindwa kwa vile katapila liliharibika, akaishia kuchapwa viboko hadharani 
Njombe. Mtu anayedaiwa kujihusisha na masuala ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ludewa, anadaiwa kumshambulia kwa kumchapa bakora mfanyakazi wa Kampuni ya Boimanda Modern Construction Company Ltd (BMCC) Alphonce Lutengano (25) inayofanya ukarabati wa kilomita 56.5 za Barabara ya Njombe-Ludewa-Manda.
Tukio hilo la aina yake limetokea hivi karibuni katika Kijiji cha Muholo, Kata ya Luana Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe wakati mfanyakazi huyo akiwa kazini,  baada ya ofisa huyo kukuta vifusi vimemwagwa katikati ya barabara wakati akipita kwenda Kata ya Lugarawa kwenye shughuli zake.
Apigwa akiwa kazini
Lutengano anadai kuwa akiwa kazini na mtumishi mwenzake Mary Luca wakisubiri katapila lao lililokuwa linazibwa baada ya gurudumu moja kupata hililafu ili kusambaza vifusi hivyo, ofisa huyo alifika eneo hilo akiwa na mwenzake ndani ya gari akitumia gari aina Nissan Hard Top, alianza kumhoji kwa nini wamemwaga kifusi katikati ya barabara na kumtaka akitoe ili apitishe gari lake kwa madai kuwa haliwezi kupita pembeni kama walivyomshauri.
“Aliponihoji nilimwambia tunasubiri katapila ili tuweze kusambaza kifusi, kwani wakati huo lilikuwa linazibwa baada ya gurudumu moja kuishiwa upepo. Nikamshauri apite pembeni, akakataa akisema nisambaze kifusi haraka ili apite akidai kuwa gari lake haliwezi kupita pembeni. Alisisitiza kuwa tufanye hivyo haraka vinginevyo atanipa adhabu,” anasema na kuongeza.
“Nilidhani utani, ghafla kweli akachuma fimbo ya mti na kuanza kunipiga huku mwenzake akishuhudia, baada ya kuona hivyo mwenzangu alikimbia ndipo nikatoa taarifa kwa mkuu wangu wa kazi Ludewa akaja na polisi wakamkuta”.
Baada ya polisi kujibiwa hivyo walimwacha kwa madai kuwa aende akaendelee na majukumu yake baada ya hapo aripoti kituoni.
Shuhuda anena
Shuhuda wa tukio hilo Mwalimu mstaafu Gerald Meshack Hiluka mkazi wa Muhola akielezea mkasa huo anasema “Mimi niliona mtu anachapwa wakati natoka kumwagilia bustani, sasa nikabaki nimeduwaa kwa mshangao, na sikujua anayemchapa kijana huyu ni nani kwa kuwa nilikuwa napita, hivyo nikabaki naangalia tu”.
Kwa upande wake, Mary Luca anasema baada ya kuona hivyo aliamua kukimbia ili kujinusuru na kipigo ambacho kingeweza hata yeye kumpata.
Fundi Sanifu wa BMCC , Taji Omary alikiri kupokea taarifa ya kupigwa mfanyakazi na kutoa taarifa Kituo cha Polisi Ludewa wakaongozana kwenda eneo la tukio lakini walipofika licha ya polisi kumkuta mtuhumiwa walimwacha aendelee na safari yake kana kwamba tukio alilotenda ni jema kwa jamii.

chanzo;mwananchi.

Tazama matokeo ya shule alizozuru mkuu wa wilaya ya Makete wakati wakifanya mtihani wao wa mwisho wa darasa la Saba‏


Ikiwa zimepita siku chache tangu kutangazwa matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba nchi nzima mwaka 2013, mkuu wa wilaya ya makete mkoani Njombe Josephine Matiro mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu alitembelea baadhi ya shule za msingi wilayani mwake na kuzungumza na wanafunzi waliokuwa wakifanya mtihani huo

Akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule hizo mh Matiro aliambiwa na wanafunzi hao kuwa mitihani hiyo ambayo walikuwa wameshaifanya na mingine ilikuwa bado, kuwa ilikuwa mirahisi na wote watachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani kwani wote watafaulu

Wanafunzi hao walimweleza mkuu wa wilaya kuwa wamesoma kwa bidii na wanauhakika wa kufaulu hata mitihani ambayo walikuwa hawajaifanya kwa muda huo ambao mkuu huyo alikuwa anazungumza nao

Kitu ambacho mtandao huu ulikikariri kutoka kwa mh Matiro ni kuwataka kuwa makini na kutopaniki wakati wakifanya mitihani yao na kuwa anategemea wote watafaulu

Ifuatayo hapa chini ni tathmini ya haraka yenye kuonesha matokeo ya wanafunzi wa shule za msingi alizoweza kuzitembelea mkuu wa wilaya ya Makete na kuahidiwa kuwa watafaulu, jionee mwenyewe matokeo ya shule hizo alizozitembelea mkuu wa wilaya

Angalia matokeo ya jumla tuu kwa kila shule aliyoitembelea mkuu wa wilaya

1.MASISIWE PRIMARY SCHOOL - P2602061

WALIOFANYA MTIHANI : 22
WASTANI WA SHULE : 107.7273
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 47 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 210 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 5479 kati ya 15656
==========

2. IKETE PRIMARY SCHOOL - P2602008

WALIOFANYA MTIHANI : 13
WASTANI WA SHULE : 109.7692
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 37 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 183 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 4989 kati ya 15656 
======

3. MALIWA PRIMARY SCHOOL - P2602059

WALIOFANYA MTIHANI : 29
WASTANI WA SHULE : 91.4138
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 80 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 362 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 10137 kati ya 15656
 -----=====

4.SUNJI PRIMARY SCHOOL - P2602080

WALIOFANYA MTIHANI : 35
WASTANI WA SHULE : 99.9429
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 66 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 289 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 7504 kati ya 15656
=====

5.LUPILA PRIMARY SCHOOL - P2602043

WALIOFANYA MTIHANI : 30
WASTANI WA SHULE : 99.7333
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 68 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 296 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 7579 kati ya 15656 
======
Mkuu wa wilaya akiwa Lupila shule ya Msingi

6.TANDALA PRIMARY SCHOOL - P2602081

WALIOFANYA MTIHANI : 45
WASTANI WA SHULE : 117.0667
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 26 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 126 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 3530 kati ya 15656
 ======

7.LUPALILO PRIMARY SCHOOL - P2602042

WALIOFANYA MTIHANI : 29
WASTANI WA SHULE : 136.3793
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 9 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 48 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 1369 kati ya 15656 
=======

8.MAGO PRIMARY SCHOOL - P2602048

WALIOFANYA MTIHANI : 21
WASTANI WA SHULE : 108.1429
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 43 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 199 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 5371 kati ya 15656 
=======

9.KISINGA PRIMARY SCHOOL - P2602036

WALIOFANYA MTIHANI : 25
WASTANI WA SHULE : 108.0000
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 44 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 202 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 5406 kati ya 15656 

=========

10.NDULAMO PRIMARY SCHOOL - P2602075

WALIOFANYA MTIHANI : 83
WASTANI WA SHULE : 92.1446
NAFASI YA SHULE KIWILAYA: 78 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KIMKOA : 357 kati ya 454
NAFASI YA SHULE KITAIFA : 9904 kati ya 15656

Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiongea na wanafunzi wa Ndulamo wakati wakifanya mitihani yao ya mwisho. Na Edwin Moshi

Wanafunzi wa kike ikuwo sekondari MAKETE NJOMBE wanalala chini‏


 Wanafunzi wa kike wa Ikuwo sekondari kwa sasa wanalala hapa kama ilivyoshuhudiwa na mtandao huu.
 kama kawaida wamepanga magodoro yao chini kwa raha zao
 Mkuu wa shule ya Ikuwo Sekondari akifafanua jambo kwa mwandishi wetu.
=====

Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana na idadi ya wanafunzi wengi wa kike wilayani Makete mkoani Njombe kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba, shule ya sekondari Ikuwo imeonesha kukerwa na tatizo hilo na kuamua kuchukua hatua za awali za kupambana nalo

Mwandishi wa mtandao huu alifika shuleni hapo na kukuta wanafunzi wa kike wote wakiwa wanalala shuleni hapo licha ya mabweni hayo kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa vitanda

Mkuu wa shule hiyo akizungumza na mwandishi wetu amesema kutokana na tatizo hilo kuzidi kuwa kubwa, uongozi wa shule na wilaya kwa ujumla walikubaliana wanafunzi hao watandike magodoro sakafuni waendelee kulala mabwenini humo, wakati serikali ikiendelea kutafuta vitanda kwa ajili ya mabweni hayo

"Kwa wakati huu ambao tunasubiri kuletewa vitanda na serikali, tumeona ni bora wanafunzi hawa wa kike waendelee kulala chini kwa kutandika matandiko yao ili kupunguza ukubwa wa kupata mimba pamoja na kufeli" alisema mwalimu mkuu huyo

Mtandao huu ulipenya kwenye mambweni hayo na kushuhudia magodoro yaliyotandikwa kwa unadhifu wa hali ya juu, ambapo wanafunzi hao wanalala kwa muda wakisubiria vitanda

Hivi karibuni katika mahafali ya kidato cha nne Iwawa sekondari afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena alikaririwa akisisitiza wanafunzi wa kike wa shule hiyo waanze kulala shuleni kuanzia mwakani hata kama mabweni hayana vitanda kama wanavyofanya Ikuwo sekondari
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa