MAUAJI ya vikongwe
yameendelea kushamiri katika mkoa wa Njombe kutokana na imani za kishirikina
zinazochochewa na waganga wa jadi ambao hupiga ramri chonganishi na kusababisha
jamii kutokuwa na amani na ndugu zao..
Imeelezwa katika
mwaka 2013 mauaji yanayoshabihiana na Imani za kishirikiana yameripotiwa kwa
watu zaidi ya 17 kuuawa kikatiri katika wilaya za Ludewa, makete,Njombe na
Wangong’ombe.
Serikali kwa
kushirikiana na jeshi la polisi limekuwa likitoa likitoa elimu kwa wananchi
kutokimbilia kwa waganga wa tiba asilia, kupiga Ramri hizo jambo hilo
limeonekana kuwa tatizo sugu katika mkoa huo.
Akizungumaza katika
kikao cha mwaka cha waganga wa jadi Dkt. Maria Lupenza amesema, kuwa
zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa hutumia tiba asilia kabla ya kufika katika
vituo vya tiba za hospitali na Zahanati jambo ambalo linaonesha ni kwa
zaidi ya asilimia 50 ya watanzania bado wanaamini zaidi tiba za asili.
Salumu Mkalla ni
Inspekta wa jeshi la polisi katika kikao hicho ameeleza kuwa mauaji ambayo
yametokea katika kip[indi cha mwaka mengi kati ya hayo yanashabihiana na imani
za kishirikina kutokana na mazingirz ya kifo hata hivyo ameonya waganga hao
kukomesha mara moja huduma ya ramri.
Menyekiti wa chawatiata mkoani humo Salumu Lugenge amesema
waganga wanaotoa huduma ya kupiga ramri ni wa kutoka nje ya mkoa na hufanya
kazi hiyo kwa kujiotangaza kupitia vyombo vya habari kisha hutoweka mara
yanapotokea mauaji ambayo ni matokeo ya kazi yao.
0 comments:
Post a Comment