Juma Msam Swedi mtumishi wa
wizara ya mambo ya ndani kitengo cha askari magereza wilayani Makete mkoa wa Njombe
amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa
iliyokuwa na lengo la kumuachia huru mfungwa anayetumikia kifungo gerezani
wilayani hapo.
Akisoma hati ya mashtaka
mbele ya hakimu mkazi wa wilaya John Kapokolo mwendesha mashtaka wa TAKUKURU
mkoani Njombe Bw. Colman Njau amesema kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kwa makosa
mawili ambayo aliyafanya mwezi Julai mwaka huu eneo la Ivalalila wilayani hapo
ambapo kosa la kwanza ni kushawishi kupewa rushwa ya laki mbili na elfu hamsini
kutoka kwa Felix Kivengi Sanga ili kuweza
kumuachia huru Godfrey Mahenge ambaye bado anaendelea kutumikia kifungo
kwa sasa.
Kosa la pili kupokea rushwa
kiasi cha laki mmoja kutoka Felix
Mahenge ili kumwachia huru mfungwa huyo kinyume cha sheria TAKUKURU sura
ya 15 kwenye mabano mmoja A ya mwaka 2007.
Hata
hivyo mshitakiwa Juma Swedi alipoulizwa mahakamani hapo alikana
kuhusika na tukio hilo na mheshimiwa hakimu Kapokolo ameiharisha kesi
hiyo hadi Desemba 13 mwaka huu na
mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na upelelezi wa tukio hilo bado
unaendelea.
0 comments:
Post a Comment