WANANCHI wa kijiji
cha Ikondo mkoani Njombe wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi
ya askari wa jeshi la polisi kuwadai fedha kama gharama ya kuwafikia
kijijini hapo mara wanapo ripoti kuwepo kwa matukio tofauti kama vifo na
mengineyo.
Hayo yamebainishwa na
wananchi katika mkutano ulioitishwa na serikali ya kijiji baada ya kutembelewa
na kamati ya ushauri ya wilaya, ambayo imefika katika kata hiyo kufanya mkutano
na wananchi ili kubaini mapungufu ya kiutendaji na kuyatafutia ufumbuzi.
Ezkieli Mhenga ni
mmoja kati ya wananchi ambao wamefunguka kwa kulitupia lawama jeshi la polisi
kuwa hutozwa fedha zaidi ya laki tano hadi milioni tano iwapo watatoa taarifa
za kuwepo kwa matukio kama ya mtu kujinyonga fedha ambazo askari hudai kuwa ni
kwaaajili ya mafuta ya gari.
Akizungumza kwa niaba
ya jeshi la Polisi Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi Issa Asali amewashauri
wananchi hao kuwa jeshi hilo linapaswa kutoa huduma bure na iwapo watakutana na
askari anayedai fedha kama malipo ya kazi taarifa zitolewe kwa viongozi ili
kumshughulikia kisheria askari atakaye bainika kupokea fedha hizo.
Katika hatua nyingine
wameelekeza malalamiko yao katika sekta ya afya wanawake wajawazito na
watoto chini ya miaka mitano kutozwa fedha , Conradi Ugonile ni mganga
mkuu wa Wilaya amesema, huduma za watoto na wajawazito ni bure, wakati
mkuu wa Wilaya Sarah Dumba amesema kero za wananchi zinashughulikiwa, ikiwemo
ukosefu wa dawa katika zahanati na bajeti ya mwaka 2013/14 fedha kwaajili ya
kuboresha miundo mbinu imetengwa kinasubiriwa ni utekelezaji
0 comments:
Post a Comment