UTENDAJI KAZI WA MBUNGE FILIKUNJOMBE WAWAVUTIA WAPIGA KURA WAAMUA KUMBEBA MGONGONI

Wananchi wa kata ya Manda Ludewa wakimfuta jasho mbunge wao Deo Filikunjombe kama kumpongeza kwa utekelezaji mzuri wa ahadi na uwakilishi uliotukuka bungeni Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebebwa na mpiga kura wake kama kumpongeza kwa utendaji wake mzuri Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akifurahia baada ya kupongezwa kwa kubebwa mgongoni na mpiga kura wake Mbunge Filikunjombe kati akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mkazi wa manda huku mkewe Habiba akishukuru (picha na Blogu ya Francis Godwin) ...

HIVI NDIVYO JINSI STENDI YA NJOMBE ILIVYOKUWA KERO KWA WANAINCHI

Mpiga picha  wa Clouds TV  akiwajibika   kuchukua  tukio la ubovu wa  stendi  ya Njombe  Abiria   wakipita kwa shida katika  stendi ya  Njombe  Mwanahabari  wa Clouds TV na Radio Recho akitafuta  eneo la  kupita  katika  stendi  hiyo ya Njombe  Madereva  na  abiria   wanaotumia  stendi ya Njombe mjini  ambayo ni stendi kuu ya mabasi  yaendayo mikoani  wamelalamikia  ubovu  wa stendi  hiyo na kumwomba  mbunge wa  jimbo  hilo Anne  Simamba  Makinda  kushughulikia...

KIJIJI CHA IKONDO KINAKABILIWA KERO MBALIMBALI.

WANANCHI wa kijiji cha Ikondo mkoani Njombe wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya askari wa jeshi la  polisi kuwadai fedha kama gharama ya kuwafikia kijijini hapo mara  wanapo ripoti kuwepo kwa matukio tofauti kama vifo na mengineyo. Hayo yamebainishwa na wananchi katika mkutano ulioitishwa na serikali ya kijiji baada ya kutembelewa na kamati ya ushauri ya wilaya, ambayo imefika katika kata hiyo kufanya mkutano na wananchi ili kubaini mapungufu ya kiutendaji na kuyatafutia ufumbuzi. Ezkieli Mhenga ni mmoja kati ya wananchi ambao wamefunguka kwa kulitupia lawama jeshi la polisi kuwa hutozwa fedha zaidi ya laki tano hadi milioni tano iwapo watatoa taarifa za kuwepo kwa matukio kama ya mtu kujinyonga fedha ambazo askari hudai kuwa ni kwaaajili ya mafuta ya...

WAGANGA WA JADI NJOMBE CHANZO CHA MAUAJI YA VIKONGWE

MAUAJI ya vikongwe yameendelea kushamiri katika mkoa wa Njombe kutokana na imani za kishirikina zinazochochewa na waganga wa jadi ambao hupiga ramri chonganishi na kusababisha jamii kutokuwa na amani na ndugu zao.. Imeelezwa katika mwaka 2013 mauaji yanayoshabihiana na Imani za kishirikiana yameripotiwa kwa watu zaidi ya 17 kuuawa kikatiri katika wilaya za Ludewa, makete,Njombe na Wangong’ombe. Serikali kwa kushirikiana na jeshi la polisi limekuwa likitoa likitoa elimu kwa wananchi kutokimbilia kwa waganga wa tiba asilia, kupiga Ramri hizo  jambo hilo limeonekana kuwa tatizo sugu katika mkoa huo. Akizungumaza katika kikao cha mwaka cha waganga wa jadi Dkt. Maria Lupenza amesema, kuwa  zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa hutumia tiba asilia kabla ya kufika katika vituo...

IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA NJOMBE YAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO YATIMA

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama Akimkabidhi Vitu Mbalimbali Mwakilishi wa Watoto Yatima.  Bi.Rose Mhagama Akitoa Taarifa ya Gharama za Msaada walioutoa Kwa Watoto Yatima Leo Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Njombe Wakiongozwa na Afisa Uhamiaji Mkoa Bi.Rose Mhagama Leo Wamekabidhi Misaada Mbalimbali Kwa Watoto Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu na Yatima Vyenye Thamani Ya Zaidi ya Shilingi Laki Nne.Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Misaada Hiyo Kwa Mwakilishi wa Watoto Yatima Afisa Uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama Amesema Kuwa Vitu Hivyo Wameamua Kuvitoa Kama Watumishi Kwa Kutambua Adha Wanazozipata Watoto Yatima...

Namna ya kuishi na mtoto mwenye vvu-1

Wiki iliyopita tuliona uchunguzi na matibabu kwa mtoto mwenye virusi vya Ukimwi, leo tunaendelea na mada hiyo na tutaangalia jinsi ya kuishi na mtoto wa mwenye VVU. Zingatia ushauri na matibabu. Mzazi au mlezi kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa afya wenye mafunzo maalumu ya VVU na Ukimwi ni jambo muhimu sana kwani itakufanya ulifahamu tatizo na namna ya kukabiliana nalo. Kupata kwako elimu hiyo kutakusaidia kulinda afya ya mtoto wako. Kama mtoto mwenye VVU alishaanza matibabu ya dawa za kufubaza makali ya VVU na dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi, hakikisha kuwa mtoto anapata dawa bila kukosa kwani dawa hizi hupewa maisha yake yote. Ni muhimu kufuata masharti kwani dawa...

ABIRIA WALIOKUWA WAKISAFIRI NA BASI LA UKINGA EXPRESS WANUSURIKA KIFO KUFUATIA AJALI MBAYA WILAYANI MAKETE

 Muonekano wa Basi la Ukinga Express likiwa kwenye eneo la ajali. Abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la Ukinga Express kutoka Njombe kwenda Makete mkoani Njombe, wamenusurika kifo baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuigonga fuso kwa nyuma iliyokuwa imepata hitilafu na kuegeshwa barabarani Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo linalohofiwa na wengi la Lwamadovela kata ya Tandala wilayani Makete, baada ya dereva wa basi hilo kuigonga kwa nyuma fuso hiyo ambayo ilipata hitilafu kwenye eneo lenye kona Wakizungumza na mwandishi wa eddy blog aliyefika eneo la tukio na kushuhudia ajali hiyo, mashuhuda hao bila...

Picha: Mvua zaanza kuleta kizaazaa Wilayani Makete

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi hivi sasa wilayani Makete, zimeshaanza kuleta madhara baada ya magari kuanza kuteleza kutokana na aina ya kifusi kilichomwagwa katika eneo la Mang'oto wilayani Makete barabara ya Makete - Njombe, kuteleza kupita kiasi Pichani hapo juu ni basi ma Mwafrika linalofanya safari zake kati ya Iringa-Makete likiwa limekwama kwa muda Kutokana na mvua zinazonyesha wilayani Makete, na hapa ni katika kata ya Mang'oto wilayani hapo, mita chache tu kabla ya kufika kwenye lami Hii inatokana na kifusi kilichowekwa kwenye barabara hiyo kuonekana na utelezi wa hali ya juu pindi mvua inaponyesha hata...

KINANA ATEMBELEA CHUO CHA VETA MAKETE

 Katibu mkuu wa CCM Ndg Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa chuo cha ufundi stadi VETA Makete wakati alipotembelea chuo hicho mapema leo jioni  Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa kimataifa Dkt. Asharose Migiro (wa pili kulia) akicheza muziki wa kuifagilia CCM wakati alipotembelea chuo cha VETA Makete, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro naye akicheza muziki  Mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini Monica Mbele akisoma taarifa ya chuo cha VETA Makete kwa katibu mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana Mkurugenzi Monica akikabidhi taarifa ya chuo cha veta Makete kwa Ndugu Kinana  Katibu wa...

Kevela Kamanda mpya UVCCM

MBUNGE wa zamani wa Njombe, Yono Stanley Kevela  amechaguliwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa UVCCM wa Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa mpya wa Njombe. Kevela ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Njombe kati ya mwaka 2005-2010 anatarajiwa kusimikwa rasmi kwenye nafasi hiyo keshokutwa mkoani Njombe. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya uteuzi huo, Kevela aliwashukuru viongozi wote wa CCM kwa kumwamini na kusema kuwa amebaki na deni kubwa la kukitumikia chama hicho kwa uadilifu na uaminifu mkubwa. “Nawashukuru wanaCCM wenzangu kuanzia ngazi ya mabalozi, tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa kwa kuona ninafaa...

HOT NEWS: ASKARI MAGEREZA WILAYANI MAKETE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Juma Msam Swedi mtumishi wa wizara ya mambo ya ndani kitengo cha askari magereza wilayani Makete mkoa wa Njombe amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa iliyokuwa na lengo la kumuachia huru mfungwa anayetumikia kifungo gerezani wilayani hapo. Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi wa wilaya John Kapokolo mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoani Njombe Bw. Colman Njau amesema kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo aliyafanya mwezi Julai mwaka huu eneo la Ivalalila wilayani hapo ambapo kosa la kwanza ni kushawishi kupewa rushwa ya laki mbili na elfu hamsini kutoka kwa Felix Kivengi...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa