Wananchi
wa kata ya Manda Ludewa wakimfuta jasho mbunge wao Deo
Filikunjombe kama kumpongeza kwa utekelezaji mzuri wa ahadi na
uwakilishi uliotukuka bungeni
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebebwa na mpiga kura wake kama kumpongeza kwa utendaji wake mzuri
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akifurahia baada ya kupongezwa kwa kubebwa mgongoni na mpiga kura wake
Mbunge
Filikunjombe kati akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mkazi wa
manda huku mkewe Habiba akishukuru (picha na Blogu ya Francis Godwin)
...
HIVI NDIVYO JINSI STENDI YA NJOMBE ILIVYOKUWA KERO KWA WANAINCHI
Mpiga picha wa Clouds TV akiwajibika kuchukua tukio la ubovu wa stendi ya Njombe
Abiria wakipita kwa shida katika stendi ya Njombe
Mwanahabari wa Clouds TV na Radio Recho akitafuta eneo la kupita katika stendi hiyo ya Njombe
Madereva
na abiria wanaotumia stendi ya Njombe mjini ambayo ni stendi kuu
ya mabasi yaendayo mikoani wamelalamikia ubovu wa stendi hiyo na
kumwomba mbunge wa jimbo hilo Anne Simamba Makinda kushughulikia...
KIJIJI CHA IKONDO KINAKABILIWA KERO MBALIMBALI.
WANANCHI wa kijiji
cha Ikondo mkoani Njombe wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi
ya askari wa jeshi la polisi kuwadai fedha kama gharama ya kuwafikia
kijijini hapo mara wanapo ripoti kuwepo kwa matukio tofauti kama vifo na
mengineyo.
Hayo yamebainishwa na
wananchi katika mkutano ulioitishwa na serikali ya kijiji baada ya kutembelewa
na kamati ya ushauri ya wilaya, ambayo imefika katika kata hiyo kufanya mkutano
na wananchi ili kubaini mapungufu ya kiutendaji na kuyatafutia ufumbuzi.
Ezkieli Mhenga ni
mmoja kati ya wananchi ambao wamefunguka kwa kulitupia lawama jeshi la polisi
kuwa hutozwa fedha zaidi ya laki tano hadi milioni tano iwapo watatoa taarifa
za kuwepo kwa matukio kama ya mtu kujinyonga fedha ambazo askari hudai kuwa ni
kwaaajili ya mafuta ya...
WAGANGA WA JADI NJOMBE CHANZO CHA MAUAJI YA VIKONGWE
MAUAJI ya vikongwe
yameendelea kushamiri katika mkoa wa Njombe kutokana na imani za kishirikina
zinazochochewa na waganga wa jadi ambao hupiga ramri chonganishi na kusababisha
jamii kutokuwa na amani na ndugu zao..
Imeelezwa katika
mwaka 2013 mauaji yanayoshabihiana na Imani za kishirikiana yameripotiwa kwa
watu zaidi ya 17 kuuawa kikatiri katika wilaya za Ludewa, makete,Njombe na
Wangong’ombe.
Serikali kwa
kushirikiana na jeshi la polisi limekuwa likitoa likitoa elimu kwa wananchi
kutokimbilia kwa waganga wa tiba asilia, kupiga Ramri hizo jambo hilo
limeonekana kuwa tatizo sugu katika mkoa huo.
Akizungumaza katika
kikao cha mwaka cha waganga wa jadi Dkt. Maria Lupenza amesema, kuwa
zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa hutumia tiba asilia kabla ya kufika katika
vituo...
IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA NJOMBE YAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO YATIMA
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama Akimkabidhi Vitu Mbalimbali Mwakilishi wa Watoto Yatima.
Bi.Rose Mhagama Akitoa Taarifa ya Gharama za Msaada walioutoa Kwa Watoto Yatima Leo
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Njombe Wakiongozwa na Afisa Uhamiaji Mkoa Bi.Rose Mhagama Leo Wamekabidhi Misaada Mbalimbali Kwa Watoto Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu na Yatima Vyenye Thamani Ya Zaidi ya Shilingi Laki Nne.Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Misaada Hiyo Kwa Mwakilishi wa Watoto Yatima Afisa Uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama Amesema Kuwa Vitu Hivyo Wameamua Kuvitoa Kama Watumishi Kwa Kutambua Adha Wanazozipata Watoto Yatima...
Namna ya kuishi na mtoto mwenye vvu-1
Wiki iliyopita tuliona uchunguzi na matibabu kwa mtoto mwenye
virusi vya Ukimwi, leo tunaendelea na mada hiyo na tutaangalia jinsi ya
kuishi na mtoto wa mwenye VVU.
Zingatia ushauri na matibabu.
Mzazi au mlezi kupata ushauri nasaha kutoka kwa
wataalamu wa afya wenye mafunzo maalumu ya VVU na Ukimwi ni jambo muhimu
sana kwani itakufanya ulifahamu tatizo na namna ya kukabiliana nalo.
Kupata kwako elimu hiyo kutakusaidia kulinda afya ya mtoto wako.
Kama mtoto mwenye VVU alishaanza matibabu ya dawa
za kufubaza makali ya VVU na dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi,
hakikisha kuwa mtoto anapata dawa bila kukosa kwani dawa hizi hupewa
maisha yake yote. Ni muhimu kufuata masharti kwani dawa...
ABIRIA WALIOKUWA WAKISAFIRI NA BASI LA UKINGA EXPRESS WANUSURIKA KIFO KUFUATIA AJALI MBAYA WILAYANI MAKETE

Muonekano wa Basi la Ukinga Express likiwa kwenye eneo la ajali.
Abiria
waliokuwa wakisafiri kwa basi la Ukinga Express kutoka Njombe kwenda
Makete mkoani Njombe, wamenusurika kifo baada ya basi hilo walilokuwa
wakisafiria kuigonga fuso kwa nyuma iliyokuwa imepata hitilafu na
kuegeshwa barabarani
Ajali
hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo linalohofiwa na wengi la
Lwamadovela kata ya Tandala wilayani Makete, baada ya dereva wa basi
hilo kuigonga kwa nyuma fuso hiyo ambayo ilipata hitilafu kwenye eneo
lenye kona
Wakizungumza
na mwandishi wa eddy blog aliyefika eneo la tukio na kushuhudia ajali
hiyo, mashuhuda hao bila...
Picha: Mvua zaanza kuleta kizaazaa Wilayani Makete

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi hivi sasa wilayani Makete, zimeshaanza kuleta madhara baada ya magari kuanza kuteleza kutokana na aina ya kifusi kilichomwagwa katika eneo la Mang'oto wilayani Makete barabara ya Makete - Njombe, kuteleza kupita kiasi
Pichani hapo juu ni basi ma Mwafrika linalofanya safari zake kati ya Iringa-Makete likiwa limekwama kwa muda Kutokana na mvua zinazonyesha wilayani Makete, na hapa ni katika kata ya Mang'oto wilayani hapo, mita chache tu kabla ya kufika kwenye lami
Hii inatokana na kifusi kilichowekwa kwenye barabara hiyo kuonekana na utelezi wa hali ya juu pindi mvua inaponyesha hata...
KINANA ATEMBELEA CHUO CHA VETA MAKETE
Katibu
mkuu wa CCM Ndg Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa chuo cha ufundi
stadi VETA Makete wakati alipotembelea chuo hicho mapema leo jioni
Katibu
wa NEC Siasa na uhusiano wa kimataifa Dkt. Asharose Migiro (wa pili
kulia) akicheza muziki wa kuifagilia CCM wakati alipotembelea chuo cha
VETA Makete, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro
naye akicheza muziki
Mkurugenzi
wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini Monica Mbele akisoma taarifa ya
chuo cha VETA Makete kwa katibu mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana
Mkurugenzi Monica akikabidhi taarifa ya chuo cha veta Makete kwa Ndugu Kinana
Katibu wa...
Kevela Kamanda mpya UVCCM
MBUNGE
wa zamani wa Njombe, Yono Stanley Kevela amechaguliwa kuwa Kamanda wa
Umoja wa Vijana wa UVCCM wa Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa mpya wa
Njombe.
Kevela ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Njombe kati ya mwaka 2005-2010
anatarajiwa kusimikwa rasmi kwenye nafasi hiyo keshokutwa mkoani Njombe.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya uteuzi huo, Kevela
aliwashukuru viongozi wote wa CCM kwa kumwamini na kusema kuwa amebaki
na deni kubwa la kukitumikia chama hicho kwa uadilifu na uaminifu
mkubwa.
“Nawashukuru wanaCCM wenzangu kuanzia ngazi ya mabalozi, tawi, kata,
wilaya, mkoa hadi taifa kwa kuona ninafaa...
HOT NEWS: ASKARI MAGEREZA WILAYANI MAKETE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Juma Msam Swedi mtumishi wa
wizara ya mambo ya ndani kitengo cha askari magereza wilayani Makete mkoa wa Njombe
amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa
iliyokuwa na lengo la kumuachia huru mfungwa anayetumikia kifungo gerezani
wilayani hapo.
Akisoma hati ya mashtaka
mbele ya hakimu mkazi wa wilaya John Kapokolo mwendesha mashtaka wa TAKUKURU
mkoani Njombe Bw. Colman Njau amesema kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kwa makosa
mawili ambayo aliyafanya mwezi Julai mwaka huu eneo la Ivalalila wilayani hapo
ambapo kosa la kwanza ni kushawishi kupewa rushwa ya laki mbili na elfu hamsini
kutoka kwa Felix Kivengi...