Mkuu wa mkoa wa NjombeKaptain Mstaafu Asseri Msangi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kaptain Mstaafu Asseri Msangi (aliyekaa wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Hassan Majaar Trust Bi. Zena Maajar Tenga (waliosimama wa pili kushoto) na Mwakilishi kutoka Kampuni ya Tigo pamoja na baadhi ya Walimu na Wanafunzi wakiwa katika picha ya ukumbusho.
Wanafunzi wakionyesha furaha baada ya kuboreshewa mazingira ya kusoma na Taasisi ya Hassan Maajar Trust ambayo lengo lake ni kutatua tatizo la Madawati nchini na kuhakikisha kauli mbiu yao ya “Dawati kwa kila mwanafunzi” inatim...
MAFUTA YA PETROLI YAADIMIKA MKOANI NJOMBE
Festus Pangani, Njombe Yetu
Kwa siku ya tatu sasa mji wa Njombe umekumbwa na adha ya
kukosekana kwa nishati ya mafuta ya petroli kwenye vituo vya mafuta hali
inayopelekea kukwama kwa usafiri na kushuka kwa uchumi miongoni mwa jamii.
Hali hiyo imetokea kuanzia septemba 30 mwezi uliopita hadi
sasa ambapo hadi hii leo ni kituo kimoja tu cha mafuta cha Ndime PetrolSstation
kinauza mafuta hayo.
Wakizungumza na Njombe Yetu kwa nyakati tofauti baadhi ya
madereva wa magari na pikipiki mjini Njombe wamesema kuwa adha hiyo imepelekea
baadhi ya magari na pikipiki kuzima njiani yakiwa na abiria kitu ambacho
kimeleta usumbufu kwa abiria.
Kwa upande wao mameneja wa baadhi ya vituo vya mafuta mjini hapa
Prosper Mtewelewa wa kituo cha Ndime Petrol Station na Kaimu Meneja wa kituo
cha mafuta cha Total...
TANESCO NA MWEKEZAJI KUTOKA MAREKANI KUZALISHA UMEME MEGAWATI 400
Na Festus Pangani, Njombe Yetu
Serikali ya Tanzania kupitia shirika la umeme tanesco kwa
kushirikiana na mwekezaji kutoka nchini marekani, inajiandaa kutekeleza mradi
wa umeme wa maji katika mto ruhuji.
Akizungmza wakati wa baraza la madiwani Mpimaji ardhi mwandamizi wa Tanesco makao makuu Hamis Boby
amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwaka 2019 na kuzalisha
umeme wa megawati takribani mia tatu hadi mia nne.
Boby amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa mgodi kufua umeme wa megawati 350 hadi 400, bwawa la kuhifadhi
maji, bwawa la kuzalisha umeme, njia ya umeme, barabara, njia ya kusafirisha
maji chini ya ardhi, ofisI na makazi.
Hata hivyo amesema hatua hiyo itazingatia haki za wananchi
katika eneo husika kwa kulipwa fidia ya ardhi, kupata huduma...
KATIBU MWENEZI WA CHADEMA MAKETE HASOMEKI......

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe
Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi, katibu wa itikadi na uenezi wa CHADEMA wilayani Makete Bw. Sinene amekifagilia chama cha mapinduzi kwa kusema kuwa kimejitahidi katika mambo yake ikiwemo kuwa na wanachama wengi wilayani hapo kwa zaidi ya asilimia 90
Sinene ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha zake alipoalikwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi wa CCM uliofanyika jana kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani hapo
Katibu huyo alisema “nikilinganisha huko nyuma na hii leo kwa kweli chama chenu kimejitahidi kwa zaidi ya asilimia 90, mna wanachama wengi na mnaendelea kufanya mengi”
Awali wakati akianza...
Diwani CCM aliyejeruhiwa sasa ahamishiwa Muhimbili
*Pia wamo Samia na Dk. MwinyiDiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ramadhani, Wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Livingstone Luvanda, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kupingwa na mgombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya hiyo, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulghence Ngonyani, akizungumza na NIPASHE jana alisema diwani huyo amehamishiwa katika hospitali hiyo kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kibena alikokuwa amelazwa awali.
Mgombea huyo ambaye anagombea nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wilaya ya Njombe (jina tunalihifadhi), alimpiga diwani huyo...
Bweni la wanafunzi lawaka moto Njombe
Zaidi ya wanafunzi 93 wa kidato cha tatu na nne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Wanike mkoani Njombe, wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.
Mkuu wa Wilaya ya Wang’ing’ombe, Esterina Kilasi, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 13, mwaka huu saa 4:00 usiku.
Alisema moto huo uliteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi.
Hata hivyo, alisema moto huo hakuleta madhara kwa upande wa wanafunzi na thamani ya vifaa pamoja na chanzo cha moto huo havijafahamika.
CHANZO: NIPA...
MWENYEKITI MPYA WA CCM LUDEWA AAHIDI MAKUBWA KWAVIJANA
Festus Pangani, Njombe Yetu.
Mwenyekiti wa vijana kupitia Chama Cha Mapinduzi wilayani Ludewa Bi.Elizabeth Augustino Haule ameahidi kufanya mambo makubwa kwa vijana baada ya kumchagua kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mine.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Bi. Elizabeth alisema kutokana na yeye kuwa mjasiliamali atatumia fulsa hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wilayani humo kutoa elimu ya kujitambua kwani vijana walio wengi bado hawajitambui.
Alisema kijana anapaswa kijiajiri na si kusubiri kuajiriwa kwa maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa kutofanya kazi na kusubiri mtu au kampuni ianzishe ndipo uajiliwe.
Elizabeth alibainisha kuwa mafanikio yake mpaka alipofikia kuwa mwenyekiti ni juhudi binafsi na si mtu alikuwa nyuma yake kwani katika mikakati yake ilikuwa...
SEKTA YA UTALII NJOMBE IMETELEKEZWA?
Na Festus Pangani, Njombe YetuSekta ya utalii katika mkoa wa Njombe imesahaulika licha ya kuliingizia taifa kipato kutokana na wageni mbalimbali wanaotembelea vituo vya utalii kwa ajili ya kujionea maajabu mbalimbali katika vivutio hivyo.
Mkoa wa Njombe unavivutio vingi vya utalii, ikiwamo hifadhi ya wanyama ya kitulo, shamba la maua yenye kuvutia na kustaajabisha lililopo Uwemba na mwamba wenye ramani ya afrika unaopatikana katika Kijiji cha Igodiva Tarafa ya Imalinyi wilayani Wanging’ombe.
Hata hivyo kutokuwapo kwa juhudi za kutosha katika kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio hivyo kumechangia vivutio vingi vya utalii kutofahamika hata kwa baadhi ya wenyeji wa mkoa wa huo.Akizungumza na Blogzamikoa Afisa Utalii, Maliasili na Mali kale wa Wilaya ya Njombe Abed Henry Chaula alikiri kuwa ...
BWENI LATEKETEA KWA MOTO NJOMBE, WANAFUNZI 93 WANUSURIKA KIFO
Festus Pangani, Njombe YetuWANAFUNZI 93 wamenusurika kufa baada ya bweni lao kutekea kwa moto usiku wa kuamkia leo katika shule ya sekondari ya wasichana ya Wanike iliyopo Kata ya Mdandu wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe.
Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Estelina Kilasi amesema, tukio hilo limetokea septemba 13 saa 4 usiku na kuteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi hao ambavyo thamani yake bado haijajulikana na chanzo cha moto huo hakijafahamika.aa
Bi Kilasi amsema, bweni ambalo limeteketea ni la wasichana wanaosoma kidato cha tatu na cha nne ambao wote walifanikiwa kutoka nje na kuacha mali zao zikiteketea kwa moto.
Amevitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja ni daftari, vitanda, magodoro na nguo za kiraia na sare zao vyote vimeteketea kwa moto huo.
Kutokana na ajali hiyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza...
NJOMBE MEDIA CLUB YAZINDULIWA
Mwandishi wetu, Njombe YetuSeptemba 11, mwaka huu jamii ya Wananjombe ilishuhudia uzinduzi wa jumuiya ya wanahabari Njombe ambayo inajulikana kwa jina la Njombe Media Club itakayokuwa ikiwaunganisha wanahabari na wadau wa habari wa mkoani humo.Lengo la kuanzishwa kwa club hiyo ya kutetea maslahi ya wanahabari Njombe na kuwekana sawa katika kahakikisha tasnia ya habari mkoani hapa inakua na kuchangia katika maendeleo.Pamoja na kwamba mkoa wa Njombe umeanzishwa muda kidogo uliopita, klabu hii ya waandishi imeanzishwa sasa hasa kwa msukumo wa mauaji ya mwandishi wa kituo cha Channel Ten Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa kijiji cha Nyololo wilayani mufindi katika...
UJENZI WA BARABARA ZA MITAA KWA KIWANGO CHA LAMI NJOMBE WAANZA KWA KASI
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
...
NJOMBE KUANZA KUSAMBAZA PEMBEJEO
Festus Pangani, NjombeWakati msimu wa kilimo ukiwa umeanza kwa baadhi ya mikoa hapa nchini, tayari serikali imeanza kusambaza vocha za ruzuku za pembejeo kwa wakulima ili kwenda sanjari na msimu wa kilimo.Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sara Dumba amesema wilaya ya Njombe ni miongoni mwa wilaya ambazo tayari zimepokea vocha hizo huku wakitarajia kuanza kuzisambaza kwa wakulima ambao shughuli za kilimo huanza mapema katika maeneo yao.Akielezea mchakato wa kufikisha vocha za pembejeo kwa wakulima Dumba amesema hatua za kuwafikishia wakulima hao zinafanyika huku akieleza kuwa zoezi hilo kwa mwaka huu linafanywa na serikali kwa kuyatumia makampuni ambayo yatatafuta mawakala watakaofanya kazi ya usambazaji. Aidha mwenyekiti huyo wa...
SAKATA LA KUHAMISHWA MTENDAJI IGWACHANYA, WANANCHI WAMTAKA MTENDAJI WAO
*RC amtetea DC kuhamia MdanduNa Waandishi wetuWananchi wa Kata ya Igwachanya wanamlilia aliyekuwa Mtendaji wa Kata yao kwa maelezo kuwa alikuwa mchapakazi.Taarifa ambazo Kwanza Jamii-Njombe imezipata zinasema Job Fute amehamishwa kutoka katika kata hiyo kimyakimya baada ya kulitaarifu gazeti hili juu ya tetesi zilizopo katika kata hiyo juu ya uamuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe kutokubali nyumba ya mbunge na kuamua kuanzia shughuli zake kata ya Mdandu.Imefahamika baada ya Fute kuondolewa katika wadhifa wake kama mtendaji wa Kata ya Igwachanya, hivi sasa yupo mapokezi katika idara ya utumishi katika ofisi za Halmashauri kama adhabu.Hata hivyo, katika mkutano na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kepteni (Mstaafu), Assery Msangi aliwaeleza wananchi wa Igwachanya kuwa, kitendo cha kuamua kutumia...
WAWILI MBARONI KWA KUKATAA KUHESABIWA MAKAMBAKO
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:"Table Normal";
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
...