Festus Pangani, Njombe
Wakati msimu wa kilimo ukiwa umeanza kwa baadhi ya mikoa hapa nchini, tayari serikali imeanza kusambaza vocha za ruzuku za pembejeo kwa wakulima ili kwenda sanjari na msimu wa kilimo.
Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sara Dumba amesema wilaya ya Njombe ni miongoni mwa wilaya ambazo tayari zimepokea vocha hizo huku wakitarajia kuanza kuzisambaza kwa wakulima ambao shughuli za kilimo huanza mapema katika maeneo yao.
Akielezea mchakato wa kufikisha vocha za pembejeo kwa wakulima Dumba amesema hatua za kuwafikishia wakulima hao zinafanyika huku akieleza kuwa zoezi hilo kwa mwaka huu linafanywa na serikali kwa kuyatumia makampuni ambayo yatatafuta mawakala watakaofanya kazi ya usambazaji.
Aidha mwenyekiti huyo wa kamati ya vocha za pembejeo amesisitiza kuwa pembejeo hizo lazima ziwafikie walengwa na si vinginevyo.
blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment