Festus Pangani, Njombe Yetu
Kwa siku ya tatu sasa mji wa Njombe umekumbwa na adha ya
kukosekana kwa nishati ya mafuta ya petroli kwenye vituo vya mafuta hali
inayopelekea kukwama kwa usafiri na kushuka kwa uchumi miongoni mwa jamii.
Hali hiyo imetokea kuanzia septemba 30 mwezi uliopita hadi
sasa ambapo hadi hii leo ni kituo kimoja tu cha mafuta cha Ndime PetrolSstation
kinauza mafuta hayo.
Wakizungumza na Njombe Yetu kwa nyakati tofauti baadhi ya
madereva wa magari na pikipiki mjini Njombe wamesema kuwa adha hiyo imepelekea
baadhi ya magari na pikipiki kuzima njiani yakiwa na abiria kitu ambacho
kimeleta usumbufu kwa abiria.
Kwa upande wao mameneja wa baadhi ya vituo vya mafuta mjini hapa
Prosper Mtewelewa wa kituo cha Ndime Petrol Station na Kaimu Meneja wa kituo
cha mafuta cha Total wamesema tatizo hilo limetokea sehema ya kusambazia mafuta
kutokana na siku za jumamosi na jumapili kutokuwepo kikazi.
Hata hivyo pamoja na kutokuwepo kwa mafuta mjini Njombe
hakuna ongezeko lolote la bei ya mafuta mkoani hapa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment