Na Festus Pangani, Njombe Yetu
Serikali ya Tanzania kupitia shirika la umeme tanesco kwa
kushirikiana na mwekezaji kutoka nchini marekani, inajiandaa kutekeleza mradi
wa umeme wa maji katika mto ruhuji.
Akizungmza wakati wa baraza la madiwani Mpimaji ardhi mwandamizi wa Tanesco makao makuu Hamis Boby
amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwaka 2019 na kuzalisha
umeme wa megawati takribani mia tatu hadi mia nne.
Boby amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa mgodi kufua umeme wa megawati 350 hadi 400, bwawa la kuhifadhi
maji, bwawa la kuzalisha umeme, njia ya umeme, barabara, njia ya kusafirisha
maji chini ya ardhi, ofisI na makazi.
Hata hivyo amesema hatua hiyo itazingatia haki za wananchi
katika eneo husika kwa kulipwa fidia ya ardhi, kupata huduma za kijamii, elimu
ya mahusiano, pamoja na huduma nyingine zitakazopendekezwa kwenye makubaliano
yao na wadau.
Kwa upande wao madiwani wa halmashauri ya mji wa Njombe na
wilaya ya Njombe wameupongeza mpango huo wa serikali na kuwataka wawekezaji hao
kutoa fidia kwa wananchi watakaohamishwa ili kupisha utekelezaji wa mradi huo
bila ubaguzi wala upendeleo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Venancy Kabelege
amewataka madiwani kushirikiana na serikali katika kuwahamasisha wananchi ili
kufanikisha zoezi hilo la mradi.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment