Home » » UWT TAIFA YASHUSHA NEEMA IKUWO SEKONDARI WILAYANI MAKETE

UWT TAIFA YASHUSHA NEEMA IKUWO SEKONDARI WILAYANI MAKETE

 naibu katibu mkuu UWT taifa Eva Kihwele akizungumza na wanafunzi wa Ikuwo Sekondari
Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania (UWT) umeahidi kutoa solar Panel  moja yenye thamani ya zaidi ya tsh laki nane kwa shule ya sekondari Ikuwo iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu katibu mkuu wa UWT Taifa Eva Kihwele wakati alipofanya ziara katika shule hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alikagua mabweni ya wasichana yaliyopo shuleni hapo

Akisomewa taarifa ya shule hiyo na Mkuu wa shule alisema pamoja na mafanikio lakini wana upungufu wa sola kwa ajili ya kutoa nishati ya umeme ambayo itawasaidia kuongeza ufanisi na utendaji kazi shuleni hapo ikiwemo kujisomea jambo lililoigusa UWT na kuamua kutoa msaada huo

Mbali na kuahidi kutoa sola hiyo, pia kiongozi huyo ametoa shilingi laki moja kwa ajili ya sukari ya wanafunzi hao ambao wanalala shuleni hapo

Akizungumza na wanafunzi hao Naibu Katibu mkuu UWT Taifa Bi Kihwele amewataka kuzingatia masomo kwa kuwa watoto wengi wa kike wamekuwa hawafikii malengo yao, na kuwataka wao kuwa mfano wa kuigwa kwa kusoma kwa bidii hadi wafikie chuo kikuu, ili badae wawe na kazi nzuri itakayowasaidia kuingiza kipato chao cha kila siku

Viongozi wa kitaifa wa UWT wapo wilayani makete kwa siku tatu kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukagua miradi ya maendeleo na kuchukua changamoto mbalimbali za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa