Home » » MFANYABIASHARA NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI LUPYANA FUTE[Jacky's]AMEFARIKI DUNIA GHAFLA

MFANYABIASHARA NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI LUPYANA FUTE[Jacky's]AMEFARIKI DUNIA GHAFLA


Lupyana Fute enzi  za uhai wake akizungumza Kwenye Moja ya Vikao vya Baraza la Madiwani Enzi za Uhai Wake.
...................................................................................................................
Na Mwandishi Wetu.

Diwani wa Kata ya Njombe Mji Lupyana Fute  ambae  pia aliuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC Wilaya ya Njombe amefariki dunia Ghafla Jioni ya jana mjini Njombe .

Taarifa za awali toka kwa Mashuhuda wa tukio hilo Akiwemo Solanus Mhagama Amesema Kuwa Kwa Mara ya Mwisho Marehemu Lupyana Fute alimpigia Simu na Kumwambia amtafutia Gari la Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Chumba cha jengo la Ofisi yake Iliyopo Karibu na Tumaini Dispensari.


Bwana Mhagama Amesema Kuwa Mara Baada ya Kufika Kwa Gari hilo na Kufanikiwa Kuzima Moto Kwa Kushirikiana na Wananchi moto uliokuwa Ukiwaka Kwenye Chumba Cha Kuhifadhia Vitu[STOO] ndipo Marehemu alipoingia Ofisini Kwake alikopotezea fahamu.

Aidha amesema Kuwa Walipoingia Ndani ya Chumba Ofisini Kwake Walimkuta Marehemu Fute akiwa amepoteza fahamu huku akiwa ameketi Kwenye Kiti Chake Ndipo walipomchukua na Kumwahisha Katika Hospitali ya Kibena.Mara Baada ya Kufika Katika Hospitali ya Mji Njombe Kibena Ndiko Waliko ambiwa ameshafariki.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Edwin Mwanzinga amesema ni Kweli diwani huyo amefariki dunia  na  kuwa taarifa zaidi zitaendelea Kutolewa.

Na Francis Godwin

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa