TUKIO KATIKA PICHA: BASI LA KAMPUNI YA JAPANESE LATUMBUKIA MTONI MKOANI NJOMBE


 Basi la Japanese lenye namba za usajili T 261 CMK aina ya YUTONG likiwa limetumbukia mtoni na kusababisha abiria kadhaa waliokuwa wakisafiri na basi hilo kutoka Ikonda wilayani Makete kwenda Makambako mkoani Njombe kujeruhiwa. Hadi tunaondoka eneo la tukio hakuna abiria aliyepoteza maisha na majeruhi wote waliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi. Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa nane mchana.
 Majeruhi wa ajali hiyo akizungumza na mwandishi wetu muda mchache kabla ya kuwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Mmoja wa wafanyakazi wa basi hilo ambaye naye amejeruhiwa kidogo katika ajali hiyo akiwa katika hali ya huzuni. Taarifa na picha zaidi za tukio hilo zitakujia hivi punde endelea kusoma Eddy Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAZIRI NYARANDU AONJA MACHUNGU NCAA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amepokelewa kwa mabango na kundi la wafugaji wa jamii ya Kimasai, wakati alipokwenda kuzindua bodi mpya ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) ambayo wanailalamikia kuwa haina uwakilishi wa kutosha toka kwa jamii hiyo.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu wiki hii wakati Waziri Nyalandu alipokuwa ofisi za makao makuu ya NCAA kwa ajili ya kuzindua bodi aliyoiteua, lakini kabla ya kufanya hivyo, alizuiwa na kundi la wafugaji wanaoishi eneo hilo huku wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe wa maneno tofauti tofauti.

Hali hiyo ilimfanya Waziri Nyalandu kusimama na kuwasikiliza kilio chao.Baadhi ya mabango yalisomeka: “Tunataka uwakilishi wa asilimia tano katika bodi, tunataka maeneo ya ufugaji, haki zangu kama mwenyeji wa hapa haijaheshimika. Wenyeji wa hapa hawajahusishwa katika kusimamia na kuhifadhi Ngorongoro, ahadi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, haijatekelezwa. Hatuhitaji zaidi uwekezaji hoteli katika kingo za creta ya Ngorongoro.”

Ujumbe mwingine ulisomeka: “Tunahitaji kuhusishwa katika ajira, chakula cha lishe bora na sio tu mahindi. Njaa: haki ya kuishi ipo hatarini kwa Wamasai wanaoishi Ngorongoro.”

Akijibu malalamiko ya Wamasai hao, Waziri Nyalandu aliahidi baada ya majuma mawili atateua mtu mmoja maarufu katika jamii ya Wamasai kuwa mjumbe wa bodi hiyo.

“Hii ni sehemu ya kutekeleza matakwa yenu kwa kuzingatia tunataka Wamasai kuwa sehemu muhimu ya kulinda raslimali hii,” alisema.

Hata hivyo alisema bodi ya sasa  ina mjumbe mmoja kutoka Baraza la Wafugaji, taasisi ambayo inawakilisha wafugaji wenyeji wa eneo hilo.

Waziri Nyalandu alikiri kuwapo kwa changamoto nyingi zinazoikabili mamlaka hiyo ikiwemo kuongezeka kwa idadi kubwa ya shughuli za kibinadamu, huku akieleza wakati Mamlaka hiyo ilipoanzishwa mwaka 1959, ilikuwa na idadi ya watu 8,000 lakini miaka  50 baadaye yaani 2009 idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia zaidi ya 66,000 na katika sense maalum iliyofanyika hivi karibuni, imeonyesha kuwa hifadhi hiyo ina jumla ya watu 87,000.

Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA ni Balozi Mwanaidi Maajar, ambaye aliahidi kufanya kazi kwa karibu katika kutekeleza maagizo yanayotolewa na wizara ili kuhakikisha mamlaka hiyo inaendeshwa pasipo vikwazo vyo vyote.
CHANZO: NIPASHE

VIONGOZI NA WATAALAM WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO WAKAGUA MAENDELEO MRADI WA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma kutoka kwa Meneja Utawala Msaidizi wa kampuni ya Tanzania – China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) Bw. Israel Mkojera. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Mlingi E. Mkucha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama wa NDC Bw. Ramson Mwilangali (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (wa pili kushoto), Erasmus Masumbuko, Tume ya Mipango (wa tatu Kushoto).
 Viongozi pamoja na Maofisa kutoka Tume ya Mipango wakiangalia sehemu ambayo makaa ya mawe yanaonekana juu ya ardhi. Kulia ni mhandisi wa madini kutoka kampuni ya TCIMRL. Kampuni hii ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania, na kampuni ya Sichuang Hongda Group Limited ya China. 
 Sehemu ambayo makaa ya mawe yanaoneka kwa juu katika uhalisia wake.
Shimo hili lilichimbwa mwaka 1956 kwa ajili ya utafiti kuangalia tabaka za makaa ya mawe katika eneo hilo la Mchuchuma.

HABARI NJEMA KWA WALE WOTE WALIOKOSA NAFASI KUENDELEA NA MASOMO KIDATO CHA TANO SERIKALINI , SASA MNAWEZA KUOMBA KUSOMESHWA SOMA HAPA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA NJOMBE WAKABIDHIWA VYETI VYA USHIRIKI WA MAFUNZO YALIYOTOLEWA NA MCT‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe Hamis Kassapa akipokea cheti cha kushiriki mafunzo yaliyotolewa na baraza la habari Tanzania MCT kwa waandishi wa habari wa mkoa huo jana Juni 19, 2014
Mtangazaji wa Uplands Fm Zenobia Mtei akipokea cheti chake kutoka kwa wawakilishi wa MCT
David Jothamson kutoka Kings FM ya Njombe akipokea cheti chake cha kushiriki mafunzo
Mtangazaji Veronica Mtauka wa redio Kitulo FM ya wilayani Makete mkoani Njombe akipokea kwa furaha cheti chake kama mshiriki wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Ice FM ya Makambako mkoani Njombe MCDonald Mase akipokea cheti chake
 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe Mercy James akikabidhiwa cheti chake
 Meneja wa kitucha redio Uplands Fm, Novatus Lyaruu akipokea cheti chake kama mshiriki wa mafunzo hayo
Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira na mtandao wa Habari Ludewa Blog NIckson Mahundi akikabidhiwa cheti chake
Mtangazaji wa Best FM ya Ludewa mkoani Njombe akipewa cheti chake cha ushiriki wa mafunzo hayo
Mmiliki wa Eddy Blog Edwin Moshi akipokea cheti cha mafunzo hayo ya siku nne yaliyoandaliwa na MCT.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na baraza la habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (NPC) yenye lengo la kuwasaidia waandishi hao kuandika habari kwa kufuata weledi wa taaluma hiyoPICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI
 

MKUU WA WILAYA YA MAKETE ATOA RAI KWA JAMII YA MAKETE KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mkuu wa wilaya ya Makete mwenye suti nyeusi (aliyesuka nywele) Mh. Josephine Matiro, mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (kulia kwa mkuu wa wilaya) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto walioshiriki maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro(wa tatu kushoto walioketi) na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (wa pili walioketi kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa shirika la wasaidizi wa kisheria Makete
 Katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari ya Iwawa Makete ambao nao walishiriki
 Wanafunzi wa shule ya msingi Ndulamo wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha/habari na Edwin Moshi na Conrad Mpila, Makete.)
Imeelezwa kuwa ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali peke yao kufanya kazi hiyo
 
Kauli hiyo imetolewa leo hii Juni 16 na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa (kwa asasi zisizo za kiserikali) katika viwanja vya mabehewani kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe

Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto walio wengi Wilayani Makete ambao ni Yatima na waishio katika mazingira magumu ambao wanahitaji msaada wa kila mmoja

"Ni kweli wilaya ya Makete ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo wilayani mwetu, hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kila mtu kwa kadri ya uwezo wake, mwenye sabuni, kalamu, fedha ama chochote anaweza kufanya hivyo kwa wakati wake" amesema Matiro

Katika risala iliyosomwa na mwanafunzi Gaudencia Malangalila wa Shule ya msingi Ndulamo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema Kuwa watoto walio wengi wanakabiliwa na unyanyasaji kwa kufanyishwa Kazi ngumu na hatarishi,kutopata haki katika huduma za matibabu,walezi kunyang'anya misaada wanayopewa na wadau mbalimbali

Naye Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Helen Kijo Bisimba amesema Kuwa kwa Tafiti alizofanya amebaini Kuwa kuna watoto ambao waliondoka kwenda nje ya Makete kwa kufanya Kazi na hawarudi tena huku wazazi hawajui Kama wapo hai au la,kwani hata mawasiliano na wazazi ama walezi wao bado ni magumu

Hivyo amewasihi wazazi/walezi Kuwa makini na watoto wao pindi wanapoitwa kwenda kufanya Kazi maeneo ya mbali kwani mara nyingi huko wanakokwenda wanakutana na mambo ambayo ni kinyume na walioyatarajia

Katika maadhimisho hayo kikundi cha wazazi kutoka Kijiji cha Isapulano na Ndulamo Maarufu Kama mama mkubwa wamesema Kuwa vikundi hivyo vitaendelea Kulinda haki za watoto na kutoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya sanaa  na kufanya uchunguzi dhidi ya watoto wanaofanyiwa unyanyasaji na watatoa taarifa katika ngazi husika na wakigundulikaa wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
 
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo"

CWT,TGNP,WATAKA BAJETI KUZINGATIA MAENEO MUHIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba
Chama cha Walimu  nchini (CWT) kimesema wananchi wanahitaji bajeti itakayowapatia mahitaji muhimu kama elimu, afya, maji na ulinzi.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba (pichani) , alisema bajeti ya elimu inatakiwa kuwa asilimia sita ya pato la taifa, lakini hadi sasa bajeti inayotengwa na serikali ni asilimia moja.

Mukoba alisema bajeti nzuri ni ile ambayo inampatia mwananchi mahitaji ya vitu muhimu ambavyo wananchi wanatarajia kuvipata.

“Vitu kama elimu, afya, maji na ulinzi ni muhimu, watu wanahitaji, afya bora ili waweze kufanya kazi na kupata kipato, ulinzi ni muhimu kwani kuna makundi yameibuka kama ‘Panya wa Rwanda’ na ‘Mbwa mwitu’ ambayo yanahatarisha usalama wa wananchi, hivyo wananchi wanahitaji kusikia ulinzi unaimarishwa,” alisema Mukoba.

Alisema ili taifa hili liweze kuendelea na kukuza uchumi wake ni vyema serikali ikazingatia vipaumbele hivyo ili kuendelea  kuinua uchumi wa wananchi wake.

Nao Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umesema   kama bajeti itakayosomwa leo haitazingatia  na kuweka vipaumbele muhimu kama afya na maji bado haitamsaidia mwananchi wa kawaida.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, alisema katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Wizara ya Afya haijahusishwa, suala ambalo ni hatari kwani jamii inahitaji kuwa na afya bora ili kufanya shughuli za maendeleo.

“Bajeti ya serikali bado haijaweza kumnufaisha mwananchi wa kawaida kama vile ambavyo wananchi wanatarajia, mfano masuala muhimu kama afya na maji ni miongozi mwa mambo ambayo bado yanawaumiza wanawake na vijana walioko pembezoni,” alisema Liundi.

Alisema kipaumbele cha sekta binafsi ambayo serikali imeboresha na kukuza uchumi wa nchi bado hakijaweza kumnufaisha mwananchi wa kawaida.

Alifafanua kuwa ukuaji wa uchumi bado haujawafikia au kuwanufaisha wananchi ambao wako pembezoni hasa wanawake na watoto.

Alisema kwa upande wa sekta ya usafirishaji bado pia haijaweza kuwanufaisha wananchi wa kawaida ambao ni wakulima wa mazao mbalimbali ambao wanatarajia kutumia barabara ili kusafirisha mazao yao.

CHANZO: NIPASHE

MKUU WA WILAYA YA MAKETE AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MADEREVA BODABODA NA WAJASIRIAMALI MAKETE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati akifunga mafunzo kwa madereva bodaboda wilayani Makete. Mafunzo hayo yametolewa na shirika la APEC
 Madereva bodaboda wakifurahia kupatiwa vyeti vya mafunzo hayo.
 Bi Rehebian Mahenge ambaye alikuwa katibu katika mafunzo hayo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
 Bi Mahenge akimkabidhi risala mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo
Mkuu wa polisi wilaya ya Makete Alfred Kasonde akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo hayo
 Mkuu wa wilaya akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi wa APEC Bw. RespiciusTimanywa akitoa maelezo ya awali jinsi walivyoendesha mafunzo hayo na matarajio wanayoyategemea kutoka kwa wahitimu hao

 Miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo ambaye pia ni askari polisi wilayaani Makete Afande Moses akipokea cheti chake
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro akiteta jambo na Mkurugenzi wa APEC Bw. Respicius Timanywa mara baada ya kumaliza kufunga rasmi mafunzo hayo
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Makete wakiwa kwenye picha ya pamoja
 wawezeshaji wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalam wilaya ya Makete

WASHANGAZWA NA USHINDI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE USAFI WA MAZINGIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na James Festo, Njombe.

KATIKA kuelekea siku ya maadhisho ya mazingira  ambayo hufanyika june tano ya kila mwaka  huku Halmashauri ya mji wa Njombe ikiwa inaendelea kushika nafasi za juu kwa usafi   wananchi wake wameendelea kuitupia lawama za kushindwa kuzoa takataka  kwenye vizimba hali ambayo inaweza kusababisha  magonjwa ya mlipuko.

Hali hiyo inakuja kufuatia kusuasua kwa uzoaji taka  katika vizimba vya takataka vikiwemo vilivyopo karibu na maeneo yanayotumika katika uuzaji wa vyakula  kitu ambacho kinaweza kusabisha madhara makubwa kwa wauzaji pamoja na wateja wao

Mwandishi wa habari hii alitembelea na kujionea  vituo mbalimbali Ndani ya halmashauri ya Mji wa Njombe  hali mbaya ya takataka zilizofurika  nje ya vizimba  licha ya wananchi kuendelea na biashara  likiwemo eneo nyuma ya kituo cha mabasi mjini njombe.

Wakizungumza na majira baadhi ya wafanyabiashara hao walisema kuwa tangu kusimama  kwa mawakala waliokuwa wakifanya kazi hiyo ya kuzoa takataka kwenye vizimba na Halmashuri kuvaa jukumu hilo  mwenendo umekuwa wa kusuasua na kueleza kushangazwa  kuona wakilipa ushuru kila uchao wakati taka hazizolewi kwa wakati.

 "   sasa hivi michango imesitishwa  ndio maana ya kwenye vizimba taka ni nyingi.... labda kila mwananchi awe anachangia  kila kaya ...tunataka tuchangie..... tukisema tufanye hivi hatufiki ...... wakala ameshindwa kufanya kazi kwa sababu  kipato anachopata halmashauri  ni kidogo "   walisema wafanyabiashara hao.

Aidha Wafanyabiashara  hao waliiomba halmashuri kutumia  fedha zinazokusanywa katika ushuru wa soko kutumika katika kufanya usafi wa soko hilo na kuwasisitiza watumishi wa sekta hiyo kuacha uzembe wa kukaa ofisini.

Andove Mgani ni mwenyekiti wa  soko la  wafanyabishara lililopo nyuma ya kituo cha mabasi cha Njombe alisema kuwa tangu Halmashuri ya Mji ianze kusimamia yenyewe  zoezi ya utoaji wa taka hizo imekuwa ikizidiwa na kusababisha  taka kukaa zaidi ya wiki  kitu ambacho ni hatari kwa wananchi  mjini hapa.

"  ninachojua zamani taka taka na yule wakala alikuwa makini na kazi yake lakini baada ya kusimamiwa na halmashauri  vizimba vya hapa mjini vyote vinakaa na takataka muda wote  kama wafanyabiashara tungekuwa na uwezo wa kuamua  tungemuaomba arudi afanye kazi ya kuzoa takataka"   alisema Bw Ndonya.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Venance Msungu alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la uzoaji wa takataka  alisimama kutokana kiasi cha fedha aliyokuwa akilipwa huku mji wa Njombe ukiendeea kuongezeka kwa uchafu.

Alisema kuwa katika kipindi cha miezi miwili baada ya wakala huyo Halmashauri hiyo imekuwa ikiendelea na zoezi hilo  huku wakisubiri mwezi julai mwaka huu wa kutangazwa kwa mzabuni ambaye ataanza kufanya kazi hiyo ambaye atakuwa na vifaa vya kutosha tofauti na Halmashauri  ambayo imekuwa ikitumia magari mawili pekee.

"  hata waandishi wa habari inayostahili watu wanaongea kwamba uchafu bado tatizo jambo linaonyesha kukosa uelewa wa kulinganisha na sehemu zingine  hapa nchini....zabuni zitafunguliwa mwezi huu  wa sita  na inapoanza mwezi julai  tutakuwa na mzabini mwenye vifaa vya kutosha vya kutolea uchafu"   alisema bw Msungu.

HABARI PICHA ZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA NJOMBE MZEE ADAM MSIGWA


 Deo Sanga ambaye ni Mbunge na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe.


Aliyekuwa  mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe, Adam Ismail Msigwa (pichani) ambaye alijukana kwa jina maarufu kama 'Shilingi ni Vita' amefariki  nyumbani katika Mitaa wa Kwivaha Njombe mjini na mazishi yalifanyika katika kijiji cha lisitu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Cept. mstaafu Aseri Msangi (kushoto ) wa pili ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw Saitabau na wa mwisho (kulia) ni Kamanda wa polisi mkoa  SACP  Ngonyani.
"MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI"
 'AMINA'
PICHA ZOTE NA JAMES FESTO & PROSPER MFUGALE.

WAAJIRI WATAKIWA KULINDA AFYA ZA WAFANYAKAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

SERIKALI imewataka waajiri wote kuhakikisha wanaanzisha mifumo bora mahali pa kazi itakayohakikisha wafanyakazi wao wana usalama na wenye afya bora.
Alisema suala hilo si jambo la hiari kwani linagusa uhai na maisha ya watu.Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi Duniani, Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliwataka waajiri wasikwepe wala kuogopa gharama katika hilo.
"Zingatieni kuwa hakuna kitu chenye thamani kuzidi uhai na maisha ya watu," alisema.
Alisema takwimu za Shirika la Afya Duniani (ILO) zinaonesha kuwa Kila mwaka duniani takriban watu milioni 337 hupata ajali kazini na kati yao wafanyakazi milioni 2.3 hufariki kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi wanazofanya.
"Takwimu zinatuonesha kuwa watu wanaofariki kutokana na magonjwa ya ajali kazini ni wengi kuliko wale wanaofariki vitani, ni wazi kuwa ajali nyingi na magonjwa kazini hutokana na wafanyakazi kutozingatia kanuni za usalama na afya kazini na waajiri kutochukua hatua za kupunguza ajali na magonjwa hayo," alisema Dkt. Bilal.
Alisema kila mfanyakazi anastahili kufanya kazi yenye ujira wa kutosha kukidhi mahitaji ya msingi katika mazingira salama bila kuhatarisha afya yake, kinyume na hapo kazi hiyo haitakuwa ya staha na haipaswi kufanywa na binadamu yeyote, inayostahili kupigwa marufuku.
Hata hivyo, alisema siku ya usalama na afya mahali pa kazi duniani ni siku muhimu kimataifa ambapo nchi zote wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) tangu mwaka 2001 zilitakiwa kuadhimisha siku hiyo.
Pia alisema maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kubainisha njia mbalimbali za kuzuia magonjwa na ajali zinazotokea kazini na kuimarisha kampeni za kuboresha usalama afya na ustawi wa wafanyakazi wakiwa kazini.
Alisema Serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha inadhibiti matumizi yasiyofaa ya kemikali sehemu za kazi na maeneo mengine kwa manufaa ya afya na wananchi wake.
"Pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali madhara ya kemikali yameendelea kuathiri jamii yetu kwa njia moja au nyingine na haya yanachangiwa na tabia za baadhi ya watu wasio waungwana miongoni mwa jamii," alisema Dkt. Bilal. Alisema Serikali itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi mabaya ya kemikali kwa kutoa elimu kwa watumiaji na wananchi kuhusu matumizi sahihi na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya kemikali.

Chanzo;Majira

Wezi waiba miundombinu ya soko la Ngiu Makete

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, wezi wasiofahamika wameiba baadhi ya miundombinu ya soko la Ngiu wilayani Makete mkoani Njombe licha ya soko hilo kuwa na mlinzi.

Mwandishi wa blog hii ambaye amefika eneo la tukio mara baada ya kupenyezewa taarifa hizi na wananchi, ameshuhudia baadhi ya miundombinu haipo ikiwemo mifuniko yote ya chuma inayofunikia masinki ya vyoo, pamoja na mabomba ya kutiririshia maji ya mvua

Taarifa kamili na picha zote za tukio hilo zitakujia baadaye kidogo.
 Muonekano wa soko la Ngiu lililopo kata ya Iwawa, Makete mjini.
 Chemba ya choo cha soko hilo ikionekana baada ya wezi kuiba mifuniko yote mitatu ya kufunikia chemba hiyo
Na Edwin Moshi

MAONI:RIPOTI YA CAG HAITOI MATUMAINI YOYOTE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha wa 2012/13 imefichua madudu ya ajabu, ambayo bila shaka yatakuwa yameondoa matumaini ya wananchi ya kukua kwa uchumi na kuwaondolea umaskini uliokithiri. Ripoti za CAG za miaka ya fedha iliyopita zilikuwa pia zinafichua madudu ya kutisha, lakini baada ya Serikali kuahidi kwamba ingeepuka kurudia madudu hayo na kuzifanyia kazi changamoto nyingi zilizokuwa zikiibuliwa na ripoti mbalimbali za CAG, wananchi wengi walipata matumaini.
Inasikitisha kwamba ripoti hiyo iliyotolewa ufafanuzi na CAG mwenyewe, Ludovick Utouh juzi, imeonyesha dhahiri  kwamba Serikali haijawa na dhamira ya kweli ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kupambana na vitendo vya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Pamoja na kuwapo kwa Bunge na mifumo mingine kadhaa ya kuhakikisha kwamba Serikali inakuwa na nidhamu katika kusimamia mapato na kudhibiti matumizi yake, bado hakuna mabadiliko wala dalili za uwajibikaji katika matumizi ya fedha za Serikali.
Ripoti ya CAG inaonyesha kwamba matumizi hayo mabaya yanaendelea pamoja na hali mbaya ya uchumi inayolikabili taifa. Kwa mwenendo huo, inaonekana hakuna uwezekano wa kupunguza Deni la Taifa ambalo lilifikia Sh21.20 trilioni, ambalo ni ongezeko la Sh4.23 trilioni sawa na asilimia 25, ikilinganishwa na Sh16.98 trilioni katika mwaka wa fedha wa 2011/12. Ndani ya Serikali umekuwamo utamaduni wa ufujaji wa fedha tunaoweza kusema ni wa mashindano, ambao umechangia kupanda kwa deni la ndani kutoka Sh4.55 trilioni mwaka 2011/2012 hadi Sh5.78 mwaka wa 2012/13, likiwa ni ongezeko la Sh1.23 trilioni, sawa na asilimia 27.
Mwenendo huo ni hatari kwa uchumi na maendeleo ya taifa letu. Baya zaidi ni pale Serikali inapoendekeza mikopo kutoka katika benki za biashara nje ya nchi. Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inasema kwamba Serikali imekuwa ikikopa wastani wa Sh360 bilioni kwa mwezi kutoka nje. Kutokana na hali hiyo,  Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki  ya Dunia (WB), vimeonya dhidi ya mwenendo huo kwamba utahatarisha uchumi, ingawa Ripoti ya CAG inasema mikopo hiyo imesaidia miradi mikubwa ya maendeleo kama uboreshaji wa miundombinu na kadhalika.
Sisi hatudhani kama mikopo hiyo ina madhara kwa uchumi iwapo utakuwapo uwazi na itasimamiwa kwa uadilifu, kwa maana ya kuhakikisha kwamba siyo tu unakuwapo usimamizi katika  matumizi ya fedha hizo, bali pia zinatumika kuendesha miradi iliyokusudiwa. Miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikikwama kutokana na fedha zake kuingizwa katika michepuko isiyofaa, mbali na wizi na ubadhirifu wa baadhi ya wanasiasa, watendaji wa Serikali na taasisi zake.
Ripoti ya CAG imebaini ufisadi mkubwa katika maeneo mengi ya mapato na matumizi ya fedha za Serikali. Kwa mfano, magari mapya 11 yenye thamani ya mamilioni ya shilingi yalinunuliwa lakini yaliishia katika miliki za watu binafsi. Sh1.62 zililipwa kama mishahara kwa watumishi hewa, huku misamaha ya kodi ikilipotezea taifa Sh1.52 trilioni ambazo zingeweza kujenga shule za sekondari za kisasa zaidi ya 300. Ripoti ya CAG haitoi matumaini. Serikali isipopambana na ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, maendeleo na ustawi wa jamii nchini utabaki kuwa ndoto za mchana.
Chanzo:Mwananchi

VETA MAKETE WATEMBELEA WATOTO YATIMA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Wafanyakazi wa VETA Makete wakiwa katika picha na watoto yatima wa kituo cha Bulongwa.
 Mfanyakazi wa VETA Makete akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituoni hapo
 Sanga akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa katika kituo cha Bulongwa
 Wakifurahia pamoja na watoto hao kwa kuimba nyombo.
 Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya kituo hicho.
 Methew Komba akiwa amembeba mtoto yatima
 watoto wakifurahia kutembelewa na wafanyakazi wa VETA Makete.
 Hapa mmoja wa wafanyakazi wa VETA Makete akicheza na watoto hao.
---------
Kufuatia wilaya ya Makete mkoani Njombe kuwa miongoni mwa wilaya zenye watoto yatima, wafanyakazi wa chuo cha VETA Makete wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Bulongwa kilichopo wilayani hapa na kutoa misaada mbalimbali

Akizungumza na mwandishi wetu kwa niaba ya wafanyakazi wenzake alioambatana nao Bw. Mathew Komba amesema wao kama VETA Makete wameguswa na namna watoto hao wanavyopata tabu kwani hawakupenda kuishi maisha hayo lakini kutokana na kufiwa na wazazi wao ndiyo maana wapo katika kituo hicho

Amesema awali walikuwa wamepanga kuwatembelea watoto hao kabla ya pasaka lakini kutokana na sababu zisizoepukika walishindwa kufanya hivyo lakini walijipanga kama walivyokuwa wamedhamiria na jana walifika kituoni hapo kuwaona watoto hao na kuwapa msaada huo

Bw. Komba amesema baadhi ya vitu walivyovikabidhi ni pamoja na mafuta ya kupikia, sukari, mchele, sabuni, juisi, dawa za meno na vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya tsh. 329,000/=

Amewaomba wadau wengine kuwaunga mkono kwa kwenda kuwasaidia watoto yatima kwani ni jukumu la jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawatunza watoto hao licha ya kwamba wanalelewa kwenye vituo mbalimbali

Kwa upande wake Bi Sekela Nkyami kutoka kituo hicho cha kulelea watoto yatima Bulongwa amesema ingawa kituo hicho kina vitega uchumi mbalimbali lakini bado kinategemea misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali wakiwemo wakazi wa Makete wenye moyo wa huruma kama walioufanya chuo cha VETA

Amesema watoto hao waliopo katika kituo hicho si mali ya kituo pekee bali ni wa jamii yote kwa hiyo kuiomba jamii kushirikiana nao katika matunzo ili watoto hao wasijisikie wapweke kutokana na uyatima walio nao

"Ni kweli uyatima unatesa, ila tunawaomba wananchi waje kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hawa, kumekuwa na kasumba kuwa wakishaletwa hapa basi si wao tena bali ni wa kituo, hii sia sawa bali tunatakiwa tushirikiane kwa pamoja chochote kidogo utakachokipata kinatosha kutusaidia" amesema Bi. Nkyami

Na Edwin Moshi, Makete

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa