Na James Festo, Njombe.
KATIKA
kuelekea siku ya maadhisho ya mazingira ambayo hufanyika june tano ya
kila mwaka huku Halmashauri ya mji wa Njombe ikiwa inaendelea kushika
nafasi za juu kwa usafi wananchi wake wameendelea kuitupia lawama za
kushindwa kuzoa takataka kwenye vizimba hali ambayo inaweza
kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Hali
hiyo inakuja kufuatia kusuasua kwa uzoaji taka katika vizimba vya
takataka vikiwemo vilivyopo karibu na maeneo yanayotumika katika uuzaji
wa vyakula kitu ambacho kinaweza kusabisha madhara makubwa kwa wauzaji
pamoja na wateja wao
Mwandishi
wa habari hii alitembelea na kujionea vituo mbalimbali Ndani ya
halmashauri ya Mji wa Njombe hali mbaya ya takataka zilizofurika nje
ya vizimba licha ya wananchi kuendelea na biashara likiwemo eneo nyuma
ya kituo cha mabasi mjini njombe.
Wakizungumza
na majira baadhi ya wafanyabiashara hao walisema kuwa tangu kusimama
kwa mawakala waliokuwa wakifanya kazi hiyo ya kuzoa takataka kwenye
vizimba na Halmashuri kuvaa jukumu hilo mwenendo umekuwa wa kusuasua na
kueleza kushangazwa kuona wakilipa ushuru kila uchao wakati taka
hazizolewi kwa wakati.
"
sasa hivi michango imesitishwa ndio maana ya kwenye vizimba taka ni
nyingi.... labda kila mwananchi awe anachangia kila kaya ...tunataka
tuchangie..... tukisema tufanye hivi hatufiki ...... wakala ameshindwa
kufanya kazi kwa sababu kipato anachopata halmashauri ni kidogo "
walisema wafanyabiashara hao.
Aidha
Wafanyabiashara hao waliiomba halmashuri kutumia fedha zinazokusanywa
katika ushuru wa soko kutumika katika kufanya usafi wa soko hilo na
kuwasisitiza watumishi wa sekta hiyo kuacha uzembe wa kukaa ofisini.
Andove
Mgani ni mwenyekiti wa soko la wafanyabishara lililopo nyuma ya kituo
cha mabasi cha Njombe alisema kuwa tangu Halmashuri ya Mji ianze
kusimamia yenyewe zoezi ya utoaji wa taka hizo imekuwa ikizidiwa na
kusababisha taka kukaa zaidi ya wiki kitu ambacho ni hatari kwa
wananchi mjini hapa.
"
ninachojua zamani taka taka na yule wakala alikuwa makini na kazi yake
lakini baada ya kusimamiwa na halmashauri vizimba vya hapa mjini vyote
vinakaa na takataka muda wote kama wafanyabiashara tungekuwa na uwezo
wa kuamua tungemuaomba arudi afanye kazi ya kuzoa takataka" alisema
Bw Ndonya.
Kwa
upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Venance
Msungu alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la uzoaji wa takataka alisimama
kutokana kiasi cha fedha aliyokuwa akilipwa huku mji wa Njombe ukiendeea
kuongezeka kwa uchafu.
Alisema
kuwa katika kipindi cha miezi miwili baada ya wakala huyo Halmashauri
hiyo imekuwa ikiendelea na zoezi hilo huku wakisubiri mwezi julai mwaka
huu wa kutangazwa kwa mzabuni ambaye ataanza kufanya kazi hiyo ambaye
atakuwa na vifaa vya kutosha tofauti na Halmashauri ambayo imekuwa
ikitumia magari mawili pekee.
"
hata waandishi wa habari inayostahili watu wanaongea kwamba uchafu bado
tatizo jambo linaonyesha kukosa uelewa wa kulinganisha na sehemu
zingine hapa nchini....zabuni zitafunguliwa mwezi huu wa sita na
inapoanza mwezi julai tutakuwa na mzabini mwenye vifaa vya kutosha vya
kutolea uchafu" alisema bw Msungu.
0 comments:
Post a Comment