Waziri
wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge
amewataka wananchi kupuuza taarifa zozote zinazotolewa kwa jina lake
kupitia mtandao wa facebook kwa kuwa yeye hatumii mtandao huo.
Waziri
Mahenge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe ametoa
kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wetu wilayani hapo na kusema
kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mitandao hiyo vibaya kwa kufungua
akaunti yenye jina lake ilihali yeye hajawahi kujiunga na facebook na
hana mpango huo.
Amesema
kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali wapo watu wanaoziamini
taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia mtandao huo wakidhani zimetolewa
na yeye lakini imekuwa tofauti na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa
hizo kwa kuwa zinatolewa na mtu ama watu fulani na si yeye.
"Ukiangalia
pale pana picha yangu kweli, lakini taarifa zingine ni uongo mtupu, kwa
mfano tarehe yangu ya kuzaliwa iliyoandikwa hapo sia ya kweli, hii
inaashiria wanavyoviweka ni vya uongo" amesema Waziri Mahenge.
Aidha
ametoa rai watu kuitumia vizuri mitandao hiyo kwa kuisaidia jamii huku
akiwataka waliofungua akaunti hiyo kuifunga na kuacha kuwapotosha watu
kwa kutumia jina lake kwani ni kinyume cha sheria na atakayebainika
sheria iko wazi dhidi yake.
Hivi
karibuni kumekuwa na watu fulani kufungua akaunti kwnye mitandao ya
kijamii kwa kutumia majina ya viongozi mbalimbali kwa lengo la kuwahadaa
watu na kuwapa taarigfa ambazo si sahihi
Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete
0 comments:
Post a Comment