Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza wakati akifungua
warsha kwa wataalamu wa kilimo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya
Makete hii leo.
Mwezeshaji kutoka shirika ka TAHA Bw. Isaac Ndamanhyilu akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wataalamu wa kilimo wa kata na vijiji vya wilaya ya Makete.
Wataalamu wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwezeshaji Manfred Bitala akiwawezesha washiriki wa warsha hiyo.
Na Edwin Moshi
Halmashauri
ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imedhamiria kuinua kilimo cha matofaa
maarufu kama apples, ili kiweze kuinua uchumi wa wakulima pamoja na
wilaya kwa ujumla
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa mabwana na mabibi shamba
wa kata na vijiji, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro
amesema wilaya imeanza kutekeleza agizo la rais Jakaya Kikwete
alipofanya ziara wilayani hapo kuwa ni lazima kilimo cha apple kiwe cha
biashara wilayani Makete
Mh.
Matiro amesema mafunzo watakayopatiwa maafisa hao wa kilimo, wanatakiwa
kuyafuata na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kata na vijiji vyao
ili mabadiliko yaanze kuonekana na ndiyo maana halmashauri imeshirikiana
na shirika la TAHA kuwapatia mafunzo ya namna ya kuboresha kilimo hicho
katika maeneo wanayotoka
Amesema
kwa kuwa jambo hili halihitaji masihara anatarajia kuona mabadiliko mara
moja pindi mafunzo hayo yatakapo malizika kwa kwenda kuwaelekeza
wakulima kitu cha kufanya ili apples zizalishwe kwa wingi na kwa ubora
unaohitajika kwani hilo linawezekana kwa mujibu wa utafiti ambao
umefanyika wilayani hapo
Mh.
Matiro amesisitiza pia badala ya wananchi kupanda miti mingi ya mbao kwa
sasa wanatakiwa wabadilike na wapande miti ya matunda hasa apples kwa
kufuata elimu ya wataalamu hao wa kilimo ambayo wamepatiwa katika
mafunzo hayo
Kwa
upande wake Bw. Isaac Ndamanhyilu kutoka shirika la Tanzania
Hoticultural Association maarufu kama TAHA ambao ni watoaji wa mafunzo
hayo, amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuongeza uzalishaji wa
apples pamoja na uuzaji wa matunda hayo
Amesema
kwa wilaya ya Makete imekuwa ikizalisha matunda hayo kwa wingi lakini
hakuna kumbukumbu zinazoonesha kama uzalishaji huo upo Makete, na pia
hakuna taarifa zinazoonesha kama wilaya hii ni miongoni mwa maeneo ndani
ya Tanzania yanayozalisha apples
Bw.
Ndamanhyilu amesema kufuatia kukosekana kwa kumbukumbu hizo, ndiyo maana
wameamua kushirikiana na halmashauri kuhakikisha elimu inatolewa kwa
mabwana shamba na mabibi shamba na wao wawaongoze wakulima kulima kilimo
cha kisasa ili matunda hayo yazalishwe kwa wingi na yenye ubora
unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa
"Kulikuwa
kuna maonesho fulani jijini Arusha, na mgeni rasmi alikuwa Rais Kikwete
na alibahatika kuona apples pale, na alipoambiwa kuwa zinazalishwa
Makete kwa kweli alishangaa, na ndiyo maana alisema atafika Makete
kujionea, na kweli alifika na amesisitiza kilimo hiki kiwe cha biashara
na ndio maana tunatoa hii elimu kwenu" alisema
Naye
mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amewaasa mabwana na mabibi
shamba hao kubadilika kwani wapo baadhi ya wataalamu hao wamekuwa
wakihubiri elimu bila kufanya kwa vitendo jambo linalowakatisha tamaa
wakulima
"Yaani
wakati mwingine ukiliangalia shamba la mabwana na mabibi shamba nia
aibu, yaani unakuta shamba la mkulima linaubora kuliko la ninyi
wataalam, sasa hii inakatisha tamaa, lazima ninyi muwe mfano wa kuigwa"
alisema Bitala
Amesema
wao wananafasi kubwa ya kuibadilisha hii nchi kutoka hapa ilipo na
kuonekana mabadiliko makubwa na yenye tija katika sekta ya kilimo kama
kila mmoja ataamua kufanya kazi yake ipasavyo
Katika
mafunzo hayo wamefundishwa mambo mengi ikiwemo dalili na aina za
magonjwa yanayoshambulia matunda, na namna ya kulima na kupata mazao
mazuri zaidi ya ilivyo sasa
0 comments:
Post a Comment