Hii
ndiyo hali halisi, baada ya mvua kunyesha hii leo mkoani Njombe, kituo
hicho kimegeuka matope matupu, na kusababisha watumiaji wa kituo hicho
kupata tabu ya kutembea kwa shida na kutafuta eneo la kukanyaga ili
wapite
Kamera
yetu imeshuhudia abiria wakikanyaga matope na madimbwi ya maji machafu
yaliyoshamiri kituoni hapo huku pia wakirushiwa maji machafu na magari
kituoni humo
Hali halisi ndiyo hii.
Abiria ambaye jina lake halijajulikana mara moja akipita kwenye matope yaliyosheheni kwenye kituo hicha cha mabasi Njombe.
Ni mwendo wa kuchagua eneo la kukanyaga, wengine wanapandisha suruali zao juu zisipate matope.
Huwenda upande huu unaafadhali kwa abiria hawa lakini wapi, tope tuu.
Tope lenyewe.
Licha
ya tabu hii inayowakumba watumiaji wa kituo hiki cha mabasi Njombe,
ushuru umekuwa ukikusanywa kama kawaida, lakini miezi michache iliyopita
halmashauri ya Njombe ilitangaza kuwa haina mpango wa kukikarabati
kituo hicho na badala yake imetenga eneo lingine kwa ajili ya kujenga
kituo kipya cha mabasi.
Eddy
Blog inaamini kuwa hii adha itaendelea kuwakumba wananchi na watumiaji
wa kituo hiki kwa pamoja hivyo kwa kauli ya halmashauri inabidi abiria
hao wazidi kuwa wapole na kuvumilia hali hii mpaka kijengwe kituo kipya!
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment