Home » » UAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MUME MWENZIE, KISA WIVU WA KIMAPENZI

UAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MUME MWENZIE, KISA WIVU WA KIMAPENZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkazi wa kijiji cha Mago kata ya Lupalilo wilayani Makete mkoa wa Njombe Bw. Frenk Sanga (35) ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto ambao ndipo moyo ulipo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 17 mwaka huu majira ya saa 7 usiku, ambapo mtuhumiwa aitwaye Yohana Sanga alimchoma kisu kifuani baada ya kumfumania akiwa na mpenzi wake(hawara) aliyetambulika kwa jina la Matilda Sanga ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho cha Mago

Imeelezwa kuwa siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bi. Matilda, waliongozana usiku hadi nyumbani kwa mwanamke huyo kwa ajili ya kulala pamoja, na ndipo mtuhumiwa ambaye ni Yohana, ambaye inadaiwa alikuwa akifuatilia nyendo zao aliwavamia nyumbani kwa mwanamke huyo na kumchoma kisu kifuani marehemu hadi akapoteza maisha

Baada ya mtuhumiwa kutenda mauaji hayo katika nyumba ya huyo hawara yake alichomoa kisu hicho na kumshikisha marehemu mkononi, kwa lengo la kupoteza ushaidi ili ionekane kuwa alijiua mwenyewe

Akizungumzia tukio hilo Afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Makete ambaye pia ni Kaimu OCD wilaya ya Makete, Mrakibu wa polisi Gosbert Komba amesema wao kama jeshi la polisi walipewa taarifa na Bw. Emannuel Sanga (25) ambaye aligundua kuuawa kwa marehemu Frenk na wao kama polisi walifuka eneo la tukio na kuthibitisha mauaji hayo


0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa