Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFANYABIASHARA
katika soko kuu la Makambako mkoani Njombe wameilalamikia Halmashauri ya Mji
kushindwa kukarabati soko hilo kwa muda mrefu.
Uchakavu
huo umedaiwa unasababisha bidhaa ambazo zinahifadhiwa ndani yake
kuharibika hususani kipindi hiki cha Mvua.
Wafanyabishara
hao wamesema, hali ya soko kwa sasa ni mbaya na usalama wa mali zao
umekuwa wa mashaka licha ya kwamba ushuru umekuwa ukitolewa hata
hivyo maombi yao ya kufanyika ukarabati hayajasikilizwa na uongozi.
Mrundikano
wa taka katika dampo pia umekuwa kero na kuhatarisa usalama wa afya
zao,hali inayotokana na kuchelewa kuzizoa taka hizo.
Mkurugenzi
wa Halamashauri ya Mji Makambako Tina Sekambo amesema kuwa katika
bajeti ya mwaka 2014/15 jumla ya sh, Milioni 150 zimetengwa kwaajili
ya ukarabati wa soko hilo.
0 comments:
Post a Comment