Home » » BIL.7 KUSAFISHA BARABARA YA MCHUCHUMA NA LIGANGA

BIL.7 KUSAFISHA BARABARA YA MCHUCHUMA NA LIGANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Zaidi ya shilingi bilioni saba zinatarajia kutumika  katika matengenezo ya  barabara  ya kutoka  katika kijiji cha Nundu  Wilayani Njombe hadi  Wilayani  Ludewa   ili kuweza kupitisha magari yatakayoanza utekelezaji 
wa mradi wa makaa ya mawe  ya mchuchuma na  mradi wa Liganga  wa 
mchuchuma  uliopo Wilayani Ludewa.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Asery 
Msangi wakati alipofanya kikao na waaandishi  juu ya ziara  aliyoifanya 
katika Wilaya za Mkoa wa Njombe tangu januari mwaka huu mpaka hivi sasa  ambapo alisema kuwa kutokana na 
magari hayo jinsi alivyoyaona kwenye picha hivyo ofisi yake imeandika  
barua kwenda serikali kuu  kwa ajili ya kuomba fedha hiyo.

Halmashauri  amezitaka   kamati itakayosimamia suala la mchakato wa ufikishaji nishati ya umeme vijijini kupitia wakala wa nishati vijijini REA,MCC, pamoja na Tanesco ili kuendana na ilani ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2010/2015 ambapo katika mpango huo  wa matokeo makubwa sasa  kwenye suala la umeme jumla ya vijiji 74 katika mkoa wa Njombe vinatarajia kunufaika na mradi huo.

Akizungumzia suala la mradi wa maji unaendelea mjini njombe Msangi alisema kuwa  jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimepokelewa kutoka serikalini ili kuweza kuedeza mradi huo ambao mpaka kumalizika kwake itanghalimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5 na kuongeza kuwa kufika mwezi june mwaka huu itakuwa imekamilika kwa asilimia 80.

Amebainisha kuwa  jumla ya miradi 41 katika wilaya nne za mkoa wa njombe imekaguliwa miradi ambayo ipo chini  mpango wa matokeo makubwa sasa  ambayo ni katika sekta za kilimo, maji, uchukuzi , nishati, na elimu na kubaini changamoto mbalimbali ambazo amewaagiza watendaji kutatua changamoto hizo na kuwazitaka Halmashauri kuwa makini wanapotoa tenda kwa wazabin.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa