Home » » Nchemba awashukia wafanyabiashara

Nchemba awashukia wafanyabiashara

Licha ya wafanyabiashara Mkoani Njombe na sehemu mbalimbali nchini kugomea suala la matumizi ya mashine za mahesabu za kielektroniki za EFD  naibu waziri wa fedha na sera Mwigulu Lameck Nchemba amewataka wafanyabaishara hao kuendelea kuzinunua na kuzitumia mashine hizo huku serikali ikiendelea kushughulikia tatizo hilo.

Akizungumza wakati wa mkutano na wafanyabiashara mbalimbali mkoani Njombe naibu waziri  Nchemba amesema kuwa kitendo cha wafanyabiashara hao kugomea mashine hizo badala ya kuomba waelimishwe juu ya matumizi yake si uzalendo katika taifa lao.

Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri huyo ameziagiza bodi na mamlaka zinazohusika na suala la kusogeza huduma za mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuhakikisha wanaanzisha haraka ofisi za TRA mkoa wa Njombe ili kupunguza gharama kwa wafanyabiashara ya kusafiri kwenda mkoani Iringa kwa ajili ya kulipa kodi na mambo mengine ya kibiashara

 
Wakihoji juu ya matumizi na gharama za ununuzi wa mashine hizo mbele ya naibu waziri huyo baadhi ya wafanyabiashara wameitaka  serikali kugharamia ununuzi wa mashine hizo huku wengine wakionekana kupinga kabisa kuendelea kutumia mashine hizo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa