Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana
na ukosefu wa elimu ya sheria barabarani miongoni mwa madereva bodaboda
wilayani Makete mkoani Njombe kunakopelekea madereva hao kukamatwa na
askari wa usalama barabarani mara kwa mara, mkuu wa wilaya ya Makete Mh.
Josephine Matiro amefanya kikao na waendesha bodaboda hao
Katika
kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya
Makete, waendesha bodaboda hao walipata fursa ya kutoa kero zao na
kuuliza maswali ambayo yalikuwa yakijibiwa papo kwa papo na Muu wa
polisi wilaya ya Makete, askari wa usalama barabarani na Meneja msaidizi
wa TRA Makete
Akizungumza
kwenye kikao hicho Mkuu wa polisi wilaya ya Makete (OCD) Alfred Kasonde
amekanusha vikali tuhuma zinazoelekezwa kwa askari wake kuwa wanakula
fedha wanazotoza kama faini kwa vyombo vya usafiri wanavyotoza kutokana
na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa ni vingumu kwa askari ambaye
amekuandikia faini ya kosa lako kwenye kitabu cha serikali kula fedha
hiyo
Bw.
Kasonde amesema askari wake hawana vitabu vya risiti na hawaruhusiwi
kutembea navyo kwa kuwa jeshi la polisi lina wahasibu wanaokusanya fedha
hizo, hivyo kwa wilaya ya Makete dereva akiandikiwa faini na askari,
askari haruhusiwi kupokea fedha na badala yake atakuandikia karatasi
maalum maarufu kama notification na baada ya hapo dereva huyo atakwenda
kulipa faini hiyo kituoni
Amewataka
madereva hao kuacha kuwapa fedha ya faini askari hao na badala yake
wahakikishe askari aliyewakamata anaandika kosa hilo kwenye kitabu cha
faini, huku akionesha rundo la risiti za madereva bodaboda ambao
wamelipia faini lakini hawajafika kuchukua risiti zao kwa madai kuwa
fedha walizotoa zililiwa na askari
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro amewataka
madereva hao kuhakikisha wanajikamilisha kwa vitu vyote vinavyohitajika
kama sheria za usalama barabarani zinavyolelekeza ili kuepukana na adha
ya kukamatwa mara kwa mara na askari na kutozwa faini
Mh
Mariro amesema ni kweli madereva wengi hawajui sheria za usalama
barabarani lakini sheria hazitambui kuwa hawafahamu sheria, hivyo ili
kuepukana na adha hiyo wanatakiwa kuwa na vitu vyote vinavyohitajika
kama leseni ya udereva, leseni ya biashara, bima, kadi ya pikipiki,
stika ya nenda kwa usalama, kofia ngumu(helment 2) pamoja na pikipiki
yenye vyake vifaa vyote
Amesema
kwa kulitambua hilo mkuu huyo atafanya mazungumzo na chuo cha VETA
Makete kifanye mafunzo maalum kwa madereva hao kwa gharama nafuu ili
wazifahamu sheria za usalama barabarani pamoja na kupata leseni za
udereva
0 comments:
Post a Comment