WAJASIRIAMALI zaidi ya 191 katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamepatiwa
mafunzo ya nadharia na vitendo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku sita na mkufunzi kutoka mkoani Morogoro Elisante Kazimoto ambaye alisema, kwa kipindi
cha mwaka 2013/14 ameshatoa mafunzo kwa wajasiriamali wasiopungua 680, katika mkoa
wa Njombe.
Akizungumzia kuhusu mafunzo alisema kuwa ni
muhimu kwa wajasiriamali kwani ni kati ya kazi ambazo zinaweza kuwakwamua na kuondokana na umaskini.
Alisema
kuwa mafunzo hayo yalihusu utengenezaji wa batiki, sabuni za mche na za
maji za kuoshea sakafu, mishumaa, mapishi ya vyakula mbalimbali, pia
wamejifunza kutotolesha vifaranga vya kuku kwa kutumia
njia ya kawaida si mashine.
Pia mafunzo hayo yalihusu jinsi ya kuotesha yoga, kutengeneza viatu vya ngozi (kimasai) na
jinsi ya kutengeneza mafuta ya mgando na bidhaa nyingine nyingi, ambapo mafunzo hayo
yamewajengea uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji kwa manufaa ya kuinua uchumi wao.
Kati
ya wadau hao Zena Mnyika ni mmojawapo wa wanufaika wa mafunzo hayo
alisema, kutokana na mafunzo hayo, uwezekano wa kupata mabadiliko
makubwa kiuchumi upo kwa sehemu kubwa na hivyo hali ya utegemezi kwa
baadhi ya wanawake itapungua.
Bi. Zena alisema pamoja na mafanikio
hayo kuna tatizo ambalo kama halitatatuliwa kwa wajasiriamali hao
kupatiwa mafunzo kwa ujumla yatakuwa hayana manufaa na kuishia kuwa na
kumbukumbu za kwenye daftari.
“Ni kweli mafunzo haya yametupa
mwelekeo wa maisha wengi hatukuwa na chochote katika ujuzi, lakini
mafunzo haya yanahitaji mali ghafi na mitaji wanawake wengi hatuna
mitaji ya kutosha kuweza kuendesha miradi inayoibuliwa kupitia mafunzo
haya,”alisema Bi.Zena.
Kupitia gazeti hili aliiomba serikali kutoa
hamasa kwa asasi za kifedha za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali
kuangalia uwezekano wa kuwapa mikopo wajasiriamali wadogo wadogo ili
waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza uzalishaji na kukuza pato la
Taifa lakini pia kwa kuongeza pato la kaya.
Mafunzo hayo yamelenga
kuwapa uelewa wananchi ambao mitaji yao ni ya chini na kwamba mchakato
uliopo ni kuwafi kia wanawake au wajasiriamali wengi zaidi katika mikoa
mbalimbali ikiwepo Kandaya kati ya kanda ya kusini mafunzo ambayo
yanatarajiwa kutolewa ndani ya mwaka 2014.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment