Njombe. Viongozi mbalimbali wa Chadema wameanza kupiga kampeni za urais mwaka 2015 kupitia Operesheni Pamoja Daima.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Njombe huku
mvua kubwa ikinyesha jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa
aliwatahadharisha vigogo wa Serikali wanaoiba fedha za umma kuwa,
atawashtaki na kuwafilisi iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mwaka
2015.
Alisema chama hicho kikishinda dola, kitaboresha
masilahi kwa watumishi waadilifu lakini mafisadi wanaotafuna fedha za
Serikali watapata wakati mgumu.
“Tutakuwa wakali kwa walarushwa,” alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema watendaji walarushwa na wezi watashtakiwa ili mali walizowaibia Watanzania zirejeshwa Serikalini.
“Ninawapa miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu, vigogo
hao kurudisha mali walizoiba vinginevyo watajuta kwa sababu tutawashtaki
tutakapoingia madarakani.” alisema.
Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo
alisema chama hicho kitatumia kila aina ya ‘silaha’ kilichonayo
kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa Kilimanjaro yananyakuliwa na chama
hicho 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Ndesamburo alisema hakuna kikwazo kuyatwaa majimbo hayo kwa vile CCM,
kimeshindwa kuwaletea Watanzania maisha bora kama waliyojinadi mwaka
2010.
Kwa sasa Chadema kinashikilia majimbo ya Moshi
Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo (2000-2015), Jimbo la Hai na Jimbo la
Rombo wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishikilia majimbo matano.
CCM kinashikilia majimbo ya Moshi Vijijini, Siha,
Mwanga, Same Mashariki na Magharibi wakati Tanzania Labour Party (TLP),
kikishikilia Jimbo la Vunjo kupitia Mbunge wake, Augustine Mrema.
Akizungumza mjini Singida jana, Mwanasheria wa
Chadema, Tundu Lissu aliwataka Watanzania kumchagua rais mwadilifu siyo
anayehonga hata mapadri fedha chafu zilizotokana na ufisadi.
Alisema baadhi ya viongozi (bila kuwataja) hivi
sasa wanapita kwenye nyumba za ibada kutoa rushwa na kudai kwamba zamu
yao ya kuwa rais imewadia.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment