*Pia wamo Samia na Dk. MwinyiDiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ramadhani, Wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Livingstone Luvanda, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kupingwa na mgombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya hiyo, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulghence Ngonyani, akizungumza na NIPASHE jana alisema diwani huyo amehamishiwa katika hospitali hiyo kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kibena alikokuwa amelazwa awali.
Mgombea huyo ambaye anagombea nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wilaya ya Njombe (jina tunalihifadhi), alimpiga diwani huyo...
Bweni la wanafunzi lawaka moto Njombe
Zaidi ya wanafunzi 93 wa kidato cha tatu na nne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Wanike mkoani Njombe, wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.
Mkuu wa Wilaya ya Wang’ing’ombe, Esterina Kilasi, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 13, mwaka huu saa 4:00 usiku.
Alisema moto huo uliteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi.
Hata hivyo, alisema moto huo hakuleta madhara kwa upande wa wanafunzi na thamani ya vifaa pamoja na chanzo cha moto huo havijafahamika.
CHANZO: NIPA...
MWENYEKITI MPYA WA CCM LUDEWA AAHIDI MAKUBWA KWAVIJANA
Festus Pangani, Njombe Yetu.
Mwenyekiti wa vijana kupitia Chama Cha Mapinduzi wilayani Ludewa Bi.Elizabeth Augustino Haule ameahidi kufanya mambo makubwa kwa vijana baada ya kumchagua kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mine.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Bi. Elizabeth alisema kutokana na yeye kuwa mjasiliamali atatumia fulsa hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wilayani humo kutoa elimu ya kujitambua kwani vijana walio wengi bado hawajitambui.
Alisema kijana anapaswa kijiajiri na si kusubiri kuajiriwa kwa maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa kutofanya kazi na kusubiri mtu au kampuni ianzishe ndipo uajiliwe.
Elizabeth alibainisha kuwa mafanikio yake mpaka alipofikia kuwa mwenyekiti ni juhudi binafsi na si mtu alikuwa nyuma yake kwani katika mikakati yake ilikuwa...
SEKTA YA UTALII NJOMBE IMETELEKEZWA?
Na Festus Pangani, Njombe YetuSekta ya utalii katika mkoa wa Njombe imesahaulika licha ya kuliingizia taifa kipato kutokana na wageni mbalimbali wanaotembelea vituo vya utalii kwa ajili ya kujionea maajabu mbalimbali katika vivutio hivyo.
Mkoa wa Njombe unavivutio vingi vya utalii, ikiwamo hifadhi ya wanyama ya kitulo, shamba la maua yenye kuvutia na kustaajabisha lililopo Uwemba na mwamba wenye ramani ya afrika unaopatikana katika Kijiji cha Igodiva Tarafa ya Imalinyi wilayani Wanging’ombe.
Hata hivyo kutokuwapo kwa juhudi za kutosha katika kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio hivyo kumechangia vivutio vingi vya utalii kutofahamika hata kwa baadhi ya wenyeji wa mkoa wa huo.Akizungumza na Blogzamikoa Afisa Utalii, Maliasili na Mali kale wa Wilaya ya Njombe Abed Henry Chaula alikiri kuwa ...
BWENI LATEKETEA KWA MOTO NJOMBE, WANAFUNZI 93 WANUSURIKA KIFO
Festus Pangani, Njombe YetuWANAFUNZI 93 wamenusurika kufa baada ya bweni lao kutekea kwa moto usiku wa kuamkia leo katika shule ya sekondari ya wasichana ya Wanike iliyopo Kata ya Mdandu wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe.
Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Estelina Kilasi amesema, tukio hilo limetokea septemba 13 saa 4 usiku na kuteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi hao ambavyo thamani yake bado haijajulikana na chanzo cha moto huo hakijafahamika.aa
Bi Kilasi amsema, bweni ambalo limeteketea ni la wasichana wanaosoma kidato cha tatu na cha nne ambao wote walifanikiwa kutoka nje na kuacha mali zao zikiteketea kwa moto.
Amevitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja ni daftari, vitanda, magodoro na nguo za kiraia na sare zao vyote vimeteketea kwa moto huo.
Kutokana na ajali hiyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza...
NJOMBE MEDIA CLUB YAZINDULIWA
Mwandishi wetu, Njombe YetuSeptemba 11, mwaka huu jamii ya Wananjombe ilishuhudia uzinduzi wa jumuiya ya wanahabari Njombe ambayo inajulikana kwa jina la Njombe Media Club itakayokuwa ikiwaunganisha wanahabari na wadau wa habari wa mkoani humo.Lengo la kuanzishwa kwa club hiyo ya kutetea maslahi ya wanahabari Njombe na kuwekana sawa katika kahakikisha tasnia ya habari mkoani hapa inakua na kuchangia katika maendeleo.Pamoja na kwamba mkoa wa Njombe umeanzishwa muda kidogo uliopita, klabu hii ya waandishi imeanzishwa sasa hasa kwa msukumo wa mauaji ya mwandishi wa kituo cha Channel Ten Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa kijiji cha Nyololo wilayani mufindi katika...
UJENZI WA BARABARA ZA MITAA KWA KIWANGO CHA LAMI NJOMBE WAANZA KWA KASI
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
...
NJOMBE KUANZA KUSAMBAZA PEMBEJEO
Festus Pangani, NjombeWakati msimu wa kilimo ukiwa umeanza kwa baadhi ya mikoa hapa nchini, tayari serikali imeanza kusambaza vocha za ruzuku za pembejeo kwa wakulima ili kwenda sanjari na msimu wa kilimo.Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sara Dumba amesema wilaya ya Njombe ni miongoni mwa wilaya ambazo tayari zimepokea vocha hizo huku wakitarajia kuanza kuzisambaza kwa wakulima ambao shughuli za kilimo huanza mapema katika maeneo yao.Akielezea mchakato wa kufikisha vocha za pembejeo kwa wakulima Dumba amesema hatua za kuwafikishia wakulima hao zinafanyika huku akieleza kuwa zoezi hilo kwa mwaka huu linafanywa na serikali kwa kuyatumia makampuni ambayo yatatafuta mawakala watakaofanya kazi ya usambazaji. Aidha mwenyekiti huyo wa...