Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo
Pinda, amesema kuwa wawekezaji wapo hatua za mwisho kuanzisha uzalishaji wa
chuma na umeme katika eneo la Ludewa.
Kufuatia
kuanza kwa miradi hiyo, Pinda aliagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuandaa
wananchi kwa kutoa elimu kuhusu fursa, zilizopo za kazi katika eneo hilo.
Alisema
kazi ya Serikali hivi sasa ni kuhakikisha inajenga barabara kupitisha mitambo
inayotakiwa kwenye miradi hiyo na kwamba, tayari Sh7 bilioni za awali
zimetengwa kwa upanuzi wa barabara
Kuhusu
ujenzi wa barabara ya lami kutoka Itoni, Ludewa hadi Manda,
Waziri Pinda
alisema tayari Serikali imetenga fedha za upembuzi yakinifu, hivyo wananchi
wasiwe na wasiwasi kuhusu miundo mbinu.
Akizungumzia
sekta ya kilimo, Pinda alisema jembe la mkono haliwezi kumaliza matatizo ya
mkulima, na kinachotakiwa ni kuangalia uwezekano wa kuwakopesha wakulima
matrekta ya bei nafuu.
Serikali
pia katika eneo hilo inapania kuanza kuzalisha megawati za umeme Megawati 600.
0 comments:
Post a Comment