KERO YA MAJI SHULE YA MSINGI NDULAMO WILAYANI MAKETE YAMALIZWA

Na Edwin Moshi, Makete   Kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji katika shule ya msingi Ndulamo wilaya ya Makete mkoani Njombe hatimaye imetatuliwa baada ya idara ya maji wilayani hapo kuamua kutilia mkazo suala hilo   Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Bosco Godigodi Malangalila (pichani) amesema maji yanapatikana kwa wingi shuleni hapo baada ya kuyakosa kwa kipindi kirefu hali iliyokuwa inaleta picha mbaya shuleni hapo.   Amesema tatizo hili limeondoka shuleni hapo baada ya idara ya maji kupeleka mabomba na kuyafunga kufidia yale ya awali yaliyokuwa yakivujisha...

Njombe wavalia njuga usafi wa mazingira

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; ...

Waziri mkuu Pinda asema eneo la Ludewa litapata miradi muhimu ya kiuchumi.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, amesema kuwa wawekezaji wapo hatua za mwisho kuanzisha uzalishaji wa chuma na umeme katika eneo la Ludewa. Kufuatia kuanza kwa miradi hiyo, Pinda aliagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuandaa wananchi kwa kutoa elimu kuhusu fursa, zilizopo za kazi katika eneo hilo. Alisema kazi ya Serikali hivi sasa ni kuhakikisha inajenga barabara kupitisha mitambo inayotakiwa kwenye miradi hiyo na kwamba, tayari Sh7 bilioni za awali zimetengwa kwa upanuzi wa barabara Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka Itoni, Ludewa hadi Manda, Waziri Pinda alisema tayari Serikali imetenga fedha za upembuzi yakinifu, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu miundo mbinu. Akizungumzia sekta ya kilimo, Pinda alisema jembe la mkono haliwezi kumaliza matatizo ya mkulima,...

Pinda ahimiza kilimo cha mazao ya biashara Njombe

WANANCHI wilayani makete Mkoani Njombe, wametakiwa kuboresha mazao ya biashara ambayo yanastawi katika Wilaya hiyo,ili kukuza uchumi kupitia rasiliamali walizo nazo. Akizungumza na wananchi waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda ameagiza wananchi kuimarisha mazao ambayo ni muhimili wa uchumi wao. Amewaondoa shaka wakulima hao kuhusu wanunuzi wa zao la Pareto na kuongeza kuwa kilimo cha matunda, Pareto vinapaswa kuboreshwa ili kuutumia vema fursa ya kilimo katika uzalishaji mazao yanakubalika kimataifa. Kambarage Sanga ni mkulima wa matunda  anayemiliki ekari 3000 za matunda, katika kijiji cha Iniho, akamweleza waziri mkuu jinsi anavyoendesha kilimo cha matunda aina mbalimbali. Baada ya kutembelea bustani ya miche ya matunda na kujionea shughuli za uzalishaji zianazofanywa na wanakikundi...

Waziri Mkuu awaonya viongozi Wanging’ombe

  Na Mwandishi Wetu, Wanging’ombe WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameipa Wilaya mpya ya Wanging’ombe mkoani Njombe hadi mwisho wa mwezi huu kuhakikisha wanafunzi zaidi ya 800, waliofaulu kuingia sekondari lakini hawajafanya hivyo, wawe shuleni. Alikuwa akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ilemela katika siku ya kwanza ya ziara ya wiki mbili katika Mikoa ya Njombe na Ruvuma.Ni dhambi kubwa kuwaacha wanafunzi hao wawe nje ya shule kwa kuwa wamefaulu na kwamba wenzao wengi wanaendelea na masomo na baadhi yao wanaweza kuwa viongozi wa kesho, alisema.“Wasakeni hawa popote walipo na mhakikishe wanakuwa shuleni badala ya kuzurura mitaani. Nakuagiza DC (Mkuu wa Wilaya Esterina...

MHESHIMIWA PINDA ZIARANI MKOA WA NJOMBE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakikagua shamba la nanasi la Katibu Mkuu kiongozi Mstaafu, Philemon Luhanjo (kulia) katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Njombe Julai 10,2013. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia kwakena ) wakikagua shamba la nanasi la Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Philemon Luhanjo (kulia) katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Njombe Julai 10,2013. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akivuna nanasi katika shamba la Katibu Mkuu Mstaafu, Philemon Luhanjo (katikati) lililopo katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako akiwa katika...

UJENZI WA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI MAULU MAKETE UNAKARIBIA KUMALIZIKA

 Kwa mbali utawaona wananchi wakiangalia ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji linalojengwa katika shule ya msingi Maulu kata ya Kipagalo wilayani Makete, kutokana na shule hiyo kukumbwa na uhaba wa maji hasa wakati wa kiangazi hali inayopelekea wanafunzi kupata tabu ya kujisaidia kutokana na vyoo kutumia maji. Ujenzi huo umefadhiliwa na AMREF  Hapa mafundi wakiwa kazini kama uonavyo  bado kidogo tuu ujenzi huo utakamilika Jamaa hasubiri apikiwe, hapa aliamua kuingia jikoni mwenyewe kujipikia ugali kwa ajili yake na mafundi wenzake wanaojenga tanki hilo Picha zote na  Edwin Mos...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa