WANAOJISAIDIA OVYO MAKETE WAICHEFUA SERIKALI
Na Edwin Moshi, Makete
Serikali
wilayani Makete mkoani Njombe imewataka wananchi kutoa ushirikiano wa
pamoja kuwakamata ama kutoa taarifa kwa ngazi husika pindi wanapowaona
watu wakijisaidia ovyo maeneo yasiyo rasmi.
Hayo
yamesemwa na afisa afya wilaya ya Makete Bw Boniphace Sanga wakati
akizungumza na mtandao huu na kuongeza kuwa kumekuwa na ongezako la
magonjwa hasa ya kuhara ambayo yanatokana na watu wanaojisaidia ovyo na
kuchafua mazingira.
Bw
sanga amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja na si la bwana ama bibi
afya pekee na kwa kuwa wananchi ndio wanaoshinda maeneo mbalimbali
wanawaona wale wanaojisaidia hovyo na kuomba watoe taarifa kwenye ofisi
yake ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesema
inashangaza kuona hadi sasa wapo watu ambao hawana vyoo na wanaongoza
kwa kuchafua mazingira kutokana na kujisaidia ovyo, na kutoa wito kuwa
msimu huu ni wa kiangazi hivyo wanatakiwa kujenga vyoo kabla mvua
haijanyesha.
"Kwa
kweli natoa wito nyumba bila choo haijakamilika, acheni
kun***a(akimaaisha kujisaidia) maeneo ambayo si kwa ajili hiyo, unakuta
mtu kavaa vizuri lakini ni namba moja kujisaidia maporini, huu si
ustaarabu na watu wa namna hii ndio wanaoleta magonjwa kwenye wilaya
yetu.
Katika
hatua nyingine Bw. sanga amewaomba wananchi kuendelea kujijengea
utaratibu wa kutupa taka maeneo yanayoruhusiwa( kwenye vizimba vya taka)
na kuwaasa kuacha tabia ya kutupa chupa za soda na maji mitaani kwani
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokamatwa.
SHULE YA MSINGI NKENJA MAKETE: INA HALI TETE!
| Majengo ya shule ya msingi Nkenja, kulia na kushoto ni vyumba vya madarasa, katikati ni ofisi ya mwalimu mkuu. |
| Uongozi wa CCM wilaya ya makete ukishangaa kuona jinsi wanafunzi wanavyopata tabu kusomea kwenye pagale. |
| Madarasa ambayo hayajakamilika lakini yanatumiaka kwa ajili ya darasa la kwanza na la pili. |
| Turubai likining'inia kwenye chumba ambacho wanasomea wanafuzni wa darasa la kwanza na la pili ambalo hulitumia kama bati kuzuia jua. |
Mazingira magumu hasa kwa elimu ya msingi nchini bado yanazidi kuonekana baada ya shule ya msingi Nkenja iliyopo kata ya Kitulo wilayani Makete mkoani Njombe kuonekana ina vyumba viwili tu vya madarasa ambavyo vina hadhi ya kutumiwa kama madarasa
Hali hiyo si imeacha hoi mtandao huu tu bali pia viongozi mbalimbali waliofanya ziara ya kukagua shule hiyo ambayo ilijengwa kwa makusudi ya kuwapunguzia wanafunzi mwendo mrefu wa kilomita 14 wanaotembea kwenda kusoma shule ya msingi Ujuni iliyopo kijiji cha jirani cha Ujuni
Mbali na shule hiyo kuwa na vyumba viwili vya madarasa, chuma kimoja wanasomea wanafunzi wa darasa la tatu na la nne kwa kuchanganywa pamoja, na chumba kimoja wanatumia darasa la tano tu peke yao
Hayo yamebainika baada ya ziara ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula kufanya ziara katika shule hiyo kukagua hali ya ujenzi na maendeleo kwa ujumla katika shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika kata mbalimbali wilayani hapo
Viongozi hao wa CCM wamezidi kushuhudia maajabu katika shule hiyo kwa kujionea chumba ambacho wanasomea wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kikiwa hakina paa, bati wala sakafu ambapo wakati mwingine waalimu hukifunika kwa turubai ili kuwakinga na jua na wakati wa mvua havitumiki
"kama mnavyojionea ndugu viongozi wa CCM hali ni ngumu kwa kweli, tunaupungufu wa vyumba vitano vya madarasa, watoto wa darasa la kwana na la pili wanasomea kwenye chumba hiki ambacho hakina bati muda wote, wakati wa mvua hakitumiki kabisa, na wote tunawachanganya kwenye chumba hiki kimoja" alisema mwalimu mkuu Hester Mahenge
Viongozi hao ambao walikagua vyumba vyote vya shule hiyo pia waligundua shule hiyo ina upungufu wa madawati 50
Akizungumza shuleni hapo katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amewapongeza wananchi wa Nkenja kwa kujitoa kwa gharama zao hadi hapo madarasa mawili yanayojengwa yalipofikia, na kuwaomba kushirikiana na kutilia mkazo suala hilo ili ujenzi huo ukamilike ndani ya mwaka huu
Amesema pamoja na wananchi hao kukabiliwa na michango mingi lakini watoe kipaumbele kwa ujenzi huo ili wanafunzi hao wasome kwa raha ukizingatia wanafunzi wanaosomea pagalani ni wa darasa la kwanza na pili ambao ndio wachanga wanaohitaji msaada kwa ukaribu zaidi
Naye mwenyekiti wa CCM wilayani hapo Francis Chaula amewataka kuandika bajeti ya vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kukamilisha miradi hiyo na waipeleke kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na nakala kwa chama chake ili kutilia mkazo zaidi namna ya kuboresha mazingira ya shule hiyo
Diwani wa kata ya Kitulo ilipo shule hiyo Mbosa Tweve amesema serikali kupitia halmashauri ya wilaya kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 imetoa sh. milioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na muda wowote kuanzia sasa zitapelekwa shuleni hapo na kuahidi kushirikiana kukamilisha ujenzi huo
baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamelalamikia michango ya ujenzi huo kuchangwa na kitongoji kimoja tu ilihali kijiji kina vitongoji vinne na kusema hali hiyo inachangia mradi huo kusuasua, huku hoja hiyo ikijibiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Zablon Chengula kuwa amesawaita wenyeviti wa vitongoji vyote kuzungumzia suala hilo na wapo wananchi ambao wameshapelekwa kwa mtendaji wa kata kushughulikiwa kutokana na kugoma kushiriki zoezi hilo
Shule hiyo ina madarasa matano (I-V) ina jumla ya wanafunzi 51 wanaofundishwa na waalimu watatu tu
Na Edwin Moshi, Makete
Katiba mpya: Wakulima wadai kupuuzwa maoni yako
Njombe
RASIMU ya katiba mpya
imeingia doa baada ya wakulima kudai kuwa tume ya katiba ya Jaji wa Joseph
Walioba imeyapuuza maoni yao.
Hoja hiyo imeibuliwa
katika mkutano mkuu wa mwaka wa muungano wa vikundi vya
wakulima wadogo wadogo nchini (MVIWATA) ambao
umefanyika katika mkoa wa Njombe.
Mkutano huo
umehusisha wanachama na viongozi wa bodi Taifa wa MVIWATA
kutoka Kanda sita zinazojumisha mikoa yote ya Tanzania
bara , ambao ulilenga kuzungumzia maendeleo ya Mtandao kwa ujumla.
Mwenyekiti MVIWATA
Habibu Simbamkuti amesema, kuna mambo ambayo ni ya msingi yamepuuzwa
katika Rasimu ya katiba mpya amabayo walianisha na kuwayawasilisha katika Tume.
Upande wao wakulima
wamesema,licha ya kuwepo vikwazo lukuki pia ushirikishwaji ni
kitendawili kisichoteguka, kile kilichodaiwa kuwa mikataba ya uwekezaji katika
sekta ya ardhi haihusishi maoni ya mkulima moja kwa moja na kusababisha
migogoro kati yao.
Mjadala wa rasimu ya
katiba mpya umehitimishwa mwishoni mwa wiki hii, ambapo maoni na mapendekezo ya
kitaasisi yanawasilishwa kwenye tume ya Jaji mstaafu Joseph
Walioba kabla ya kupeleka kwenye Bunge la katiba Novemba mwaka huu.
mwisho
ZIARA YA VIONGOZI WA CCM WILAYA YA MAKETE YAZIDI KUIBUA MENGI
Viongozi wa CCm wilaya ya Makete wakikagua chumba cha darasa wanachosomea wanafunzi wa darasa la tatu na la nne kwa pamoja
Katibu wa CCM wilaya ya makete Miraji Mtaturu, mwenyekiti Francis Chaula na diwani wa kata ya Kitulo Mbosa Tweve wakisikiliza maelezo kutoka kwa mkuu wa shule ya msingi Nkenja Hester Mahenge ofisini kwake
Viongozi wa CCM wakikagua ujenzi wa madarasa unaodaiwa kusuasua, mwenyekiti wa CCM wilaya ya makete (katikati) akizungumzia ujenzi huo
darasa wanalotumia wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kusomea
Turubai linalotumika kama bati kwenye jengo hilo
Vyumba viwili vya madarasa ambavyo vinafaa kwa matumizi shuleni hapo.
(Picha zote na Edwin Moshi)DK. MAHANGA ATEMBELEA VIWANDA, MASHAMBA YA CHAI NJOMBE
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kulia) akioneshwa mitambo ya kuzalisha majani ya chai katika Kiwanda cha Chai cha Luponde, wilayani Njombe, alipofanya ziara ya kutembelea viwanda na mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi. Kushoto ni Meneja wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Antony Mwai.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akionja aina jibini (cheese) zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa cha CEFA Njombe, wilayani Njombe, alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na Meneja Biashara wa Kiwanda cha Chai Luponde, Athanas Mwasamene alipotembelea hivi karibuni shamba la majani ya chai-dawa (herbal tea) wilayani Njombe. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Chai Luponde, wilayani Njombe, Anthony Mwai (mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), shehena za chai-dawa (herbal tea) zinazozalishwa kiwandani hapo, tayari kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungmza na wafanyakazi.
CHANZO: MICHUZI BLOG
CHANZO: MICHUZI BLOG
MKUU WA WILAYA YA MAKETE AWATAKA NLC KUMALIZA TOFAUTI NA KKKT KATIKA WILAYA HIYO.
Mkuu
wa wilaya ya makete bi. Josephine matilo amewataka viongozi wa dhehebu
la kanisa la kiinjili la kilutheli KKKT Dayosisi ya kusini kati kumaliza
tofauti zilizopo baina yao na viongozi wa huduma ya maisha mapya ndani
ya kristo NLC wilayani hapa.
Ameyasema
hayo akiwa mgeni rasmi wakati wa kufungua mkutano wakuelekea kilele
maadhimisho ya miaka hamsini ya huduma hiyo ya maisha mapya ndani ya
kristo ambao utadumu kwa siku saba ambao unafanyika katika viwanja vya
mabehewani kijiji cha iwawa na kuwataka kudumisha amani na mshikamano
ili kuweza kuyafikia malengo yao.
'viongozi
tunakaa tunarumbana tunawapotosha wananchi tukae meza moja ili kuweza
kumaliza tofauti zetu na si kuendelea kila watu kivyao hapo mnawaumiza
wananchi sote mungu wetu ni mmoja malumbano yanatoka wapi?' aliuliza bi
matilo.
Aidha
mgeni rasmi huyo bi matilo ameeleza kuitambua huduma hiyo na kuwashauri
viongozi na kuwataka kueneza dini jinsi katiba yao inavyosema bila ya
kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania
sisi
kama serikali tunatambua huduma yenu na tunataka injili ifike kila
mahala kwa jinsi mlivyoyaainisha malengo yenu ya kuweza kuimarisha
amani na utulivu kwa wananchi na hatutakaa kimya kama kuna kanisa
linapotosha wananchi alisema bi matilo.
kwa
Upande wake katibu mkuu taifa wa huduma hiyo bw. Daimon Mwandambo
wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema kwa huduma hiyo
imesambazwa katika mikoa 18 ya tanzania bara na kuufanannisha utofauti
huo na uliowahi kujitokeza jijini dar es salaam na ule wa mkoani iringa
ambao ulidumu kwa miaka saba.
CHANZO: JIACHIE BLOG
Mkutano
huo utakaodumu kwa siku saba ambapo kilele cha maadhimisho hayo
yatakuwa septemba 13 na mkutano mkuu kitaifa utafanyika mkoani morogoro
pia katika ufunguzi huo ulilhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa huduma
hiyo wakiwemo uongozi wa mkoa serikali akiwemo mwenyekiti wa
halmashauri bw daniel Okoka na mwakilishi wa mkurugenzi bw. jakob mena,
viongozi siasa nawageni wengine waalikwa.
MWANAFUNZI ALAZIMISHWA NGONO BILA KONDOMU NA MAJANGA MENGINE WILAYANI MAKETE
Kata ya Iwawa ilipo shule hiyo.
Na Edwin Moshi wa Globu ya Jamii, Makete
Wafunzi
wa shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe wamekiri
uwepo wa wanafunzi wenzao ambao wanajihusisha na vitendo vya ngono na
wengine wanaishi na virusi vya UKIMWI, licha ya jamii kudhani kuwa
wanafunzi hawawezi kuwa na virusi hivyo kwa minajili kwamba bado ni
wadogo.
Hayo
yamebainika baada ya mtandao huu kufanya mahojiano ya kina na baadhi ya
wanafunzi wanaosoma shuleni hivi karibuni kwa ruhusa ya mkuu wa shule
hiyo Bw. Christopher Haule hapo kufuatia wananchi wengi wilayani hapo
kudhani kuwa wanafunzi hao hawana maambukizi ya vvu kwa kuwa ni wadogo
na huwenda hawajaanza kujihusisha na vitendo vya ngono.
Mwanafunzi
mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) amesema ana marafiki
zake zaidi ya watano ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI na hajui
walivipataje, hivyo anaamini wapo wanafunzi wengi ambao wana maambukizi.
Amesema
jamii inapaswa kuondokana na dhana potofu kuwa mabinti ama vijana
wadogo hawana vvu waache mara moja kwa kuwa virusi vinampata mtu yeyote
bila kujali umri.
“Mtu
anayedhani kuwa wanafunzi huwa hawana vvu ni uongo, na pia waanatakiwa
kuacha kujihusisha kimapenzi na wanafunzi kwa madai kuwa hawana vvu,
lakini wakumbuke sheria za nchi haziruhusu kujihusisha kimapenzi na
wanafunzi, jamani Ukimwi upo kwa kila mtu” alisema mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi
mwingine amesema yeye hafahamu kama wanafunzi hao wenye vvu
wanajihusisha kimapenzi na watu kwa kuwa wapo ambao wanaishi na wazazi
wao na wengine wamepanga kwenye nyumba maarufu kama mageto ambao kwa
kiasi kikubwa wako huru kufanya mambo yao kwa kuwa hawana muangalizi.
“Ni
kweli kabisa wapo wanafunzi wenye vvu wanaoishi wenyewe kwenye mageto,
lakini mimi sijui kama wana wapenzi ama lah, maana ni ngumu kujua na
mimi sipo hapa kwa ajili ya kufuatilia maisha ya mtu, na hao ninao
kwambia kwa kuwa ni marafiki zangu na waliwahi kuniambia kuwa wanaishi
na vvu” alisema mwanafunzi huyo(jina tunalo)
Mmoja wa mwanafunzi aliyezungumza na mtandao huu
Mwanafunzi upande wa kushoto wa picha hii amemweleza mwandishi wetu kuwa mpenzi wake anamlazimisha kufanya mapenzi bila kondomu
“Mimi
kwa upande wangu Kusema kweli nina mpenzi na nilishawahi kupima vvu
mwaka jana (2012) na kujikuta sina maambukizi namshukuru Mungu kwa hilo,
na pia nimekuwa nikifanya mapenzi kwa kutumia kondomu lakini kuna
wakati mwingine hatutumii mimi na mpenzi wangu na mara nyingi yeye
ndiyo ananishawishi tusitumie, na huyo mpenzi wangu si mwanafunzi ni
jamaa tu wa pale mtaani kwetu, na mimi huwa nakwenda home kwake(Nyambani
kwake) na wakati mwingine anakuja geto kwangu, ili atumie kondom huwa
namwambia leo ni siku zangu za hatari, hapo ndipo atavaa kondomu”
alisema mwanafunzi huyo wa kike ambaye anaishi kwenye nyumba ya
kupanga.
Akizungumzia
suala hilo, diwani wa kata ya Iwawa Benjamin Mahenge alikiri kuwepo kwa
tatizo la ukimwi kwa kila mtu, na kuongeza kuwa hata wanafunzi wapo
wenye vvu ingawa ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na miaka iliyopita
na pia wapo wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya ngono, na ambao
wameshabainika wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria
Diwani wa kata ya Iwawa Benjamin Mahenge (kushoto) akizungumza na mwandishi wa habari hizi
"Unajua
ni ngumu mwanafunzi kuniambia mimi ama kiongozi mwingine kuwa
anajihusisha kimapenzi na mtu lakini kwako mwandishi kasema, mimi
ninaomba wawe wawazi ili tuweze kuwasaidia hasa pale linapojitokeza
tatizo hasa mimba kwa kuwa hawawataji wahusika" alisema Mahenge
Mahenge
amesema huu ni muda wa jamii kubadilika na kuondokana na dhana potofu
kuwa wanafunzi hawawezi kuwa na vvu, na pia wawaache wanafunzi hao
wasome na si kuwarubuni na kujikuta wakifanya nao mapenzi
Pia
amesema wapo wanafunzi katika kata yake ambao wamepanga na uangalizi
wao si mzuri kwa kuwa wanajiamulia mambo yao wenyewe hata kama si mazuri
kutokana na kukosa uangalizi wa watu wazima.
“Unakuta
mwanafunzi kajipangia kwenye chumba chake, yeye ndio kila kitu, akitaka
kusoma haya, akitaka kwenda disco hakuna wa kumuuliza, hii ni hatari
pia” alisema Mahenge
Moja ya nyumba iliyoko Makete mjini amayo wanafunzi wamepanga
Kwa Hisani ya Edwin Moshi
MKUU WA WILAYA WA MAKETE ATAKA ELIMU YA VVU IENDE PAMOJA NA UJASILIAMALI
Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya akisikiliza maelezo ya mradi huo
kutoka SUMASESU
Mkurugenzi
wa shirika la SUMASESU Egnatio Mtawa akitoa maelezo kwa washiriki
kuhusu utambulisho wa mradi uitwao "Vijana wa makete na mapambano dhidi
ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi" katika ukumbi wa HIMA Makete
wakati wa utambulisho wa mradi huo ngazi ya wilaya Augusti 09, 2013.
Shirika la SUMASESU ndilo litakalotekeleza mradi huo kwa ushirikiano na
UNICEF
Washiriki wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa SUMASESU (hayupo pichani)
Mratibu wa ukimwi halmashauri ya wilaya ya Makete CHAC Ester Lamosai(kushoto) akiwa na Anifa Mwakitalima kutoka SUMASESU
Mtaribu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga akichangia hoja kwenye kikao hicho
Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati wa
ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya katika ukumbi wa HIMA Makete
Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Makete Jison Mbalizi akiahirisha kikao hicho
***********************888888
Na Edwin Moshi, Makete
Wadau
wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana wilayani Makete
mkoani Njombe wametakiwa kutoa elimu hiyo sanjari na elimu ya
ujasiriamali kwa pamoja kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza
ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo kwa kasi zaidi
Rai
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro wakati
akifungua mradi wa vijana wa Makete na mapambano dhidi ya UKIMWI
uliozinduliwa Ijumaa Agosti 9, 2013 ngazi ya wilaya, mradi ambao
utatekelezwa na shirika la sumasesu kwa ufadhili wa UNICEF
Matiro
amesema vijana wengi wamekuwa wakipatiwa elimu hiyo ya namna ya
kujilinda na maambukizi mapya ya vvu na baada ya hapo wanakosa kazi ya
kufanya hivyo kuwa rahisi kwao kujiingiza kwenye vitendo
vitakavyowasababishia kupata vvu
"Kijana
anapewa elimu sawa lakini hana cha kufanya mwishowe akija mtu wa
kuwarubuni hasa kifedha wanaingia kilaini kwa kuwa hana shughuli yeyote
inayomuingizia kipato, mwishowe anaweza kupata vvu"alisema Matiro
Amewataka
vijana kujiunga na vikundi mbalimbali ili waweze kupatiwa mikopo nafuu
kwa ajili ya shughuli hasa kilimo kwa kuwa wakishajiunda na kutoa
taarifa yeye kwa kushirikiana na halmashauri watawasaidia kupata mkopo
ambapo wakati huo huo wakiwa na shughuli ya kufanya halafu wakapata
elimu ya kujikinga na vvu itakuwa bora na yenye manufaa kwao
Wadau
walioshiriki katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa HIMA
Makete akiwemo mratibu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga
amelitaka shirika hilo wakati wa kutekeleza mradi huo watoe elimu ya
tohara kwa vijana wa kiume ambapo akiwataarifu wao kama idara ya afya
wako tayari kuungana nao jambo lililoungwa mkono na kaimu mganga mkuu
Boniphace Sanga ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho
Kwa
upande wao shirika la SUMASESU kupitia kwa mkurugenzi Egnatio Mtawa
alipongeza kwa ushirikiano uliooneshwa na wadau wote huku akimuahidi
mkuu wa wilaya kuwa wataingiza mada ya ujasiriamali wakati wakitoa elimu
ya ukimwi kwa vijana ili iwasaidie huku akiahidi kushirikiana na kila
wahusika ili mradi huo ufanikiwe
Mradi huo utakaotekelezwa hadi Julai 2015, utahusisha kata za Ipelele, Iniho, Iwawa, Isapulano na Kitulo




