Home » » MKUU WA WILAYA YA MAKETE AWATAKA NLC KUMALIZA TOFAUTI NA KKKT KATIKA WILAYA HIYO.

MKUU WA WILAYA YA MAKETE AWATAKA NLC KUMALIZA TOFAUTI NA KKKT KATIKA WILAYA HIYO.




NA James Festo, Makete

Mkuu wa wilaya ya makete bi. Josephine matilo amewataka viongozi wa dhehebu la kanisa la kiinjili la kilutheli KKKT Dayosisi ya kusini kati kumaliza tofauti zilizopo baina yao na viongozi wa huduma ya maisha mapya ndani ya kristo NLC wilayani hapa.


Ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi wakati wa kufungua mkutano wakuelekea kilele  maadhimisho ya miaka hamsini ya huduma hiyo ya maisha mapya ndani ya kristo ambao utadumu kwa siku saba ambao unafanyika  katika viwanja vya mabehewani kijiji cha iwawa  na kuwataka kudumisha amani na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo yao.


'viongozi tunakaa tunarumbana tunawapotosha wananchi tukae meza moja ili kuweza kumaliza tofauti zetu na si kuendelea kila watu kivyao hapo mnawaumiza  wananchi sote mungu wetu ni mmoja malumbano  yanatoka wapi?' aliuliza bi matilo.


Aidha mgeni rasmi huyo bi matilo ameeleza kuitambua huduma hiyo na kuwashauri viongozi na kuwataka kueneza dini jinsi katiba yao inavyosema  bila ya kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania


sisi kama serikali tunatambua huduma yenu na tunataka injili ifike kila mahala  kwa jinsi mlivyoyaainisha malengo yenu ya kuweza kuimarisha amani na utulivu kwa wananchi na hatutakaa kimya kama kuna kanisa linapotosha wananchi  alisema bi matilo.


kwa Upande wake katibu mkuu taifa  wa huduma hiyo bw. Daimon Mwandambo wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema kwa huduma hiyo imesambazwa katika mikoa 18 ya tanzania bara na kuufanannisha utofauti huo na uliowahi kujitokeza jijini dar es salaam na ule wa mkoani iringa ambao ulidumu kwa miaka saba.  

CHANZO: JIACHIE BLOG
Mkutano huo utakaodumu kwa siku saba ambapo kilele cha maadhimisho hayo yatakuwa septemba 13 na mkutano mkuu kitaifa utafanyika mkoani morogoro pia katika ufunguzi huo  ulilhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa huduma hiyo  wakiwemo uongozi wa mkoa serikali akiwemo mwenyekiti wa halmashauri bw daniel Okoka na mwakilishi wa mkurugenzi bw. jakob mena, viongozi siasa nawageni wengine waalikwa.  

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa