Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya akisikiliza maelezo ya mradi huo
kutoka SUMASESU
Mkurugenzi
wa shirika la SUMASESU Egnatio Mtawa akitoa maelezo kwa washiriki
kuhusu utambulisho wa mradi uitwao "Vijana wa makete na mapambano dhidi
ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi" katika ukumbi wa HIMA Makete
wakati wa utambulisho wa mradi huo ngazi ya wilaya Augusti 09, 2013.
Shirika la SUMASESU ndilo litakalotekeleza mradi huo kwa ushirikiano na
UNICEF
Washiriki wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa SUMASESU (hayupo pichani)
Mratibu wa ukimwi halmashauri ya wilaya ya Makete CHAC Ester Lamosai(kushoto) akiwa na Anifa Mwakitalima kutoka SUMASESU
Mtaribu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga akichangia hoja kwenye kikao hicho
Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati wa
ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya katika ukumbi wa HIMA Makete
Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Makete Jison Mbalizi akiahirisha kikao hicho
***********************888888
Na Edwin Moshi, Makete
Wadau
wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana wilayani Makete
mkoani Njombe wametakiwa kutoa elimu hiyo sanjari na elimu ya
ujasiriamali kwa pamoja kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza
ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo kwa kasi zaidi
Rai
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro wakati
akifungua mradi wa vijana wa Makete na mapambano dhidi ya UKIMWI
uliozinduliwa Ijumaa Agosti 9, 2013 ngazi ya wilaya, mradi ambao
utatekelezwa na shirika la sumasesu kwa ufadhili wa UNICEF
Matiro
amesema vijana wengi wamekuwa wakipatiwa elimu hiyo ya namna ya
kujilinda na maambukizi mapya ya vvu na baada ya hapo wanakosa kazi ya
kufanya hivyo kuwa rahisi kwao kujiingiza kwenye vitendo
vitakavyowasababishia kupata vvu
"Kijana
anapewa elimu sawa lakini hana cha kufanya mwishowe akija mtu wa
kuwarubuni hasa kifedha wanaingia kilaini kwa kuwa hana shughuli yeyote
inayomuingizia kipato, mwishowe anaweza kupata vvu"alisema Matiro
Amewataka
vijana kujiunga na vikundi mbalimbali ili waweze kupatiwa mikopo nafuu
kwa ajili ya shughuli hasa kilimo kwa kuwa wakishajiunda na kutoa
taarifa yeye kwa kushirikiana na halmashauri watawasaidia kupata mkopo
ambapo wakati huo huo wakiwa na shughuli ya kufanya halafu wakapata
elimu ya kujikinga na vvu itakuwa bora na yenye manufaa kwao
Wadau
walioshiriki katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa HIMA
Makete akiwemo mratibu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga
amelitaka shirika hilo wakati wa kutekeleza mradi huo watoe elimu ya
tohara kwa vijana wa kiume ambapo akiwataarifu wao kama idara ya afya
wako tayari kuungana nao jambo lililoungwa mkono na kaimu mganga mkuu
Boniphace Sanga ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho
Kwa
upande wao shirika la SUMASESU kupitia kwa mkurugenzi Egnatio Mtawa
alipongeza kwa ushirikiano uliooneshwa na wadau wote huku akimuahidi
mkuu wa wilaya kuwa wataingiza mada ya ujasiriamali wakati wakitoa elimu
ya ukimwi kwa vijana ili iwasaidie huku akiahidi kushirikiana na kila
wahusika ili mradi huo ufanikiwe
Mradi huo utakaotekelezwa hadi Julai 2015, utahusisha kata za Ipelele, Iniho, Iwawa, Isapulano na Kitulo
0 comments:
Post a Comment