Na Edwin Moshi, Makete
Serikali
wilayani Makete mkoani Njombe imewataka wananchi kutoa ushirikiano wa
pamoja kuwakamata ama kutoa taarifa kwa ngazi husika pindi wanapowaona
watu wakijisaidia ovyo maeneo yasiyo rasmi.
Hayo
yamesemwa na afisa afya wilaya ya Makete Bw Boniphace Sanga wakati
akizungumza na mtandao huu na kuongeza kuwa kumekuwa na ongezako la
magonjwa hasa ya kuhara ambayo yanatokana na watu wanaojisaidia ovyo na
kuchafua mazingira.
Bw
sanga amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja na si la bwana ama bibi
afya pekee na kwa kuwa wananchi ndio wanaoshinda maeneo mbalimbali
wanawaona wale wanaojisaidia hovyo na kuomba watoe taarifa kwenye ofisi
yake ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesema
inashangaza kuona hadi sasa wapo watu ambao hawana vyoo na wanaongoza
kwa kuchafua mazingira kutokana na kujisaidia ovyo, na kutoa wito kuwa
msimu huu ni wa kiangazi hivyo wanatakiwa kujenga vyoo kabla mvua
haijanyesha.
"Kwa
kweli natoa wito nyumba bila choo haijakamilika, acheni
kun***a(akimaaisha kujisaidia) maeneo ambayo si kwa ajili hiyo, unakuta
mtu kavaa vizuri lakini ni namba moja kujisaidia maporini, huu si
ustaarabu na watu wa namna hii ndio wanaoleta magonjwa kwenye wilaya
yetu.
Katika
hatua nyingine Bw. sanga amewaomba wananchi kuendelea kujijengea
utaratibu wa kutupa taka maeneo yanayoruhusiwa( kwenye vizimba vya taka)
na kuwaasa kuacha tabia ya kutupa chupa za soda na maji mitaani kwani
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokamatwa.
0 comments:
Post a Comment