MAKALA MICHEZO: BUSWITA NA OBI KOSA MOJA ADHABU TOFAUTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na Honorius Mpangala

Ilikuwa ni mwaka 2006 klabu ya Manchester United ilipofanya ujanja kumsainisha John Michael Nchekwube Obinna. Obi kama anavyojulikana na wengi akiwa klabu ya FK Lyn ya Norway alijikuta akiingia tamaa ya kuvaa jezi ya United na kuingia mkataba wa awali bila wakala wake na klabu yake kujua.

Akili aliyoitumia Obi ni ya wachezaji wetu wa kiafrika ambao wana teswa na ile methali "tamaa mbele mauti nyuma".Akiwa mzaliwa wa mji wa Jos katikati ya Nigeria alianza safari yake ya soka katika klabu ya hapo nyumbani kwao ya Plateau United.

Akiwa Norway Obi alipotea ghafla katika klabu yake na kusemekana kuwa ametekwa. Kumbe iligundulika alikuwa na Watu wa Manchester United ndipo alifanya 'uswahili' wa kusaini kandarasi ya kuitumikia United. Baadae picha zikasambaa kwenye mitandao akiwa na jezi ya United.
Kwa mapungufu yaliyofanywa na United iliwafanya Chelsea,kupita njia halali ya kumsajili. Uhalali na uwazi walioutumia Chelsea ukaonekana kuwa Manchester walimlazimisha Obi na kutokana na ukubwa wa klabu yao alijikuta anashindwa kukataa kuichezea klabu yao.
Baada ya sakata kufikishwa mbele ya Uefa maamuzi yanatolewa kuwa Manchester United walimsajili Obi kwa njia zisizo sahihi. Hawakumtumia wakala wake walimteka kijana wa watu lakini katika mazingira ambayo hata klabu yake inasemekana walijua ila hawakutaka kuwa wawazi. Maamuzi yalimnufaisha Chelsea na hatimaye Obi mwenyewe kwa kinywa chake akasema nataka kucheza Chelsea na sio Manchester United. Akakazia kuwa huko nilisaini kwa kushinikizwa.

HAKIMU MAKETE: ACHENI KUWALAUMU POLISI WANAPOTOA DHAMANA KWA WATUHUMIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Edwin Moshi

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Makete Mjini ameitaka jamii kuacha kutupa lawama kwa polisi ama Mahakama pale Mtuhumiwa anapoachiwa kwa dhamana

Ameyasema hayo hivi karibuni katia kikao Maalum cha timu ya ulinzi na usalama wa Mtoto kilichoketi katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete kujadili mambo mbalimbali Kuhusu Watoto

"Kama kuna mahali unapoona huridhiki na kupewa dhamana mtuhumiwa, nenda polisi ukaulize, na kama ni mahakamani nenda mahakamani ukaulize na sio kuwalaumu polisi au mahakama mitaani" amesema hakimu huyo

Zaidi Tazama video hii hapa chini:-

WATANZANIA TUUNGE MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KWA VITENDO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na Agness Moshi - MAELEZO.
 
Tukielekea miaka miwili tangu kuapishwa kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Awamu Ya Tano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ni wajibu wa kila Mtanzania mwenye kiu ya maendeleo na mzalendo kwa nchi yake kuunga mkono juhudi za Rais ili kuifikia Tanzania ya uchumi wa kati ifikapo mwaka  2025.
 
Nakumbuka hotuba yake ya kwanza baada ya kula kiapo cha kulitumikia Taifa hili  aliyoitoa katika shughuli za kuapishwa uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam, Novemba 5, mwaka  2015 ambayo ilibeba maneno yenye busara, hekima na yenye hamasa ya  kuleta maendeleo ya nchi yetu.
 
“Nchi yetu ni kubwa kuliko vyama vyetu vya siasa, mapenzi yetu na matakwa yetu.Uchaguzi Mkuu sasa umekwisha sote tushikamane kama watu wa Taifa moja kuijenga nchi yetu kwa kuweka itikadi na vyama vyetu pembeni”,alisema Rais Magufuli.
 
Ni wazi maendeleo ya nchi hayana dini, kabila, itikadi au chama bali yana undugu na uzalendo, ushirikiano, umoja, kufanya kazi kwa bidii na amani baina ya wananchi na serikali kwa ujumla.
 
Hivyo basi, tunawajibu wa kushikamana kama watoto wa baba mmoja na kufanya kazi kwa bidii na kuunga mkono juhudi  za Rais  Magufuli kwa vitendo ili tuweze kuifikisha Nchi kwenye uchumi wa kati utakaotuwezesha kupambana na maadui wakubwa watatu ambao ni Maradhi, Ujinga na Umaskini badala ya kukaa vijiweni kujadili mambo yasiyo na tija kwa  maendeleo yetu.
 
Aidha, hivi karibuni tumeshuhudia Taasisi, Mashirika,Viongozi mbalimbali wa dini na serikali  na watu mbalimbali wakituma salamu za pongezi kwa Rais Magufuli kwa juhudi na utendaji kazi wake. Lakini je?,tumewahi kujiuliza pongezi hizi na za maneno tu au wanashiriki kwa vitendo?
 
Sina maana kuwa, kumpongeza Rais ni vibaya au uovu,ni jambo jema lakini ingekua vyema zaidi kama pongezi zingeambatana na vitendo  kwani  “maneno bila vitendo si kitu” ndio maana Serikali  Awamu Ya Tano inaongozwa na  kaulimbiu  ya “HAPA KAZI TU” kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kufanyakazi kwa  bidiii badala ya kusubiri serikali kuwafanyia kila kitu.Kauli mbiu hii imekua ikitumika pia nchi mbalimbali duniani ili kuhamasishana katika kufanyakazi na kujiletea maendeleo.
 
Maneno ya Rais Magufuli alipohutubia Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya Kwanza yanaishi na kutekelezwa kwa vitendo katika Serikali ya Awamu ya Tano hadi  kwa wananchi wenye kupenda maendeleo .
 
“Kila mmoja wetu afanye kazi, awe shambani, ofisini, kiwandani, sokoni, kwenye bustani na kadhalika badala ya kupoteza muda vijiweni”, alisema Rais Magufuli.
Ni wazi kuwa , Rais Magufuli amekuwa kiongozi  anayeisimamia na kutekeleza kauli mbiu ya Serikali yake kikamilifu tangu aingie  madarakani kwa  kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha utekelezaji wa  miradi mbalimbali ambayo imekua na manufaa makubwa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.
 
Hivi karibuni,  tumeshudia Mradi  wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka kwenye bandari ya Tanga kwasababu  ni  moja ya mradi mkubwa ambao nchi imetekeleza na utakaobadilisha maisha ya watanzania takribani elfu 30 kwa wakati mmoja. Pia, kuinufaisha Serikali kupitia kodi na utengenezaji wa ajira kwa wananchi wake.
 
Ipo miradi midogo ambayo imetekelezwa na tumeona , ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, mfano barabara ya Msata-Bagamoyo na  Kagoma-Biharamuro-Lusahunga na  mabadiliko kwenye sekta ya afya ambayo yamekua msaada mkubwa katika  kubadilisha maisha ya watanzania na kuifanikisha safari ya nchi kuelekea uchumi wa kati na ujenzi wa Tanzania ya viwanda.
 
Kama Serikali iliahidi na imetekeleza, yatupasa kuhakikisha tunafanya kazi kwa biidi kwenye miradi hiyo na kuhakisha tunailinda ili isiharibike kwa namna yoyote badala ya kutoa pongezi za maneno matupu.

HALMASHAURI YA MJI NJOMBE YANG’ARA KWA HATI SAFI RIPOTI YA CAG, IDARA ZAASWA KUTOKIONA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI KAMA MWIBA WA PORI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.








Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Njombe Dorcas Mkello akiwasilisha hoja za ukaguzi mbele ya Mkutano Maalumu wa Baraza Kuu la Madiwani.




Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Mji Njombe wakisikiliza kwa Makini mapendekezo ya Baraza la Madiwani.




Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu akitoa mapendekezo yake mara baada ya kupitia hoja za ukaguzi.




Madiwani wakipitia makabrasha yenye hoja za Ukaguzi.

Na Hyasinta Kissima, Njombe

Halmashauri ya Mji Njombe imerudisha heshima yake kwa kupata Hati safi katika ripoti ya mthibiti na mkaguzi wa serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/2016) ambapo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Halmashauri hiyo ilipata hati inayoridhisha na yenye maswala ya msisitizo.

Akitoa mapendekezo yake wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani la kujadili hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Katibu Tawala Mkoa wa Njombe  Jackson Saitabahu ameipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi na kwa kukusanya mapato kwa asilimia 100.1 na amezitaka idara na vitengo vya Halmashauri kutoona Ofisi ya Ukaguzi wa ndani kama mwiba wa pori na mahali pasipoingilika kwani Kitengo hicho kipo kwa ajili ya kutoa ushauri lakini pia kuiandaa Halmashauri kwa Ukaguzi Mkuu hivyo wasisite kuomba ushauri pale inapobidi.

“Hati safi haiji kwa bahati mbaya, napenda niwapongeze kwa jitihada kubwa mlizoonyesha lakini pia niwasihi sana msikwepe Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo hiki kinatakiwa kiwezeshwe vizuri na Halmashauri ijenge mahusiano mazuri na Kitengo cha Ukaguzi kwani wakaguzi wa ndani ndio wanatuandaa kwa ajili ya ukaguzi wa nje.Tunapoimarisha mahusiano mazuri miongoni mwetu hatutakua na hoja za ukaguzi.Tusiwe mabingwa wa kujibu hoja zaidi ya kuwa wataalamu wa kuzuia hoja zisitokee.”Alisema Katibu Tawala.

Sambamba na hilo Halmashauri pia imeendelea kuimarika kwa kufikia asilimia 35% za kuweza kujitegemea jambo ambalo limeendelea kuifanya Halmashauri ya Mji Njombe kufanya vizuri katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa mwaka 2017/2018 Halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa hoja zote zinafungwa, kukusanya mapato zaidi ya mwaka uliopita na kuhakikisha kuwa Halmashauri haitoruhusu kufanya biashara na Wakandarasi na wazabuni wasio na mashine za kielektroniki na kuhakikisha kuwa nyaraka na kumbukumbu zote za manunuzi zinatunzwa ipasavyo.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa