Na Agness Moshi - MAELEZO.
Tukielekea
miaka miwili tangu kuapishwa kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa Rais wa
Awamu Ya Tano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ni wajibu wa kila
Mtanzania mwenye kiu ya maendeleo na mzalendo kwa nchi yake kuunga mkono
juhudi za Rais ili kuifikia Tanzania ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Nakumbuka
hotuba yake ya kwanza baada ya kula kiapo cha kulitumikia Taifa hili
aliyoitoa katika shughuli za kuapishwa uwanja wa Uhuru jijini Dar Es
Salaam, Novemba 5, mwaka 2015 ambayo ilibeba maneno yenye busara,
hekima na yenye hamasa ya kuleta maendeleo ya nchi yetu.
“Nchi
yetu ni kubwa kuliko vyama vyetu vya siasa, mapenzi yetu na matakwa
yetu.Uchaguzi Mkuu sasa umekwisha sote tushikamane kama watu wa Taifa
moja kuijenga nchi yetu kwa kuweka itikadi na vyama vyetu
pembeni”,alisema Rais Magufuli.
Ni
wazi maendeleo ya nchi hayana dini, kabila, itikadi au chama bali yana
undugu na uzalendo, ushirikiano, umoja, kufanya kazi kwa bidii na amani
baina ya wananchi na serikali kwa ujumla.
Hivyo
basi, tunawajibu wa kushikamana kama watoto wa baba mmoja na kufanya
kazi kwa bidii na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa vitendo ili
tuweze kuifikisha Nchi kwenye uchumi wa kati utakaotuwezesha kupambana
na maadui wakubwa watatu ambao ni Maradhi, Ujinga na Umaskini badala ya
kukaa vijiweni kujadili mambo yasiyo na tija kwa maendeleo yetu.
Aidha,
hivi karibuni tumeshuhudia Taasisi, Mashirika,Viongozi mbalimbali wa
dini na serikali na watu mbalimbali wakituma salamu za pongezi kwa Rais
Magufuli kwa juhudi na utendaji kazi wake. Lakini je?,tumewahi
kujiuliza pongezi hizi na za maneno tu au wanashiriki kwa vitendo?
Sina
maana kuwa, kumpongeza Rais ni vibaya au uovu,ni jambo jema lakini
ingekua vyema zaidi kama pongezi zingeambatana na vitendo kwani
“maneno bila vitendo si kitu” ndio maana Serikali Awamu Ya Tano
inaongozwa na kaulimbiu ya “HAPA KAZI TU” kwa lengo la
kuhamasisha Watanzania kufanyakazi kwa bidiii badala ya kusubiri
serikali kuwafanyia kila kitu.Kauli mbiu hii imekua ikitumika pia nchi
mbalimbali duniani ili kuhamasishana katika kufanyakazi na kujiletea
maendeleo.
Maneno
ya Rais Magufuli alipohutubia Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania
kwa mara ya Kwanza yanaishi na kutekelezwa kwa vitendo katika Serikali
ya Awamu ya Tano hadi kwa wananchi wenye kupenda maendeleo .
“Kila
mmoja wetu afanye kazi, awe shambani, ofisini, kiwandani, sokoni,
kwenye bustani na kadhalika badala ya kupoteza muda vijiweni”, alisema
Rais Magufuli.
Ni
wazi kuwa , Rais Magufuli amekuwa kiongozi anayeisimamia na kutekeleza
kauli mbiu ya Serikali yake kikamilifu tangu aingie madarakani kwa
kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi
mbalimbali ambayo imekua na manufaa makubwa kwa wananchi na Serikali kwa
ujumla.
Hivi
karibuni, tumeshudia Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima
nchini Uganda mpaka kwenye bandari ya Tanga kwasababu ni moja ya mradi
mkubwa ambao nchi imetekeleza na utakaobadilisha maisha ya watanzania
takribani elfu 30 kwa wakati mmoja. Pia, kuinufaisha Serikali kupitia
kodi na utengenezaji wa ajira kwa wananchi wake.
Ipo
miradi midogo ambayo imetekelezwa na tumeona , ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, mfano barabara ya
Msata-Bagamoyo na Kagoma-Biharamuro-Lusahunga na mabadiliko kwenye
sekta ya afya ambayo yamekua msaada mkubwa katika kubadilisha maisha ya
watanzania na kuifanikisha safari ya nchi kuelekea uchumi wa kati na
ujenzi wa Tanzania ya viwanda.
Kama
Serikali iliahidi na imetekeleza, yatupasa kuhakikisha tunafanya kazi
kwa biidi kwenye miradi hiyo na kuhakisha tunailinda ili isiharibike kwa
namna yoyote badala ya kutoa pongezi za maneno matupu.
0 comments:
Post a Comment