BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha Sita na ule wa Ualimu, umeanza vizuri katika maeneo yote
nchini. Akizungumza jana ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa mtihani
wa taifa, Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi alisema mtihani huo
umeanza kwa wakati uliopangwa na umefanyika katika hali ya utulivu na na
amani.
“Taarifa za kanda zote zinaonesha kuwa mtihani umeanza vizuri maeneo
yote, kwa wakati na umefanyika katika mazingira ya utulivu kama taratibu
za mtihani zinavyotaka,” alisema Nchimbi. Mtihani wa Kidato cha Sita
ulianza Jumatatu na utafanyika hadi Mei 19, mwaka huu wakati ule wa
Ualimu utafikia tamati Mei 13, mwaka huu.
Jumla ya watahiniwa 74,920 wanafanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha
Sita katika shule mbalimbali nchini huku watahiniwa 11,597 wakifanya
mtahini wa ualimu. Kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa
65,610 ni watahiniwa wa shule huku watahiniwa wa kujitegemea wakiwa
9,310.
Kati ya watahiniwa wa shule 65, 610, wasichana ni 24,549 na wavulana
ni 41,061 huku watahiniwa wa kujitegemea wasichana wakiwa ni 3,176 na
wavulana ni 6,134. Kwa upande wa mtihani wa ualimu, watahiniwa 11,597
wanafanya mtihani wa Ualimu.
Kati ya hao watahiniwa 10,942 wanafanya mtihani wa Ualimu daraja A na
watahiniwa 654 wanafanya mtihani wa Diploma ya sekondari na mmoja
anafanya mtihani wa Ualimu wa Diploma ya Ufundi.
Chanzo
Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment