Na Benedict Liwenga, MAELEZO
JUMLA
ya dola Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa
Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari
mini Dodoma.
Amesema
mradi huo unaojengwa kwa ubia kati ya Tanzania Kupitia Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya China ya Sichuan Hongda Group
unatarajia kuanza mwaka huu.
Mhe.
Mwijage amesema kuwa fedha za kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka
maeneo ya mradi huo ziko tayari ambapo zinatarajiwa kutumika zaidi ya
bilioni 13 kwa ajili ya fidia na makazi.
Alisema
kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasadia kuzalisha umeme Megawati 600
ambapo 250 zitatumika katika Kiwanda cha Chuma na nyingine 350
zitapelekwa kwenye Gridi ya Taifa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika
nishati ya umeme.
‘’Pamoja
na kuchimba chuma, Mradi wa Mchuchuma na Liganga utahusisha ujenzi wa
Kinu cha Umeme chenye uwezo wa Megawati 600”, alisema Mhe. Mwijage.
Ameongeza
kuwa, Tanzania kwa sasa itakuwa na umeme wa gesi, maji na umeme wa
makaa ya mawe ambapo umeme wa makaa ya mawe utakuwa msaada mkubwa kwa
nchi kwani hautegemei tabianchi kama ilivyo vyanzo vingine vya umeme.
Mhe.
Mwijage amesema kuwa katika mradi huo, Tanzania itakuwa na hisa
asilimia 20 na Mwekezaji kutoka China atakuwa na asilimia 80, lakini
hisa za Tanzania zinaweza kuongezeka hadi kufikia 45.
Chini
ya mradi huo, Mwekezaji huyo anatakiwa kutoa elimu kwa Vijana katika
ngazi zote za teknolojia zitakazohusika kutengeneza mgodi huo.
‘’Tutafundisha
vijana wetu kwa ngazi tofauti kwani kampuni hii ni ya ubia kati ya
Tanzania na China, tuna mamlaka sawa, tuna Wakurugenzi wetu wa Tanzania
ndani ya hiyo kampuni, kwahiyo tutashiriki na hatutakuwa watazamaji”,
alisema Mhe. Mwijage.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia Viwanda,
Biashara na Uwekezaji ambaye pia ni Mtaalam katika masuala ya madini,
Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu amesema kuwa, lengo la kuwajengea makazi wakazi
wa maeneo ya mradi huo ni kuwawezesha wakazi hao kuwa na uhusiano mzuri
na mgodi unaotarajiwa kujengwa.
‘’Serikali
imeamua kuwajengea makazi wananchi ambao wanazunguka mradi Ili kuepusha
wakazi hao kutumia pesa watakayolipwa kama fidia kwa matumizi mengine
na kukosa makazi baadaye kuja kuilaumu Serikali kwamba imewadhulumu kwa
kutowapa pesa za kutosha za kujenga nyumba”, alisema Dkt. Kafumu.
0 comments:
Post a Comment