Baadhi ya vijana wanaonufaika na fursa hiyo |
Baadhi ya wanafamilia na wadau mbali mbali |
washiriki wakifuatilia hafla hiyo |
Mkurugenzi wa taasisi ya Mafanikio foundation for personal development na mratibu wa raslimali watu Bw Michael uhahula akitoa maelezo mafupi kabla ya mgeni rasmi |
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Adam Ngamanga kutoka Afrika ya kusini akifungua hafla hiyo |
Mkurugenzi wa Hotel ya Miriam akifuatilia hotuba ya ufunguzi |
Baadhi ya washiriki wakiwa katika hafla hiyo |
baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakiungana na Mkurugenzi wa Hotel ya Miriam Njombe Bw Ditram Msemwa wa sita kushoto akiungana na mgeni rasmi Bw Ngamanga kuzindua kitabu cha Jitambue kilichoandikwa na Ngamanga wa katikati , |
Hiki ndicho kitambu cha jitambue |
Mwigizaji maarufu nchini Bw ras katikati akiwa na kitabu hicho Na Matukiodaimablog KIASI cha Tsh milioni 100 zimetumika kusaidia kusomesha familia zenye shida na kutoa mitaji ya Tsh milioni 20 kwa kila kijana mwenye ndoto ya kujiendeleza katika familia ya Msemwa na nje ya wanafamilia hao wilayani Njombe mkoani Njombe. Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika jana katika ukumbi wa Hotel ya Miriam Njombe mkurugenzi wa Hotel ya Miriam Bw Ditram Msemwa alisema kuwa wameanzisha utaratibu huo ambao uliamnza ndani ya familia kwa dhana ya kusaidiana kimaisha ila kwa sasa wameendelea kupanua wigo zaidi kwa kusaidia jamii nyingine ya wana Njombe. "Tilianza kusaiodiana kama familia kwa kupeana mitaji na pesa za kusomesha watoto ila sasa tumepanua wigo kwa kusaidia wengine wa nje ya familia na lengo letu kuona Njombe inakuwa na vijana wasomi wengi zaidi" Hata hivyo wanamapango wa kuanzisha taasisi kamili ambayo itafanya kazi ya kuisaidia jamii ya wana Njombe ili kuondokana na dhana iliyojengeka toka kwa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa hawapendi kurudi kusaidia kwao baada ya kupata nafasi ya uongozi. Pia mkurugenzi huyo alimpongeza mkazi wa Njombe Bw Ngamanga ambae kwa sasa anaishi nchini Afrika ya kusini kwa kuendelea kuwakilisha vema mkoa wa Njombe kwa kutoa elimu kupitia kitabu chake cha jitambue ambacho kimezinduliwa Njombe na kutaka vijana wengine kuiga mfano huo . Kuhusu mitaji inayotolewa alisema kuwa kila mwaka wameweka utaratibu wa kutoa mtaji wa Tsh milioni 20 kwa mtu mmoja ili kufanya biashara pamoja na kusomesha watoto na kuwa toka wameanza mpango huo kiasi cha Tsh milioni 100 zimetolewa . |
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment