Baadhi ya wanavicoba wa Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wakiwa na mabango katika maandamano siku ya uzinduzi wa Vicoba.
Raisi wa Vicoba Tanzania Devotha Likokora (katikati) akiwa na kushoto ni makamu wake Scholastika Kevela wakiongoza maandamano siku ya uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.
Raisi wa Vicoba Tanzania Devotha Likokora akionesha mkasi juu kama ishara ya kutaka kukata utepe wa uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.
Burudani ya ngoma zikitumbuiza katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Green city Makambako mkoani Njombe
Raisi wa Vicoba Tanzania Devotha Likokora akisakata ngoma siku ya uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.
Makamu wa Raisi wa Vicoba Tanzania Scholastika Kevela akipiga chekeche siku ya uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.
Na Blogger wa Njombeyetu, Makambako.
WANANCHI waliojiunga na Vicoba
wameiomba Serikali kutunga Sera na Sheria zinazohusu fedha ili Taasisi hiyo
itambulike na kuendeshwa kitaalamu kwa manufaa ya Watanzania.
Aidha wamesema Serikali
inatakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi ya kujiunga na Vicoba
inayotekeleza Sera ya maisha bora kwa kila Mtanzania ambapo imetakiwa Serikali
kuwawezesha kwa kufuata miongozo ya Taasisi za Fedha.
Mwito huo ulitolewa mwishoni
mwa Wiki na Wanachama wa Vicoba wa Halmashauri ya Mji wa Makambako wakati wa
Uzinduzi wa Vicoba katika Hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Green City
Makambako Mkoani Njombe.
Raisi wa Vicoba Tanzania Devota
Likokora, alisema mbali na Serikali kutambua uwepo wa Vicoba inatakiwa kutunga
Sheria na Sera ili viweze kutambuliwa rasmi katika mifumo ya Fedha kwa
kushirikiana na Wizara ya Fedha, Uwekezaji na Benki kuu.
Likokora alisema Watanzania
wengi wa vipato vya chini ndiyo wanaomiliki na wanachama wa Vicoba na kwamba
mfumo wake ni kwa kila Mwanachama kumiliki uchumi wake pasipo kukatwa riba
kubwa kama taasisi zingine zinavyofanya.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Likokora alisema tangu aanze harakati za kupigania Vicoba Mwaka 2002
wamefikisha idadi ya Wanachama zaidi ya Laki tano wakiwa katika Vikundi 9000
kwa Nchi nzima ambapo kwa sasa limeanzishwa daftari kwa ajili ya kuwatambua
wanachama wote.
Kwa upande wake Makamu wa Raisi
wa Vicoba Tanzania Scholastika Kevela Vicoba vipo kwa ajili ya Wananchi wenye
vipato vya Chini kutokana na wengi wao kutokuwa na uwezo wa kupewa dhamana ya
mikopo katika Mabenki.
Aliongeza kuwa lengo la Vicoba
ni kumwezesha kila mwananchi kupata elimu namna ya kumiliki uchumi wake
mwenyewe ili waweze kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa pasipo
manung’uniko yoyote.
Alisema mara nyingi wananchi
wanashindwa kuchangia shughuli za maendeleo kutokana na kutokuwa na vipato vya
kutosha hivyo kupitia Vicoba kila mwananchi atakuwa tayari kuchangia kutokana
na kuwa na uchumi mzuri.
Katika Uzinduzi huo Jumla ya
Vikundi 12 vinavyounda Mji wa Makambako vilizinduliwa ambavyo ni kikundi cha
Upendo, Twendepamoja, Ujamaa, Chinga group, Mshikamano, Umoja, Mani, Amka,
Ukombozi, Agape, Twitange na Lukelo.
Mratibu wa Vicoba wa Mji wa
Makambako Muhimba Payovela alisema Vicoba vilianzishwa rasmi mwaka 2010 ikiwa
na wanachama 150 na vikundi 13 na lengo lao ikiwa ni kuwaunganisha nguvu na
mawazo ili kuwa na chama cha kuwaletea maendeleo.
Alisema tangu kipindi hicho
idadi ya Wanachama imeongezeka na kufikia wanachama 501 wanawake 401 na wanaume
100 wakiwa na fedha zaidi ya Shilingi Milion 10,800,000 ambapo wameweza
kuwakopesha wanachama zaidi ya 1500 shilingi Milioni 168,930,000 na Milioni 60
zimetengwa kwa ajili ya Elimu na Afya.
Aliongeza kuwa katika Mkopo huo
wamepata faida ya Shilingi Milioni 56,310,000 na Bima ya Shilingi 1,133,300 na
kuongeza kuwa vikundi vingi vinakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na elimu ya
utunzaji wa fedha licha kufanikiwa kuwa na fedha nyingi.
Aidha katika uzindizi huo Raisi wa Vicoba
alifuatana na makamu wake na timu ya wataalamu mbali mbali kutoka makao makuu
ambao ni Mratibu wa michezo na ujasiliamali wa Vicoba Anna Basita, Makundi
maalum Subira Msimbazi, Vijana Vicent Herman Sekta ya ukaguuzi Jojina Chai na
kitengo cha mafunzo mikoani Aidani Bumburu.
Na blogs za mikoa.
Na blogs za mikoa.
0 comments:
Post a Comment