HASSAN MAAJAR TRUST YAKABIDHI MADAWATI 680 KWA RC WA NJOMBE.

 Mkuu wa mkoa wa NjombeKaptain Mstaafu Asseri Msangi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi.  Mkuu wa mkoa wa Njombe Kaptain Mstaafu Asseri Msangi (aliyekaa wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Hassan Majaar Trust Bi. Zena Maajar Tenga (waliosimama wa pili kushoto) na Mwakilishi kutoka Kampuni ya Tigo pamoja na baadhi ya Walimu na Wanafunzi wakiwa katika picha ya ukumbusho. Wanafunzi wakionyesha furaha baada ya kuboreshewa mazingira ya kusoma na Taasisi ya Hassan Maajar Trust ambayo lengo lake ni kutatua tatizo la Madawati nchini na kuhakikisha kauli mbiu yao ya “Dawati kwa kila mwanafunzi” inatim...

MAFUTA YA PETROLI YAADIMIKA MKOANI NJOMBE

Festus Pangani, Njombe Yetu Kwa siku ya tatu sasa mji wa Njombe umekumbwa na adha ya kukosekana kwa nishati ya mafuta ya petroli kwenye vituo vya mafuta hali inayopelekea kukwama kwa usafiri na kushuka kwa uchumi miongoni mwa jamii. Hali hiyo imetokea kuanzia septemba 30 mwezi uliopita hadi sasa ambapo hadi hii leo ni kituo kimoja tu cha mafuta cha Ndime PetrolSstation kinauza mafuta hayo. Wakizungumza na Njombe Yetu kwa nyakati tofauti baadhi ya madereva wa magari na pikipiki mjini Njombe wamesema kuwa adha hiyo imepelekea baadhi ya magari na pikipiki kuzima njiani yakiwa na abiria kitu ambacho kimeleta usumbufu kwa abiria. Kwa upande wao mameneja wa baadhi ya vituo vya mafuta mjini hapa Prosper Mtewelewa wa kituo cha Ndime Petrol Station na Kaimu Meneja wa kituo cha mafuta cha Total...

TANESCO NA MWEKEZAJI KUTOKA MAREKANI KUZALISHA UMEME MEGAWATI 400

Na Festus Pangani, Njombe Yetu Serikali ya Tanzania kupitia shirika la umeme tanesco kwa kushirikiana na mwekezaji kutoka nchini marekani, inajiandaa kutekeleza mradi wa umeme wa maji katika mto ruhuji. Akizungmza wakati wa baraza la madiwani Mpimaji ardhi   mwandamizi wa Tanesco makao makuu Hamis Boby amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwaka 2019 na kuzalisha umeme wa megawati takribani mia tatu hadi mia nne. Boby amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa mgodi kufua  umeme wa megawati 350 hadi 400, bwawa la kuhifadhi maji, bwawa la kuzalisha umeme, njia ya umeme, barabara, njia ya kusafirisha maji chini ya ardhi, ofisI na makazi. Hata hivyo amesema hatua hiyo itazingatia haki za wananchi katika eneo husika kwa kulipwa fidia ya ardhi, kupata huduma...

KATIBU MWENEZI WA CHADEMA MAKETE HASOMEKI......

Mwenyekiti  wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi, katibu wa itikadi na uenezi wa CHADEMA wilayani Makete Bw. Sinene amekifagilia chama cha mapinduzi kwa kusema kuwa kimejitahidi katika mambo yake ikiwemo kuwa na wanachama wengi wilayani hapo kwa zaidi ya asilimia 90 Sinene ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha zake alipoalikwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi wa CCM uliofanyika jana kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani hapo Katibu huyo alisema “nikilinganisha huko nyuma na hii leo kwa kweli chama chenu kimejitahidi kwa zaidi ya asilimia 90, mna wanachama wengi na mnaendelea kufanya mengi” Awali wakati akianza...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa