WANANCHI LUDENDE WALIA UKOSEFU WAHUDUMU WA AFYA.

Festus Pangani, Njombe Yetu BlogWananchi wa Kata ya Ludende wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kushindwa kupeleka wahudumu wa afya katika Zahanati Ludende hali inayosababisha adha kubwa kwa wakazi wa kata hiyo.Pamoja na Zahanati hiyo kufunguliwa wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania mwaka jana lakini hakuna mfanyakazi hata mmoja na kwamba majengo ya zahanati hiyo ikiwa ni pamoja na nyumba ya mganga mkuu vimetelekezwa.Akiongea kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa wananchi hao alisema kuwa haoni sababu ya kuwa na majengo mazuri yaliyojengwa kwa kodi ya wananchi bila ya kuwepo wahudumu wa afya huku wananchi wakiendelea kuumia.Mtendaji wa Kata ya Ludende, Lezile Luoga alikiri kutokuwepo kwa mfanyakazi yeyote...

BARABARA YA NJOMBE-LUDEWA YATENGEWA FEDHA

Festus Pangani, Dodoma Hatimaye Serikali imesikia kilio cha Mbunge wa Ludewa, Mhe. Deo Filikunjombe (CCM) cha kuitaka barabara ya Njombe, kupitia Ludewa hadi Manda ijengwe kwa kiwango cha lami. Akijibu Swali namba 264 bungeni jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Gerson Lwenge, alisema kufuatia ombi la Filikunjombe, katika mwaka huu wa fedha wa 2012/2013, tayari Serikali imetenga shilingi 1,600 millioni kwaajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara hiyo kwaajili ya ujenzi wa kiwango cha lami. “Aidha, katika kuhakikisha barabara ya Ludewa inatengenezwa na kupitika kwa urahisi,” alisema jumla ya shilingi milioni 800 zingine zimetengwa katika bajeti hii ya 2012/2013 kwaajili ya matengenezo maalum ya barabara kuu kwa kiwango cha changarawe.  “Lengo ni kuifanya barabara...

Karibu Mkoa Mpya wa Njombe

Mkoa mpya wa NjombeMkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa mipya Tanzania, ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya na Iringa.Mwaka 2002 katika eneo hilo kulikuwa na wakazi 654,929 [1] katika wilaya zifuatazo: Makete (wakazi 106,061), Njombe (wakazi 420,348), Ludewa (wakazi 128,520).Kutokana na hadhi mpya, wilaya ya Njombe imegawanyika kati ya ile ya mjini na ile ya vijijini. Pia imeanzishwa wilaya ya Wanging'ombe.Makao makuu yako Njombe mjini.Wenyeji wa mkoa ni hasa kati ya makabila yafuatayo: Wabena, Wakinga, Wapangwa, Wawanji, Wakisi na Wamanda....
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa